This time nimekuwa nikifikiria sana, Juu ya hatma ya chama tawala chama chamapinduzi ccm pale nguvu ya uma itakapotumika kukiondoa madarakani. Mimi ni kati ya mamilioni ya watanzania ambao maisha yeto yametobolewa matundu ya risasi za magumu ya maisha, achilia mbali risasi zile zilizotoboa kwenye miili ya ndugu zetu waliotangulia mbele za haki, au risasi silizo piga miili ya wanyonge na kuwasababishia vilema na majeraha ya kudumu. Mrundikano wa madai ya wananchi na jamii kwa ujumla, kesi na malalamiko dhidi ya serikali na chama nijambo ambalo huwa nikilifikiria ninaona kwa taswira ang'avu kabisa jinsi viongozi wa chama tawala na serikali watakavyokuwa katika wakati mgumu kabisa kihistoria barani Afica kukubali kukubaliana na maamuzi ya wananchi ya kubadilisha utawala wa nchi, na hili ndio linadhihirisha wazi kuwa watakuwa tayari kwa gharama yoyote pengine hata kwa kumwaga damu kama kawaida ili kuhakikisha hawakiachii kiti cha kuwa madarakani.
Hii ni kwasababu kitendo cha kubadilisha utawala kitatoa fulsa sawa ya kila mmoja kufidiwa Dosari iliyowekwa kwenye maisha yake kwa haki na usawa, Sasa Hoja yangu ipo hapa; Je Utawala huu utaweza kulipa kila jeraha la mwananchi ambalo imeliweka tangu 1964? Roho za watu waliouwawa na jeshi la polisi zitafidiwa na nini? Kunajinsi ya kumrudishia Dk Ulimboka meno yake aliyopewa na mwenyezi mungu badala ya yale ya wazulu? kama hakuna nini itakuwa fidia stahiki?, Pamoja na kwamba naumia sana na ukatili na unyanyaswaji ambao tumekuwa tukiendelea kufanyiwa, wizi na ubadhilifu ambao tunaendelea kutendewa ila siku zote naamini kila mhusika atalipa, Sio raisi wala waziri wala mbunge, sio jaji wala hakimu, hakuna mkuu wa wilaya wala diwani. Tukishaweka serikali tunayoiamini madarakani kila mmoja lazima atalipa kila nukta ya baya alilotenda. Nani atasalimika......... Mengine sina uhakika huwa nasikia tu, lakini kama ni kweli, babu seya akikata rufaa mchezo mchafu aliochezewa ukabainika, Mh Atapona?
Wananchi tumesha choka, CCm ni lazima itambue kuwa 2015 ni kufa au kuolewa, Either iibe sana kura na kupiga mpaka kuua kila mwananchi na mwanaharakati atakaepigania uchaguzi huru na wahaki kama ilivyodesturi za mataifa yetu ili iendelee kubaki mdarakani, au ikubali kuachia madaraka kidemocrasia na kuanza kulipa na kuwajibika kwa kila tundu la risasi iliyo weka kwenye maisha ya watanzania.
CCM 2015 ni kufa au Kuolewa
Msamiati.