Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,482
Posted on April 25, 2012 by www.mzalendo.net
Kamishna Ali Abadalla kushoto akiangalia kifaa kipya cha kuzimia moto kijulikanacho kama DSPA 5 kutoka kwa askari wa kikosi cha Zima Moto na Uokozi katika hafla ya uzinduzi wa kifaa hicho hapo Maisara Mjini Zanzibar
KIKOSI Cha Zima Moto na Uokozi Zanzibar jana kimezindua kifaa kipya cha kisasa cha kuzimia moto kisichotumia maji kiitwacho Dry Sprinkler Powder Aerosol (DSPA5). Kifaa hicho ambacho huzima moto ndani ya dakika mbili baada ya ya kutumbuliwa nyuzi zake kwa kwa sekunde nane kina uwezo wa kutumika na kudumu kwa miaka 15 bila kuharibika bada ya kukinunua. Uzinduzi wa kifaa hicho umefanyika Maisara Mjini Zanzibar mbele ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Issa Haji Ussi pamoja na makamanda mbali mbali wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na makamishina kutoka vikosi vyote.
Ussi alisema kupatikana kwa kifaa hicho kutasaidia kwa kisi kikubwa majanga ya moto yanayotokea hapa Zanzibar hasa kwa kuzingatia magari ya zima moto yaliopo ni kidogo na hayakidhi haja kutokana na ukumbwa wa mahitaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ‘Your Solution Tanzania LTD' ambayo imeshirikiana na AFG Group ya Uholanzi, Damian George akitoa ufafanuzi wa kifaa hicho cha DSPA alisema kuwa lengo hasa la kifaa hicho ni kuwaonesha wazanzibari na watanzania namna ya kukitumia.
Alisema DSPA ni muhimu kutumika pale inapokea janga la moto ambapo hutumika kwa kuzima moto bila ya kutumia maji ya aina yoyote na kinapofunguliwa huzima moto unaowaka.
Akiwatoa wasiwasi watu walifika kushuhudia kifaa hicho na maafisa wa serikali na vikosi vya SMZ, George alisema DSPA ni teknolojia ya kisasa ambayo haina madhara yoyote ya kiafya wakati wa uzimaji moto hata pale mtu atakapokuwa yupo ndani wakati wa uzimaji wa moto huo.
George alisema kifaa hicho kwa nchi za Afrika, Tanzania imekuwa nchi ya kwaza kufika ambacho huzima moto kwenye chumba chenye ukubwa wa mita 100 za mraba kwa DSPA 5 moja yenye uzito wa kilo moja ambapo uwezo wake wa kufanya kazi ni mkubwa na huchukua muda wa miaka 15 bila ya kuharibika.
Akitoa shukrani katika uzinduzi huo Kamishina wa kikosi hicho, Ali Abdalla alisema amefurahi sana kuwa kifaa hicho kimekuja wakati muafaka na ni njia mbadala ya kuzimia moto baada ya magari ya kawaida kutumika hapa Zanzibar.
Alisema kutokana na kuwepo kwa matukio mbali mbali ya kuwaka kwa majengo ya Serikali, taasisi za kijamii na hata baadhi ya nyumba za makaazi ya watu binafsi hivyo kifaa hicho kitakuwa muokozi wa maafa hayo iwapo yatatokea kwa sasa.
Amesema Zanzibar ni Taifa linalohitaji mabadiliko ya kidunia ili kwenda sambamba na dhana za kisasa za uokozi pale ambapo pametokea janga la moto na kwamba hakuna budi kupambana nalo bila ya kuleta maafa mengine kwa jamii na nchi.
"Ni matumaini yetu kwamba kifaa hiki kitatumika vizuri, ni kifaa muhimu kwani hakitumii maji kitasaidia kwa kiasi kikubwa nchini kwetu kwani sisi ni sehemu ya dunia" alisema Kameshina Abdalla.
Kamishna huyo alisema Zanzibar ambayo imekubwa na tatizo kubwa la maji na ukosefu wa magari ya kuzimia moto majanga yanapotokea kifaa hicho kitasaidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma hiyo ambayo haitahitaji kupatikana kwa maji.