Kila kiongozi analalamika awe rais,waziri mkuu n.k. Kama nchi imewashindeni si mkabidhi kwa wachapa kazi.
Kulalamika katika uongozi ni dalili ya kushindwa.Huwezi kulalamika kama uko sawasawa.
Leo hii ukimuuliza kiongozi,hivi tatizo hili chanzo chake ni nini,jibu atakalokupa utashangaa anasema hata mimi(yeye) hajui,utasikia "Ooh chadema walisema nchi haitatawalika" uvivu wa kufikiri.
Waziri anaulizwa vipi hili tatizo la ajira,jibu ata sema vijana wajiajiri,as if sio waziri.Kusema wajiajiri si hata mchimba kokoto anaweza kusema hivyo? Sasa kkutakuwa na tofauti gani ya waziri na mchimba kokoto?
Nasema hivi,kiongozi anayelalamika juu ya tatizo fulani na hajui/anajua chanzo chake na wananchi analalamika tatizo hilo hilo,lakini kiongozi huyo hachukui hatua huyo ni kiongozi anayeangamiza taifa lake.
Sisi wote tunayashuhudia nchini. Maoni yangu!!