Kichekesho cha siasa za Ugozi Zanzibar

Kichekesho cha siasa za Ugozi Zanzibar

Kuzunguka kama pia ni kwa kule kwetu ZNZ ni Neno ambalo hutumika kwa kumtanabahisha mtu anafanya/anaongea kitu kile kwa kujirejea sasa sijui wapi nimekuvunjia staha.Tuje historia ya mapinduzi na huko kwa bamkwe mimi babu yangu mzalia baba ni mtumbatu na alikuwa akiuza nyama marikiti darajani pale...na unajua wakati wa alfajiri wanaenda pale na habari za mapinduzi alizisikia wakati yupo marikiti na alikuwa ni HIZBU mkubwa sana alienda kutolewa kwenda masanduku ya kuhifadhia nyama alikojificha na hakuiona familia yake kwa miaka 4. Sasa hizo historia ya ba mkwe na mapinduzi Nimezipata kutoka kwake..lakini hii leo ukiniuliza je ninayakubali mabadiliko yale.. basi jibu langu ndiyo hasa ukizingatia jamii ya kizanzibar iliyokuwa wakati ile basi mabadiliko yalikuwa ni ya lazima ijapokuwa babu yangu alikuwa ni victim wa mabadiliko yale. I'm sorry ya kuwa kuna watu hawana hatia walikufa na wengine wakafungwa na wengine wakakimbia nchi yao. Ukija kuhusu ubaguzi wa uchotara, mama yangu binafsi ni chotara na yeye ni mpemba wa ziwani na mkanyageni..kwa hivyo siongei haya kutokana na chuki yangu binafsi ya machotara au vp. Ubaguzi wa rangi znz upo na utaendelea kuwepo kwani watu wanajisifia Zaidi makabila ya babu zao.. (pengine ni 1/8 ni muarabu) kuliko uzanzibar wao na hao wanajiona wao wako noble Zaidi kuliko watu wengine.Na tuje ubaguzi mwengine wa upemba na uunguja huu watu wanafikiria umeenza baada ya vyama vingi but kusema kweli huu ubaguzi upo tangu zamani na nimeweza kuuushuhudia tangu nikiwa mdogo kwani kuna kipindi Fulani nililelewa na babu/bibi kwa mama yangu. Na mpaka 1995 nilikuwa mfuasi mzuri wa CUF mpaka ilipotokea event moja kuanzia hapo nikaona hichi chama hakifai kwa wazanzibar kwani ilikuwamanifestation yake ni Pembas movement na hao wengine wote ambao si wapemba just si wasindikizaji tu na siyo priority. Kwa hivyo kama unataka kuongelea suala la ubaguzi znz usisome kwenye magazeti au kuangalia vyombo vya habari nenda znz na kaa na ile jamii ya kizanzibari na utaona jinsi gani ubaguzi unavyoivuruga nchi.. tena kwa pande zote mbili... na ndiyo maana mimi ni muumini mkubwa wa muungano kwanibila ya muungano znz ni somali
Kizibao,
Umekuja na mengine kabisa na mimi nakushukuru kwa hilo.
Mimi kama wewe napenda muungano kwani umoja una faida nyingi sana.

Kuhusu kuja Zanzibar mie sina haja ya kuja.
Zanzibar ni kwetu pia yaani ''second home.''

Hili sikuanza mimi.

Baba yangu alikuwa rafiki mkubwa wa Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala katika
1950s wakati huo wote ni vijana.

Mimi nina marafiki-ndugu Zanzibar.

Nadhani tumeelewana.
 
Jingalao,
Mwaka wa 2011 nilishiriki katika kipindi cha Meza ya Duara kinachoendeshwa na
Sauti ya Ujerumani.

Washiriki wengine wenzangu walikuwa Salehe Feruzi wa CCM Zanzibar, Ahmed Rajab (London),
Dr. Harith Ghassany (Washington DC) na mimi nikizungumza kutoka Tanga.

Mwenyekiti alikuwa Othman Miraj kutoka Bonn aliyetuunganisha kwa simu.

Nilimwambia Salehe Feruzi hayo niliyoeleza hapa kuwa CCM Zanzibar hawajapatapo kushinda
uchaguzi.

Bwana Feruzi akaniomba ushahidi kama unavyoniomba wewe hii leo.
Nikamwambia kuwa inasikitisha kuwa yeye kiongozi wa juu wa CCM Zanzibar lakini hajui hilo.

Nikamuongozea kitu kingine.

Nikamwambia kuwa CCM Zanzibar wanaogopa uchaguzi na nikamweleza yale wanayofanya
kuwazuia wafuasi wa CUF kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.

Baada ya haya ndipo nikamkumbusha barua ya Ali Ameir katika uchaguzi wa mwaka wa 1995
baada ya CCM kushindwa waliyakataa matokeo.

Haya yote niliyosema hapa ni kweli wala si ushabiki.
Tujadili haya kabla hatujakwenda mbele katika chaguzi zilizofuatia.
Nilikuuliza swali kuhusu kuitwa mchochezi hujalijibu!
Nimekueleza kuwa mamlaka ya kumtaja mshindi wa Zanzibar ni nani hujaongekea hilo....ukikamatwa kwa uchochezi utakuwa umeonewa?

Mimi sikulazimishi wewe kusema kuwa CUF imeshinda ...lakini ninachohoji ni nani aliyethibitisha hilo?

Ili mada yako ya ubaguzi ijadiliwe kwa muktadha wa uwazi na ukweli na bila kujali itikadi ni vyema ukaondoa huo msimamo wa CCM kushindwa Zanzibar kwa kuwa hatuna matokeo ya uchaguzi hadi sasa...unapoendelea kuwa mshabiki wa msimamo huo unatoa fursa kwa mwanaccm au yoyote ambaye ni mchangiaji huru kuchukua upande kwenye swala hili ambalo naliona ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa.

Unategemea mwanaccm anayepinga ubaguzi achangie kwa uhuru ilhali umeshaweka msimamo wako kisiasa??

Kama lengo lako ni kujadili ubaguzi bila kujali itikadi za kisiasa huna budi kufuta kipengele cha CCM HAIJASHINDA ZANZIBAR...ni rahisi sana kama kweli wewe ni msomi...

CCM kuogopa uchaguzi Zanzibar haimaanishi kuwa wanashindwa katika uchaguzi!!

Futa hiko kipengele au badilisha na kusema kwa mujibu wa CUF au kwa mujibu wako tujue msimamo wako!!

Tambua kwamba hata mimi nina nasaba na undugu huko Zanzibar na Oman pia!
 
Uchaguzi wa Zanzibar unarudiwa kwa sababu uliharibiwa...na walioharibu kwa maslahi yao ndio hao wasiotaka kurudia simply kwa sababu wanajua chance ya kuuharibu tena haipo!
Mwenye uwezo wa kuharibu uchaguzi Tanzania ni chama dola tu.
Kwa nini mliuharibu?
Kura hazikutosha?
Kwa nini mara hii Jecha alishindwa kumtangaza Dr. Shein kuwa Mshindi?

Wakiwabagua wasio wazanzibar hatuoni hizi hekaya lakini wanapoanza kubaguana wao kwa wao ati mmatumbi wa Tanganyika anatafuta angle na kuanza kubweka.

Ubaguzi Zanzibar uko kwenye damu wala siyo kwenye hayo mabango ya wanasiasa labda kama mnawalaumu hao vijana kwa kuionesha dunia nzima kilichoko kisiwani.

Hata hao machotara mnaotaka kutuaminisha kwamba wanabaguliwa wao pekee yao ukichangamana nao wewe na kisogo chako chenye ncha ya mkuki watakubagua tu.

Tuupinge ubaguzi kwa sababu hatuupendi siyo kwa sababu za kisiasa tu.

Mkuu, nimeipenda sana hii.
 
..tatizo ni ccm kutokuwa na guarantee ya kura zenu.

..akiibuka kiongozi wa upinzani toka kanda nyingine utasikia nao wanaanza kubaguliwa.

Pumba tupu! Kama mmekosa hoja zenye mashiko kaeni kimya acheni kujidhalilisha!
 
..tatizo ni ccm kutokuwa na guarantee ya kura zenu.

..akiibuka kiongozi wa upinzani toka kanda nyingine utasikia nao wanaanza kubaguliwa.

Pumba tupu! Kama mmekosa hoja zenye mashiko kaeni kimya acheni kujidhalilisha!
 
Nilikuuliza swali kuhusu kuitwa mchochezi hujalijibu!
Nimekueleza kuwa mamlaka ya kumtaja mshindi wa Zanzibar ni nani hujaongekea hilo....ukikamatwa kwa uchochezi utakuwa umeonewa?

Mimi sikulazimishi wewe kusema kuwa CUF imeshinda ...lakini ninachohoji ni nani aliyethibitisha hilo?

Ili mada yako ya ubaguzi ijadiliwe kwa muktadha wa uwazi na ukweli na bila kujali itikadi ni vyema ukaondoa huo msimamo wa CCM kushindwa Zanzibar kwa kuwa hatuna matokeo ya uchaguzi hadi sasa...unapoendelea kuwa mshabiki wa msimamo huo unatoa fursa kwa mwanaccm au yoyote ambaye ni mchangiaji huru kuchukua upande kwenye swala hili ambalo naliona ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa.

Unategemea mwanaccm anayepinga ubaguzi achangie kwa uhuru ilhali umeshaweka msimamo wako kisiasa??

Kama lengo lako ni kujadili ubaguzi bila kujali itikadi za kisiasa huna budi kufuta kipengele cha CCM HAIJASHINDA ZANZIBAR...ni rahisi sana kama kweli wewe ni msomi...

CCM kuogopa uchaguzi Zanzibar haimaanishi kuwa wanashindwa katika uchaguzi!!

Futa hiko kipengele au badilisha na kusema kwa mujibu wa CUF au kwa mujibu wako tujue msimamo wako!!

Tambua kwamba hata mimi nina nasaba na undugu huko Zanzibar na Oman pia!
Jingalao,
Niwie radhi kuhusu ''uchochezi.''
Nilijibu swali hilo katika bandiko langu huko nyuma.

Inaelekea limekupita.
Itapendeza ukiwa unasoma na post za nyuma hii itakusaidia kutojirudia.

Jibu langu liko hapo chini:
Kizibao,
Tunaweza tukajadiliana kwa heshima ikiwa tutatumia lugha za staha.
Ukianza mjadala kwa lugha za ''pia,'' hatutofika mbali.

Nakushukuru kwa kunifahamisha kuwa kuna ''Machotara Hizbu,'' na
''Machotara,'' wengineo.

Hili sikupata kulijua kabla.
Hayo mengine ulosema sina ujuzi kwa hiyo nitawaachie wengine wachangie.

Kuhusu uchochezi nitashukuru kunifahamisha wapi nimechochea.
Kwa kumalizia ningependa uingie hapa yapo mengine:
Mohamed Said: KIPINDI AZAM TV KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI ZANZIBAR 2016

Jingalao,
Vipi tena unakuja na mambo ya kukamatwa kwani wewe unahusika na vyombo
vya sheria?

Hili swali la kumtangaza mshindi mbona Maalim Seif kalieleza kwa kirefu kuwa
yeye hakutangaza ila yale matokeo yalokuwa yameshatolewa.

Fanya rejea katika mkutano wake na waandishi wa habari utakuta taarifa zote.

Sina haja ya mie kurudia barua ya Ali Ameir aliyekataa matokeo baada ya CCM
kushindwa kwenye uchaguzi wa 1995.

Hebu ingia hapa kuna mengi utajifunza:
Mohamed Said: NAMDURUSU ALI AMEIR UCHAGUZI WA ZANZIBAR 1995 NA JABIR IDRISSA

Sina cha kufuta kwani haya niandikayo nimeyafanyia utafiti na najua ukweli wake.
 
Mwenye uwezo wa kuharibu uchaguzi Tanzania ni chama dola tu.
Kwa nini mliuharibu?
Kura hazikutosha?
Kwa nini mara hii Jecha alishindwa kumtangaza Dr. Shein kuwa Mshindi?

Naona unaweka irrelevant attachments...jibu hoja
 
SAM_0914.JPG

Mabango ya kampeni Uchaguzi Mkuu Mji Mkongwe Zanzibar 2015

Nimekuta katika "archives" zangu picha hizi za kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2010 kutoka Mji Mkongwe. Mabango mawili ya juu kushoto linamuonyesha mgombea wa CUF Ismail Jussa na pembeni kuna bango la marehemu Nassor Mughery na chini Simai Mohammed Said. Mbele ya mabango hayo amesimama mwandishi. Sote tuliokuwa katika picha hiyo hapo juu ni Watanzania lakini...

Nimeileta "lakini," kwa sababu moja tu nayo ni kuwa ikiwa fikra zako zimeathirika na siasa za ubaguzi wa rangi utamwaona mwandishi ni "Mwafrika," na hao waliokuwa nyuma yake ni ''Machotara.''

DSC_2469.jpg

Bango la ''Machotara''
SAM_0911.JPG

Bango la CUF

Mwandishi muonekano wa rangi yake kwa hakika ni "nyeusi," na hao nduguze nyuma yake kwa muonekano wao ni "weupe."

Tunakabiliwa na siasa za kibaguzi.

Kuna swali litafuatilia hapa kwa upande wa CCM.

Ikiwa chama hicho hakitaki "Machotara," imekuwaje akina Mughery wakafikia hadi ngazi ya kuaminiwa kuwa wagombea wa uongozi katika Zanzibar ilhali hawa si katika ''wao?''

Lakini ni kweli kuwa hawa akina Mughery na Said si Waafrika?

Jibu linalokuja kwa haraka ni kuwa hapana.

SAM_0915.JPG

Bango la Dr. Shein na Maalim Seif

Hawa ni Waafrika kwa kuwa wana damu za Waafrika kutoka upande wa bibi zao nenda nyuma vizazi na vizazi kutoka makabila tofauti yaliyokuwa Zanzibar karne kwa karne kuanzia Wamanyema hadi Wanyamwezi.

Swali lingine litakuja.
Sasa imekuwaje haya yakaingizwa katika siasa za Tanzania?

SAM_0909.JPG

Wazanzibari
Mtu aliyekuwa katika taharuki hurukwa na akili na akafanya maamuzi mabaya.

Inawezekana taharuki ya kushindwa uchaguzi Zanzibar umeifanya CCM Zanzibar ipoteze kwa muda uwezo wa kutafakari na hii ndiyo ikawa sababu ya wao kutoa kauli ambazo kwa hakika zimefedhehesha Tanzania kama nchi.

Ingia hapa kutazama mwandishi akifanya kipindi Azam TV:

Mohamed Said: Kumbukumbu ya Mapinduzi Zanzibar Azam TV 2016
mohamed

Mohamed Said Hili La ubaguzi kwa CCM Zanzibar ni Donda Ndugu au Kilema cha Maisha..kwa Ufupi Wamechoka Kisiasa. Na vile fikra zao zimechoka basi mpaka Miti basi nayo kwao ni "MACHOTARA" Alimradi yana rangi ya cuf

miti.jpg
mittt.jpg
 
Naona unaweka irrelevant attachments...jibu hoja
Nioneshe mfano kwa kujibu hoja. Au ndio uwezo na aina yako ya kujibu hoja?
Haya bandungu, jitutumue, jitahidi kujibu maswali unayoulizwa usijitowe ufahamu.
Unakaribishwa kutoa majibu, ndugu Jingalao
 
Jingalao,
Niwie radhi kuhusu ''uchochezi.''
Nilijibu swali hilo katika bandiko langu huko nyuma.

Inaelekea limekupita.
Itapendeza ukiwa unasoma na post za nyuma hii itakusaidia kutojirudia.

Jibu langu liko hapo chini:
Kizibao,
Tunaweza tukajadiliana kwa heshima ikiwa tutatumia lugha za staha.
Ukianza mjadala kwa lugha za ''pia,'' hatutofika mbali.

Nakushukuru kwa kunifahamisha kuwa kuna ''Machotara Hizbu,'' na
''Machotara,'' wengineo.

Hili sikupata kulijua kabla.
Hayo mengine ulosema sina ujuzi kwa hiyo nitawaachie wengine wachangie.

Kuhusu uchochezi nitashukuru kunifahamisha wapi nimechochea.
Kwa kumalizia ningependa uingie hapa yapo mengine:
Mohamed Said: KIPINDI AZAM TV KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI ZANZIBAR 2016

Jingalao,
Vipi tena unakuja na mambo ya kukamatwa kwani wewe unahusika na vyombo
vya sheria?

Hili swali la kumtangaza mshindi mbona Maalim Seif kalieleza kwa kirefu kuwa
yeye hakutangaza ila yale matokeo yalokuwa yameshatolewa.

Fanya rejea katika mkutano wake na waandishi wa habari utakuta taarifa zote.

Sina haja ya mie kurudia barua ya Ali Ameir aliyekataa matokeo baada ya CCM
kushindwa kwenye uchaguzi wa 1995.

Hebu ingia hapa kuna mengi utajifunza:
Mohamed Said: NAMDURUSU ALI AMEIR UCHAGUZI WA ZANZIBAR 1995 NA JABIR IDRISSA

Sina cha kufuta kwani haya niandikayo nimeyafanyia utafiti na najua ukweli wake.
Ndio maana nikasema urekebishe hoja yako pale juu iwapo unafanya reference za ki-CUF.

Kurekebisha haitakucost chochote zaidi ya kuiweka hoja yako huru!..au weka reference yako kuwa 'nimemsikiliza maalim Seif akijitangaza mshindi'

Ondoa hiyo itikadi tujadili hoja kwa uhuru!
 
Naona unaweka irrelevant attachments...jibu hoja
Wewe unasema irrelevant attachments.
Kwenye video ya pili,umemwona Jecha?
Anazungumza na nani?
Huo ni ushahidi wa Chama wa dola kilivyomtumia Jecha kusitisha kumalizia kutangaza matokeo yaliyobakia.
Inaoneka hata kuzitizama hujazitizama. Unapata wapi uthubutu wa kusema ni irrelevant?
 
Jecha ameambiwa nini?ameambiwa futa matokeo?
Labda mimi sioni wala kusikia!
 
Ndio maana nikasema urekebishe hoja yako pale juu iwapo unafanya reference za ki-CUF.

Kurekebisha haitakucost chochote zaidi ya kuiweka hoja yako huru!..au weka reference yako kuwa 'nimemsikiliza maalim Seif akijitangaza mshindi'

Ondoa hiyo itikadi tujadili hoja kwa uhuru!
Jingalao,
Nimejitahidi kukueleza na si lazima ukubaliane na mimi.
Ninapoingia JF mimi silengi kuzungumza na mtu mmoja.

Huingia humu kuzungumza na umma kwa kile Allah kwa
hisani yake alichonijaalia.

Naamini wengi wamenufaika.
 
Hii Picha upande mmoja Inaonesha Ile Picha Ya Ubaguzi ya CCM ...na nyngine inaonesha wahuni maarufu unguja kama mazombie...hawa hutembe ndani ya magari Serikali , Hawa huranda mjini na wakiwa na AK 47 , Marungu , Mapanga, mashoka na mishare.
hutembea wakiwa wamejifunga nyuso zao kama wafanyavyo magaidi.
sasa hizi picha mbili jee alobeba bango na huyu wa kati picha ya pili sio mtu mmoja ?
SAMA.jpg
 
Hata mimi ninapoingia JF Siingii kuzungumza na mtu mmoja bali naingia kuzungumza na wengi wenye uelewa mdogo na mkubwa...kama nilivyojaliwa na mwana wa Mungu yesu kristu!!

Na kwa jina la Yesu maelezo yangu hueleweka kwa wengi ukiacha maruhani wachache!

HOJA HUJIBIWA KWA HOJA NA SIO KILIO AU VIHOJA!
 
Ahsante kwa fikra zako.
 
Hii Picha upande mmoja Inaonesha Ile Picha Ya Ubaguzi ya CCM ...na nyngine inaonesha wahuni maarufu unguja kama mazombie...hawa hutembe ndani ya magari Serikali , Hawa huranda mjini na wakiwa na AK 47 , Marungu , Mapanga, mashoka na mishare.
hutembea wakiwa wamejifunga nyuso zao kama wafanyavyo magaidi.
sasa hizi picha mbili jee alobeba bango na huyu wa kati picha ya pili sio mtu mmoja ?
View attachment 320718
Crabat,
Hatari ya mambo haya ni kubwa sana na athari zake huenda mbali sana.
Walikuwapo akina Hassan Mandera kabla ya hawa vijana.

Je, leo wako wapi?
Tuna dhima ya kuwafikia hawa vijana na kuwatanabaisha.

Wafahamishwe kuwa watu wanawatambua nawasijidanganye na huu ukimya
wa wale wanaowapiga na kuwafanyia kila aina ya ushenzi.

Waelezwe kuwa kila mbwa ana siku yake.
 
Back
Top Bottom