Kicheko free

IrDA

JF-Expert Member
Aug 26, 2010
743
350
Machungwa ngumi
Mwalimu alikuwa akiwafundisha watoto wa darasa la kwanza kwa vitendo, alianza kwa kuwafundisha kuhesabu vitu kwa kuonesha vidole viwili. "Haya machungwa mangapi?"
"Machungwa mawili"

"Na machungwa haya?" Aliuonesha vidole vinne.
"Machungwa manne"
Mwalimu alikunja ngumi akimaanisha vidole vitano na kuuliza.

"Na machungwa haya yatakuwa mangapi?"
"Machungwa ngumi."
Mwalimu alibakia kimywa wazi asiamini alichokisikia kwa wanafunzi mwake.

Mgonjwa amshtukia muuza majeneza
Kuna mgonjwa mmoja alilazwa hospitalini, alipelekwa akiwa mahututi asiyetambua mtu anayeingia na anayetoka.

Baada ya kupata nafuu aliweza kuwaona wanaoingia na wanaotoka. Siku moja alimuona jamaa mmoja aliyekuwa akifanya kazi ya kutengeneza majeneza na kuyauza.

Jamaa alipomuona alikosa raha kwa kuamini kuwa haingii hospitalini kutazama wagonjwa, bali kuwaombea mabaya ili wafe auze majeneza yake.

Kila alipomuona alikosa raha lakini kusema alishindwa, ili kufikisha ujumbe aligoma kumeza dawa. Ilibidi aitwe daktari ambaye alikuwa akimuhudumia tangu alipolazwa.

Daktari: Vipi ndugu yangu, kulikoni kugoma kumeza dawa?
Mgonjwa: Kumeza dawa hakuna maana yoyote kama mnaruhusu wauza majeneza waingie wodini ili kutuombea dua baya tufe wauze majeneza yao, unafikiri hapo dawa itakuwa na nguvu kweli?

Kauli ile iliwafanya wote waliomzunguka wacheke kimoyomoyo kuogopa kumuudhi mgonjwa. Mmh, kweli uhai mtamu!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom