Nina makovu yaliyobaki kwenye kichwa cha uume

Status
Not open for further replies.

Future Bill

New Member
Sep 28, 2023
2
5
Habari zenu, natumaini wote ni wazima. Ninaomba mawazo yenu juu ya swala langu.

Mwishoni mwa mwezi wa name nilianza kupata vipele mfano wa malengelenge katikati ya vidole vya miguuni, upele ulivyokua unaanza haukua na muwasho lakini baada ya siku kadhaa muwasho ukaanza haswa wakati wa usiku, vipele vikasambaa na mikononi pia katikati ya vidole, na kimoja kikatoka kwenye kichwa cha uume, sikukigundua kwasababu hakikua na maumivu ila muwasho ulikuwepo kwenye uume ndo ulifanya nije kukiona.

Kuna siku moja nilienda kukojoa nikahisi maumivu, ikanibidi niende dispensery siku hiyohiyo nikapimwa na kukutwa na UTI maumivu yale yalikata lakini siku hiyo hiyo bila hata kuanza kutumia dawa.

Baada ya muwasho kuendelea kua mkali ikabidi niende hosp tena kumuelezea doc kuhusu vipele akaniandikia antibiotics na dawa ya kupaka pamoja na sabuni ya kuogea. Naweza kusema vilinisaidia kidogo kukausha vipele ila sio kupunguza muwasho mwilini na vipele japo kua vilikua vinakauka viliendelea kutoka.

Nilienda hosp tena kuhusu kipele cha kwenye uume maana kilikua kinanipa wasiwasi kwasababu hakiumi kipo tu ila kinatoa maji kikipasuka ila hakikutengeza kidonda. Nikapima HIV, kipimo cha damu pamoja na Syphilis lakini vyote vikawa negative. Kipele kilikua kimeshaanza kupona sijajua ni kwasababu ya antibiotics au ni ile cream ya kupaka.

Baada ya siku kadhaa tu kikauka na kuweka gamba juu ambalo nililitoa na ndo imebaki sehemu ya ngozi iliyonyanyuka ni kama kovu kama mtavyoona kwenye picha.

Naombeni kujua inaweza kua ni nini hii au nawezaje kuondoa kovu. Kuna doctor Regency hosp alinambia hii ni Scabies Kuna maktari wengine wa hosp nyingine hawakunambia ni nini ila walinipa dawa acyclovir ambazo hazijanisaidia chochote kwenye kupunguza muwasho wala vipele sehemu nyingine, ila nimeanza kutumia scaboma jumatatu iliyopita.

View attachment 2765547View attachment 2765548View attachment 2765549
 
Mkuu hicho kichwa hakijapona...Kipeleke hospitali ukamuonyeshe Daktari, usifiche - unaonekana uligonga sehemu mbaya. Kuwa Makini sana Mkuu....Hao watu wa Kimboka, Kona Bar, Kitambaa Cheupe na maeneo mengine kama hayo - usiwe unawaamini sana na kucheza pekupeku.
 
Hofu na kunywea kwa uume vinahusiana:D,pole sana.Pima kipimo kinaitwa VDRL,pamoja na kuwa umeshapima vingine,then baada ya hapo onana na Daktari akushauri utumie dawa gani,inaweza kuwa ni alergy ya kitu flani ambacho umeanza kula siku za hivi karibuni...
 
Kama umeanza scaboma uunapona soon ondoa shaka zingatia kupaka iyo scaboma aliuguwa mdog angu dushe ilikuwa kama inataka kukatika alikuwa anawashwa usiku adi huruma adi anaruk ruka
 
Hofu na kunywea kwa uume vinahusiana:D,pole sana.Pima kipimo kinaitwa VDRL,pamoja na kuwa umeshapima vingine,then baada ya hapo onana na Daktari akushauri utumie dawa gani,inaweza kuwa ni alergy ya kitu flani ambacho umeanza kula siku za hivi karibuni...
Niliwaza kama wewe kuhusu allergy.
Kama kapima magonjwa ya zinaa Hana. Akamuone daktari wa magonjwa ya ngozi pia.
 
Mkuu pole Sanaa ,mm vilinitokeaa km hvyo hvyo na Kwenye mapaja .nilitumiaa dawa vikagomaa ,Dem mmoja nikamwelezea akaniambiaa nitumiee sabun ya family kuogeaa na baada ya kuoga nijipake mwili wt na Kwenye kichwa Cha mboo nilifanya hvyo wiki nikaponaa kbs na uumee ukaanza kusimama imara maana ulipoteza nguvu,,,jaribu na ww sabun ya family mkuu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom