Kifo cha Askofu Mayalla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kifo cha Askofu Mayalla

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mutekanga, Aug 24, 2009.

 1. M

  Mutekanga Member

  #1
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 26, 2007
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Askofu Mayalla, ameaga dunia. Mazishi yake ni Jumatano. Tunasikitika kumpoteza. ingawa wengine wanafurahi maana wamesubiri kiti chake kwa hamu kubwa.

  Tunaomba kanisa lisifanye makosa ya kumpatia Kiti hicho, Askofu Severine NiweMugizi wa jimbo katoliki la Rulenge-Ngara. Kuna sababu nyingi za kumzuia Askofu huyu kuwa Askofu Mkuu. Sababu nyingi na za msingi tulizieleza wakati wa kumsaka Askofu mkuu wa jimbo la Tabora. Mengi halijitokeza hadi mtoto wake Mkunde wa kule Maji ya chai Arusha.

  Sababu mpya ni ile ya ukabila. Wakati wa uchaguzi mdogo wa Biharamulo, Askofu Severine, alihubiri makanisani na kuwashawishi watu wasimchangue Mkukasa, kwa vile si mzaliwa wa Biharamulo. Ukabila kama huo, hauwezi kumruhusu kwenda Mwanza, ambako hakuna wasubi. Kule ni Wasukuma, wakelewe, wajita na mchanganyiko wa makabila mengine mengi.

  Ujumbe huu ni wa watu wa Mwanza na watanzania wenye nia njema, kumkataa kwa nguvu zote Askofu Severine Niwemugizi. Ni bora dunia yote ikafahamu kwamba Askofu huyu ni mkabila.

  Mungu, amlaze mahali pema Askofu Mayala!
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  kaazi kweli kweli, kumbe ni kweli ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, yaani tulikuwa tunajua ubaguzi wa kidini tu, kumbe nae kiongozi wa dini anawabagua wenzie kwa ukabila japo wapo dini moja, nadhani hata kama ni kabila moja hatakubagua kwa koo
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Unafahamu mchakato ambao Kanisa Katoliki hufuata ili kumpata Askofu Mkuu?
   
 4. K

  Kaka Mdogo Member

  #4
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mutekanga, umeleta hoja lakini hukuileta vizuri! Umeshaonyesha jinsi gani unavyompinga Niwemugizi na hoja yako ni kututaka kutupeleka kwenye kumpinga niwemugizi. Lakini nafikirii hii forum haitosaidia sana, ingawa kwa wewe umeshatoa frustration zako. Jimbo la Mwanza lina wenyewe na hata wa kulitawala wanajulikana. Labda kama unampigia debe Niwemugizi kwa jinsi hiyo. Au labda unataka kusema sasa unataka askofu mkuu atoke jimbo la Rulenge au Bukoba. Kwahiyo unataka na wa Musoma waanze kumtaja mtu wao, vile vile na wa Geita, Shinyanga etc. Nafikiri approach yako siyo sahihi na hata sentensi yako ya kwanza kwamba kuna watu wamesubiri kiti hicho kwa hamu kubwa bado siyo sahihi. Kwanza Askofu hakuwa mgonjwa kusema watu walisubiri afe. Amekufa ghafla. Hakuwa mzee wa kusema ukilinganisha na umri wa maaskofu wengi wa kanisa katoliki la Roma na angeweza kuendelea kuongoza jimbo hata akiwa na umri wa miaka 75 au hata 80. Kwahiyo huyo mtu aliyekuwa anatamani hicho kiti angeendelea kumsubiri tu. Au labda useme yeye ndio kamuua.
  Lakini mchakato wa uchaguzi wa askofu kwa wakatoliki unajulikana. Mchakato utaanza na askofu atajulikana. Na wana jimbo la Mwanza wanamjua atakayekuwa askofu wao na wanamzungumza
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Bwana mkubwa mbona hii thread yako imejaa utata na uchochezi vile. Kwani kuna ubaya gani askofu kusema ukweli kuwa Oskar Mukassa si raia?? Ni kweli Oskar Mukassa si raia, ninamfahamu sana!!!! Na anapenda sana kujisifia kuwa ni mganda!!! Nilishangaa mno siku ile kiongozi wa uchaguzi aliposema eti kuwa madai ya uraia ni fitina!!! Kweli Tz tumekwisha!!!

  Oskar aje hapa atueleze kama yeye na wazazi wake wameshaukana uraia wa Uganda!!!! Kama walishaukana na kuomba uraia Tz basi nitanyamaza kimya. Oskar unanisikia??
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Nafikiri hafahamu.It will take time kumpata askofu pale hasa ukizingatia kuwa alikufa ghafla na hawakuwa na clue!!! The process itself balaaaa. Mleta mada aulize aambiwe!
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,327
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Hii mesage yako imeniacha mdomo wazi. Ninavyojua ni kuwa uchaguzi wa askofu anaufanya papa na sio mtu mwingine. Inawezekana baadhi ya wakuu wa kanisa kutoa recommendation ila decision ya mwisho ni ya papa mwenyewe.
  Tukumbuke pia, ni wajibu wetu kuomba mapenzi ya mungu yatimizwe na sio mapenzi ya binadamu. Mi naona ungelitendea vema kanisa kama ungehamasisha watu tuliombee lipate viongozi bora.
  Kama kweli kuna watu walikuwa wananyemelea kiti chake basi ninajiuliza kuna biashara gani kwenye kanisa badala ya kutoa huduma?Au kuna waliokuwa wanabebwa na marehemu wanaogopa kupoteza maslahi yao?
  Kwangu mimi, naiombea roho ya marehemu Askofu Mayala mipumzike vema peponi. Haya mengine ya nani atakuwa nani, naomba mungu ayashughulikie maana najua sitaulizwa na yeyote opinion yangu.
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,327
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Pengine aliyetoa mada ana analolificha maana sijamuelewa kabisa. au kuna makundi yaliyopoteza maslahi kwa kifo cha Askofu nini? Au ndo kumpigia debe kiaina huyo askofu anayemtaja?
  Lakini Askofu mkuu sio lazima toke mwanza.anaweza kutoka popote. Askofu Mgulunde alikuwa mtu wa Iringa akahamishiwa Tabora, Yule Mwalunyungu alikuwa Tunduru Masasi ingawa ni mhehe na list goes on.Mi sioni anachokiogopa nini?
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  kimsingi ni hivi!
  mchakato huwa ni mrefu sana, kuna mapendekezo ambyo huwa yanatoka kwa maaskofu then yanakwenda vatikani kwa papa.lakini papa ndo msemaji wa mwisho.
  alichokisema huyu jamaa kina ukweli flani ila sema kakosea namna ya kukiweka.kuna mapadre wenye uchu na kupata uaskofu tena sana. mi nakumbuka wakati niko seminari kulikuwa na mapadre wanapiga jaramba ya namna ya kutembea na fimbo wakai wa mchakato wa kumpata askofu wa jimbo la geita. papa aliwaacha midomo wazi akateua mwingine kabisa DAmian dennis dallu, akiwa na miaka 42 tu. kwa jimbo la mwamza toa nihame nchini kulikwa na mapadre wenye sifa wachache kama vile pd Bilingi. kuna wengine waliingia wito wa upader kama kimbilio la wakosefu na hawa ndo huwa wasumbufu sana
   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kama hizi ndizo infighting za kanisani bora hata mie ninayetumia Jumapili zangu kusoma magazeti na kuangalia TV, walks around the hood etc kuliko kwenda kanisani.

  Kanisani kunakuwa na infighting utafikiri uongozi wa Yanga? Hata uongozi wa Yanga afadhali.
   
 11. S

  Simon Marandu New Member

  #11
  Aug 24, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusimpinge sana mtoa hoja kwani mambo hayako wazi sana, uovu upo hata kanisani. Kuwa askofu hakumaanishi kuwa huyu ni mcha mungu sana. Naye hana ubinadamu wake, ambao waliokaribu kama mtoa hoja wameona. Huyu askofu amekuwa akilalamikiwa sana siku nyingi. Tujitahadhari.
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wakuu JF haihusiani kabisa na uteuzi wa askofu Mkuu Mwanza, Kanisa katoliki lina autonomy yake ya kupata viongozi wake. Mnajaza thread tu hapa sijui askofu wa Rulenge hafai mnajichosha tu....Papa anaweza teuwa padri wa Tunduru kuwa askofu. Sijui mtaandamana.....
   
 13. M

  Mutekanga Member

  #13
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 26, 2007
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnanishangaza! Kana kwamba mnaishi mwezini? Hakuna cha roho mtakatifu wala Papa. Uchaguzi wa maaskofu ni siasa kama siasa za kawaida. Ni kweli kwamba Askofu Mayala, alikuwa mgonjwa siku nyingi.Watu wamekuwa wakiiangalia kiti chake kwa hamu. Mbona hili ni jambo la kawaida? Hata kule Geita, yule Askofu, alichaguliwa kwa vila alikuwa na ujamaa na Mgurunde.Ukweli ndo huo!

  Askofu Severine Niwemugizi, amekuwa kisubiri kuwa Askofu Mkuu na pengine Papa. Huyu ni mtu mwenye tamaa na uchu wa madaraka. Mtashanga kusikia anateuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Mwanza. Kama mnafikilia Msonganzila, mmeotea njia. Labda angekuwa Balina, ila na yeye anaumwa! Ukweli ndo huo. Kwanini wasiumwe? Wanaishi dunia hii na maisha yao ni sawa na ya kwetu!
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Acha ulongo na pumba hapa wewe...!
   
 15. M

  MC JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mutekanga,

  Hili jina limekaa ki Karagwe karagwe, Je wewe ni Padri Karugendo? Kama siyo lazima mnacommunicate believe me or not?

  Anyway, nikuunge mkono, kwamba kama yaliyosemwa nyuma na Karugendo ni ya kweli basi Niwemugizi hastahili hata huko aliko!
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Una post 13 tu mkubwa lakini mambo yako ni makubwa .
  Niwemugize naweza kumpinga kuwa Askfu wa jimbo kwa sababu zingine lakini si Mukasa , wewe labda na CCM wenzako mliumia .Hata hivyo Askofu hachaguliwi na JF , andika kwa Pengo ambaye naamini hatakuelewa na hasa akiwepo Kilaini, then kwa Mjumbe wa Pope pale Dar .
   
 17. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280

  Pole pole MC. Ni kweli chuki anazoonyesha Mute zinashabihiana sana na chuki anazoonyesha Privatus Karugendo kwa askofu Niwegumizi.

  Mmmhh! Kazi kweli kweli.

  NB: Sijaribu kuingilia vita ya huko Kagera. Mimi kwetu nyumbi i bombi i.
   
 18. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Unamuweka wapi Fr. Nkwande huyu jamaa anafaa sana na alikuwa karibu sana na Marehemu Mayalla huyu ndo atachukua kiti lakini tumuachie mwenyewe Papa.
   
 19. O

  Omumura JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
   
 20. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Turudi kwenye mada, nani wanahudhuria mazishi yake? kiongozi gani atakuwa MWanza? Waraka wa Wakatoliki utaguswa huko?
   
Loading...