Kidonda kwenye Uume

Ikena

JF-Expert Member
Oct 24, 2007
553
393
Wakuu naomba mumsaidie mdogo wangu anasumbuliwa na kidonda kwenye kichwa cha uume.

Kilianza kama ngozi iliyobabuka au fungus, kukojoe huku anasikia raha na muwasho, lakini sasa kuna kidonda kwenye kichwa na hawezi kuvaa nguo yeyote sasa.

Tafadhali naombeni matibabu yake ili nikamsaidie.

Alienda hospitali akapimwa damu na mkojo, dr akamwambia hana maambukizi yeyote hata kaswende ambayo dr alidhani, haikuwepo.

Alipewa Ampiclixilian na dawa ya kupaka, ila mpka sasa siku ya tatu, kidonda kinazidi kutkua na kutoa maji na usaa.
 
Kwanini usimpeleke Hospitali nyingine kwa ajili ya uchunguzi maalum?
 
Nadhani nae pia ilimuanza hasa baada ya kunywa dawa za maleria, kwani anakama siku ya 7, tangu anywe, japo sina uhakika kama iyo inaweza kuwa sababu.

Naendelea kusubiri ushauri wenu.
 
Hahaaaaaa mambo ya kavu hayo.. Hiyo ni syphilis kudadadekiiiii chezea kona bar wewe
 
Hakikisha unampeleka hospitali wafanye kipimo inaitwa kalicha, yaani waoteshe vimelea wa vidudu na kisha wa test dawa inayoweza kumtibu.

Ni wewe nini Kaka, usirudie tena ngono. Kuwa na mpenzi mmoja a.k.a mchumba ambaye utamuoa. Usione demu anapendeza ndani kumeoza.
 
Alitumia dawa ya malafini. Wakuu dawa gani ya kukausha kidonda?
 
Wakuu naomba mumsaidie mdogo wangu anasumbuliwa na kidonda kwenye kichwa cha uume.

Kilianza kama ngozi iliyobabuka au fungus , kukojoe huku anasikia raha na muwasho,lakini sasa kuna kidonda kwenye kichwa na hawezi kuvaa nguo yeyote sasa...

Mpeleke Hospital ya Rufaa haraka sana
 
pole sana mpaka unaamua kuandika humu inaonekana ni jinsi gani ugonjwa wa mdogo wako unavyookuumiza, cloxa ni miongoni mwa dawa za kukausha vidonda.

unawezapata ushauri wa kitaalamu, dose, gani atumia kutoka kwenye pharmacy yenye wataalamu kwasababu hujataja umri wake,ila ushauri wangu akafanye vipimo zaidi ili aepuke kutibiwa kwa kubahatisha,pia wazo aliotoa mdau la kufanya kipimo kinachoitwa culture ni zuri,atapata uhakika wa dawa ya kumtibu.mpeleke hospitali kubwa haraka kwani inawezakumletea madhara katika mfumo wa uzazi! Pole sana!
 
Tumia tiba mbadala zile ambazo wanapima mifumo yote ya mwili kwa computer na kutoa sumu mwilini na kutumia vijalizo vya lishe (food supplements) badala ya dawa za kemikali. Na kama uko Dar nenda WAPO redio Kurasini pia wana matawi Mbezi Beach Samaki na Kimara Mwisho. Mimi walinisaidia sana mwaka jana, ingawa tatizo langu lilikuwa tofauti kabisa na la dogo. Mpe pole sana dogo.
 
Nilishasikia case kama hii, kuwa na kidonda bila kuwa na ugonjwa wa zinaa. Muambie anunue broad spectrum antibiotic ya kupaka aone kama itakauka. Otherwise mtaftie 'urologist' amuone asije akakatwa nanilii bure akastaafu kilimo kwanza kwa manufaa ya umma.
 
ikena vipi tena mambo ya mdogo wako vipi, ni wewe mkuu usijali, kwa sababu umetumia dawa ya malaria angalia kama ina sulfur inaweza kukuletea allege, hatua ya kwanza tumia maziwa fresh ili kuditoxify sumu mwilini, halatu tumia deto ya maji ukipata ni nzuri kwa kuoshea vidonda, pole sana
 
Chukua mmea wa Aloevera kamulia hapo yale maji maji yake kwa siku tatu,utaona mabadiliko!!

Septrin pia ni dawa nzuri kwa serious infection kama hiyo!
 
Back
Top Bottom