Kidono/Kinkuti ni kitu gani?

Kidono/Kinkuti ni kitu gani?

Peaa chanzo cha matatizo. Mimi napenda zitakazonikidhi mahitaj yangu, ndugu zangu na wenye kuhitaji msaada
JOKES ASIDE!

Pesa yoyote inayokutoa kwenye matendo ya kawaida ya kibinadamu!
IKIMBIE mwanangu!
 
Kidono ni kinga ya kuzuwia kujeruhiwa na silaha zenye ncha kali kama panga, kisu, shoka, jembe,mkuki, sime, mundu nk. Kinga hii ni maarufu sana huko Kigoma na imekua ni kama moja ya jadi ya watu wa huko. Wao husema kuwa ni aibu kwa mtu wa huko kufa kwa kisu au panga nk. Kuna vidono nya aina nyingi ukianzia nilicho taja hapo juu yaani hiyo ni basic/cha msingi ambacho wengi wanacho na wanakijua na pia ukubwa wa kidono huenda juu zaidi kama Kidono cha Risasi/Bomu, Kidono cha Ajali mapala Kidono Cha sumu. ingawa ukitaja kidono wengi hufikiri hicho cha msingi cha visu lakini huwa mchanganyo wake unaongezeka kadiri ya utaalamu. Kipo kodono hata sindano hospitali haiingii mpaka mgonjwa atoe ruhusa. Njia ya kupata chanjo hiyo zipo nyingi kuanzia kuchanja na shoka,kisu, wembe kn, kunywa, au kuchimbiwa. Elimu hii ima mengi sana. Huko zipo mpaka kinga za magonjwa ya zinaa.Huko zipo hata zile za kutafuna chupa au wembe.
Kinkuti/kinguti hii ni dawa ya nguvu za kupigana. Hii huwa na mchanganyo wa mifupa ya wanyama kama tembo,simba,sokwe,mamba,faru,Gorila mpaka chatu. lakini iliyo maarufu ni ile ya gorila. Hii hufanya kazi pindi mtu anapo chokozwa au kuvamiwa na vibaka. unaweza kupiga watu mpaka wakaomba poo, unapo chokozwa mtu huwa kama kapandisha mapepo na ukichaa flani na hapo unakua na nguvu za ajabu na hukamatiki. Ili upoa unalazi ika kuwa na mtu anaye jua siri ya kukupoza kama kuvuta nywele za kati ya kuchwa au kukumwagia mkaa au majibu kisogoni kn. Dawa hii imua adimu sana au kupoteza ufanisi kutokamna na uadimu wa kupata mchanganyo wake kwakua inatumia sana wanyama walio hatarini kutoweka dunianai na wanao lindwa kwa sheria kali. Hivyo imekua ngumu kupata mchangavyo gradeA. lakini zipo za miti pia na kila mtaalamu anajua option zake ili kudhibiti ubora wa akzi yake. Mtu mwenye Kidono na Kinkuti manaake huyo haduliki kwa silaha na wakati huo anapiga balaa so unapigwa na panga lako mkononi.
Kwa kifupi mambo yako hivyo na hiyo ndio maana ya Kidono hasa cha Waha wa huko Kigoma.
Aiseee!
 
Swali la kizushi!
unaweza kuwa una Kinkuti bila kujijua!
yani katika kumbukumbu zako hukumbuki kuwa ulishawahi kuchanjwa popote!
wala kufukiwa popote!
But una nguvu za ajabu inapotokea umekasirika!
Da'Vinci na wengine shule kidogo hapa!
Son remember the other day kulikuwa na uzi wa vifo vya mastaa and the like tukadivert kwenye issue ya reactions za hasira na kujizuia kudhuru mtu au watu hence unajizuia kukasirika?
 
Swali la kizushi!
unaweza kuwa una Kinkuti bila kujijua!
yani katika kumbukumbu zako hukumbuki kuwa ulishawahi kuchanjwa popote!
wala kufukiwa popote!
But una nguvu za ajabu inapotokea umekasirika!
Ndio ila hicho hakiwi kinkuti wala kidono. Ni Mungu anakua kaku Gift.. Ndio unakua mutant..
Mfano MTU mwenye mfupa mmoja hua ananguvu sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom