Kichekesho cha siasa za Ugozi Zanzibar

Kichekesho cha siasa za Ugozi Zanzibar

Msemaji Ukweli,
Nakupa jibu la haraka kabla sijafanya utafiti kuhusu ubaguzi wa Watanganyika Zanzibar.
Ikiwa hili limetendeka huko huo ni ubaguzi na unastahili kupigwa vita.
Mohamed Said umekuwa kwenye anga za kisiasa kwa muda mrefu na kwa maana hii ninaamini unafahamu kilichowapata Tanganyika wanaoishi Zanzibar.

Ninawashangaa watu kama wewe ambao mnataka kutuaminisha kama mnashangaa kilichofanywa na hao vijana wa CCM wakati ilifikia kiwango cha waumini wengine kuchomewa sehemu zao za ibada kwa sababu ya notion ya kwamba Zanzibar ni nchi ya Waislam.

Ubaguzi unawatafuna Wazanzibari.
 
CCM INATUCHUKIA SANA SISI WATU WA KASKAZINI

..tatizo ni ccm kutokuwa na guarantee ya kura zenu.

..akiibuka kiongozi wa upinzani toka kanda nyingine utasikia nao wanaanza kubaguliwa.
 
CCM INATUCHUKIA SANA SISI WATU WA KASKAZINI
Kwani CCM niya watu wa wapi?

Mashariki, Magharibi au Kusini?

Kuna watu wengine huwa wanajibagua wenyewe!

Kwa nini watu wa Kaskazini wanadai wanabaguliwa?
 
..huku Tanganyika kumezuka siasa za kikabila na kikanda.

..walengwa wakubwa wa siasa hizo chafu za ccm ni wenyeji wa kilimanjaro na arusha.

cc Mohamed Said
Kitu gani kinakufanya udhani kuna siasa za kikabila na kikanda?

Kama zipo, kwa nini unadhani zinawalenga wenyeji wa Kilimanjaro na Arusha?
 
Kuna mambo yanahitaji utumiaji wa common sense ili kujua jibu!! Mbona huku Bara ambako UKAWA walilalamika na kwenda kumuona Mwenyekiti wa tume hawakupewa hata nafasi ya kuwasilisha malalamiko yao ............. huko ambako hatukusia hata chama chochote kikilalamikia matokeo ndiyo yamekuwa na dosari na kufutwa!!
Unatumiaje common sense wakati chombo chenye mamlaka ya kusema hivyo kipo?
 
SAM_0914.JPG

Mabango ya kampeni Uchaguzi Mkuu Mji Mkongwe Zanzibar 2015

Nimekuta katika "archives" zangu picha hizi za kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2010 kutoka Mji Mkongwe. Mabango mawili ya juu kushoto linamuonyesha mgombea wa CUF Ismail Jussa na pembeni kuna bango la marehemu Nassor Mughery na chini Simai Mohammed Said. Mbele ya mabango hayo amesimama mwandishi. Sote tuliokuwa katika picha hiyo hapo juu ni Watanzania lakini...

Nimeileta "lakini," kwa sababu moja tu nayo ni kuwa ikiwa fikra zako zimeathirika na siasa za ubaguzi wa rangi utamwaona mwandishi ni "Mwafrika," na hao waliokuwa nyuma yake ni ''Machotara.''

DSC_2469.jpg

Bango la ''Machotara''
SAM_0911.JPG

Bango la CUF

Mwandishi muonekano wa rangi yake kwa hakika ni "nyeusi," na hao nduguze nyuma yake kwa muonekano wao ni "weupe."

Tunakabiliwa na siasa za kibaguzi.

Kuna swali litafuatilia hapa kwa upande wa CCM.

Ikiwa chama hicho hakitaki "Machotara," imekuwaje akina Mughery wakafikia hadi ngazi ya kuaminiwa kuwa wagombea wa uongozi katika Zanzibar ilhali hawa si katika ''wao?''

Lakini ni kweli kuwa hawa akina Mughery na Said si Waafrika?

Jibu linalokuja kwa haraka ni kuwa hapana.

SAM_0915.JPG

Bango la Dr. Shein na Maalim Seif

Hawa ni Waafrika kwa kuwa wana damu za Waafrika kutoka upande wa bibi zao nenda nyuma vizazi na vizazi kutoka makabila tofauti yaliyokuwa Zanzibar karne kwa karne kuanzia Wamanyema hadi Wanyamwezi.

Swali lingine litakuja.
Sasa imekuwaje haya yakaingizwa katika siasa za Tanzania?

SAM_0909.JPG

Wazanzibari
Mtu aliyekuwa katika taharuki hurukwa na akili na akafanya maamuzi mabaya.

Inawezekana taharuki ya kushindwa uchaguzi Zanzibar umeifanya CCM Zanzibar ipoteze kwa muda uwezo wa kutafakari na hii ndiyo ikawa sababu ya wao kutoa kauli ambazo kwa hakika zimefedhehesha Tanzania kama nchi.

Ingia hapa kutazama mwandishi akifanya kipindi Azam TV:

Mohamed Said: Kumbukumbu ya Mapinduzi Zanzibar Azam TV 2016
Naona maandiko yako yanazunguka humo humo tu kama pia.. lile bango limesema machotara wa KIHIZBU.. na wapo wanajulikana.na siyo kila chotara na hao uliwataja si machotara wa kihizbu.

kuna kitu chengine ubaguzi ZNZ haukuletwa na CCM wala CUF bali uko katika nafsi wa wazanzibar mimi ni mnzanibar wazazi wangu wanatoka katika visiwa vyote viwili..lakini ninachokuambia mimi kuna watu wa aina Fulani wanajiona wao ni bora zaid kuliko wengine..na wanawakebehi wengine kwa sababu tu pengine wana one drop ya hayo makabila. katika historia ya marekani walivyokuwa wanabaguliwa watu weusi kuna principle ilikuwa inatumika one drops blood kama wewe ni muafrika basi wewe ni black it doent matter rangi yako iko vp. kwa upande wa Zanzibar iko opposite kama una one drop ya uarabu au uhindi basi wewe siyo mtu mweusi na huwa wanajiona bora Zaidi kuliko wale wengine.wewe ingia website ya mzalendo na soma maoni na angalia mentality za wale wachangiaji. kwa hivyo suala la ubaguzi lipo Zanzibar kwa pande zote mbili.. Nakumbuka Fatma magimbi alipotoka CUF jinsi watu walivyoanza kumkebehi na wakaanza kuidharau nasabu yake.. hivi leo Zanzibar ukiwa hukubaliani na mawazo ya CUF unaambiwa siyo mzanzibari..nenda kasome mzalendo.net(website ya CUF) na soma habari za Amina salum ali na utaona jinsi gani watu walivyotokwa na akili. kwa hivyo wacha uchochezi kama unaamuwa kukemea ubaguzi basi sema kwa pande zote mbili na moja usiwe unaifumbia macho kwani hao magozi kama unavyo waita wao pia ni binaadam kama wewe.
 
Aliyesema CCM imeshindwa Uchaguzi Zanzibar ni nani na kwa mamlaka gani...hivi ukiitwa mchochezi utasema unaonewa?Tuchunge kauli zetu hata kama tunatawaliwa na itikadi zetu!

Makala yako umeiharibu hapo chini tu...
hivi mnataka kurudia uchaguzi wa nini wakati tayari mna mshindi wenu mezani? kwa nini hizo pesa msipeleke kwenye mambo mengine hata kama ni kuwapa mikopo wanafunzi wa vyuo vikuu?
 
Kweli mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadamu mchungu.

Ubaguzi upo zenji tokea enzi.
 
hivi mnataka kurudia uchaguzi wa nini wakati tayari mna mshindi wenu mezani? kwa nini hizo pesa msipeleke kwenye mambo mengine hata kama ni kuwapa mikopo wanafunzi wa vyuo vikuu?
Uchaguzi wa Zanzibar unarudiwa kwa sababu uliharibiwa...na walioharibu kwa maslahi yao ndio hao wasiotaka kurudia simply kwa sababu wanajua chance ya kuuharibu tena haipo!
 
Naona maandiko yako yanazunguka humo humo tu kama pia.. lile bango limesema machotara wa KIHIZBU.. na wapo wanajulikana.na siyo kila chotara na hao uliwataja si machotara wa kihizbu.

kuna kitu chengine ubaguzi ZNZ haukuletwa na CCM wala CUF bali uko katika nafsi wa wazanzibar mimi ni mnzanibar wazazi wangu wanatoka katika visiwa vyote viwili..lakini ninachokuambia mimi kuna watu wa aina Fulani wanajiona wao ni bora zaid kuliko wengine..na wanawakebehi wengine kwa sababu tu pengine wana one drop ya hayo makabila. katika historia ya marekani walivyokuwa wanabaguliwa watu weusi kuna principle ilikuwa inatumika one drops blood kama wewe ni muafrika basi wewe ni black it doent matter rangi yako iko vp. kwa upande wa Zanzibar iko opposite kama una one drop ya uarabu au uhindi basi wewe siyo mtu mweusi na huwa wanajiona bora Zaidi kuliko wale wengine.wewe ingia website ya mzalendo na soma maoni na angalia mentality za wale wachangiaji. kwa hivyo suala la ubaguzi lipo Zanzibar kwa pande zote mbili.. Nakumbuka Fatma magimbi alipotoka CUF jinsi watu walivyoanza kumkebehi na wakaanza kuidharau nasabu yake.. hivi leo Zanzibar ukiwa hukubaliani na mawazo ya CUF unaambiwa siyo mzanzibari..nenda kasome mzalendo.net(website ya CUF) na soma habari za Amina salum ali na utaona jinsi gani watu walivyotokwa na akili. kwa hivyo wacha uchochezi kama unaamuwa kukemea ubaguzi basi sema kwa pande zote mbili na moja usiwe unaifumbia macho kwani hao magozi kama unavyo waita wao pia ni binaadam kama wewe.
Kizibao,
Tunaweza tukajadiliana kwa heshima ikiwa tutatumia lugha za staha.
Ukianza mjadala kwa lugha za ''pia,'' hatutofika mbali.

Nakushukuru kwa kunifahamisha kuwa kuna ''Machotara Hizbu,'' na
''Machotara,'' wengineo.

Hili sikupata kulijua kabla.
Hayo mengine ulosema sina ujuzi kwa hiyo nitawaachie wengine wachangie.

Kuhusu uchochezi nitashukuru kunifahamisha wapi nimechochea.
Kwa kumalizia ningependa uingie hapa yapo mengine:
Mohamed Said: KIPINDI AZAM TV KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI ZANZIBAR 2016
 
Jingalao,
Ukifuatilia vizuri sakati hii ya uchaguzi ukasoma na kusikiliza utajua mengi.
Kuandika bila utafiti ni tatizo.
 
Weye kenge upo wapi ushahidi wa uchaguzi kuharibiwa?
 
Mohamed Said umekuwa kwenye anga za kisiasa kwa muda mrefu na kwa maana hii ninaamini unafahamu kilichowapata Tanganyika wanaoishi Zanzibar.

Ninawashangaa watu kama wewe ambao mnataka kutuaminisha kama mnashangaa kilichofanywa na hao vijana wa CCM wakati ilifikia kiwango cha waumini wengine kuchomewa sehemu zao za ibada kwa sababu ya notion ya kwamba Zanzibar ni nchi ya Waislam.

Ubaguzi unawatafuna Wazanzibari.
Msemaji Ukweli,
Haya matatizo ya kuchoma makanisa ni mambo mageni kote Tanzania,
Hayajapatapo kutokea huko nyuma.

Bahati mbaya mimi sina taarifa za kutosha kuweza kulichangia.

Kuhusu Zanzibar kuwa ni nchi ya Kiislam hili ni kweli na imekuwa hivyo
siku zote lakini hilo halikupata kuwa tatizo.

Masultani wa Zanzibar ndiyo waliowapokea Wamishionari na kuwapa kila
aina ya msaada.

Iweje leo ghafla tuwe na matatizo?
 
Jingalao,
Ukifuatilia vizuri sakati hii ya uchaguzi ukasoma na kusikiliza utajua mengi.
Kuandika bila utafiti ni tatizo.
Mkuu hebu kuwa muungwana...mada yako inahusu ubaguzi ni mada nzuri sana...lakini umeingiza ushabiki kwa kusema ccm Zanzibar haijashinda ...sielewi umetumia utafiti gani na kama ni sahihi kutumia utafiti kutangaza kuwa ccm haijashinda...labda ungesema kwa mujibu wa CUF ...CCM haijashinda nisingekutaka ufute hiyo kauli.

kuna muda tuweke ushabiki pembeni...hata mimi siwezi kusema mshindi kwa kuwa mwenye mamlaka hayo hajatangaza mshindi!!

Hata huku bara wafuasi wa UKAWA wanaamini wameshinda lakini NEC ndiye aliyetutangazia mshindi.

Nakushauri ufute hiko kipengele halafu turejee kwenye mjadala wa ubaguzi kulingana na ushahidi' ulioleta
 
Kizibao,
Tunaweza tukajadiliana kwa heshima ikiwa tutatumia lugha za staha.
Ukianza mjadala kwa lugha za ''pia,'' hatutofika mbali.

Nakushukuru kwa kunifahamisha kuwa kuna ''Machotara Hizbu,'' na
''Machotara,'' wengineo.

Hili sikupata kulijua kabla.
Hayo mengine ulosema sina ujuzi kwa hiyo nitawaachie wengine wachangie.

Kuhusu uchochezi nitashukuru kunifahamisha wapi nimechochea.
Kwa kumalizia ningependa uingie hapa yapo mengine:
Mohamed Said: KIPINDI AZAM TV KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI ZANZIBAR 2016
Kuzunguka kama pia ni kwa kule kwetu ZNZ ni Neno ambalo hutumika kwa kumtanabahisha mtu anafanya/anaongea kitu kile kwa kujirejea sasa sijui wapi nimekuvunjia staha.Tuje historia ya mapinduzi na huko kwa bamkwe mimi babu yangu mzalia baba ni mtumbatu na alikuwa akiuza nyama marikiti darajani pale...na unajua wakati wa alfajiri wanaenda pale na habari za mapinduzi alizisikia wakati yupo marikiti na alikuwa ni HIZBU mkubwa sana alienda kutolewa kwenda masanduku ya kuhifadhia nyama alikojificha na hakuiona familia yake kwa miaka 4. Sasa hizo historia ya ba mkwe na mapinduzi Nimezipata kutoka kwake..lakini hii leo ukiniuliza je ninayakubali mabadiliko yale.. basi jibu langu ndiyo hasa ukizingatia jamii ya kizanzibar iliyokuwa wakati ile basi mabadiliko yalikuwa ni ya lazima ijapokuwa babu yangu alikuwa ni victim wa mabadiliko yale. I'm sorry ya kuwa kuna watu hawana hatia walikufa na wengine wakafungwa na wengine wakakimbia nchi yao. Ukija kuhusu ubaguzi wa uchotara, mama yangu binafsi ni chotara na yeye ni mpemba wa ziwani na mkanyageni..kwa hivyo siongei haya kutokana na chuki yangu binafsi ya machotara au vp. Ubaguzi wa rangi znz upo na utaendelea kuwepo kwani watu wanajisifia Zaidi makabila ya babu zao.. (pengine ni 1/8 ni muarabu) kuliko uzanzibar wao na hao wanajiona wao wako noble Zaidi kuliko watu wengine.Na tuje ubaguzi mwengine wa upemba na uunguja huu watu wanafikiria umeenza baada ya vyama vingi but kusema kweli huu ubaguzi upo tangu zamani na nimeweza kuuushuhudia tangu nikiwa mdogo kwani kuna kipindi Fulani nililelewa na babu/bibi kwa mama yangu. Na mpaka 1995 nilikuwa mfuasi mzuri wa CUF mpaka ilipotokea event moja kuanzia hapo nikaona hichi chama hakifai kwa wazanzibar kwani ilikuwamanifestation yake ni Pembas movement na hao wengine wote ambao si wapemba just si wasindikizaji tu na siyo priority. Kwa hivyo kama unataka kuongelea suala la ubaguzi znz usisome kwenye magazeti au kuangalia vyombo vya habari nenda znz na kaa na ile jamii ya kizanzibari na utaona jinsi gani ubaguzi unavyoivuruga nchi.. tena kwa pande zote mbili... na ndiyo maana mimi ni muumini mkubwa wa muungano kwanibila ya muungano znz ni somali
 
Naona maandiko yako yanazunguka humo humo tu kama pia.. lile bango limesema machotara wa KIHIZBU.. na wapo wanajulikana.na siyo kila chotara na hao uliwataja si machotara wa kihizbu.

kuna kitu chengine ubaguzi ZNZ haukuletwa na CCM wala CUF bali uko katika nafsi wa wazanzibar mimi ni mnzanibar wazazi wangu wanatoka katika visiwa vyote viwili..lakini ninachokuambia mimi kuna watu wa aina Fulani wanajiona wao ni bora zaid kuliko wengine..na wanawakebehi wengine kwa sababu tu pengine wana one drop ya hayo makabila. katika historia ya marekani walivyokuwa wanabaguliwa watu weusi kuna principle ilikuwa inatumika one drops blood kama wewe ni muafrika basi wewe ni black it doent matter rangi yako iko vp. kwa upande wa Zanzibar iko opposite kama una one drop ya uarabu au uhindi basi wewe siyo mtu mweusi na huwa wanajiona bora Zaidi kuliko wale wengine.wewe ingia website ya mzalendo na soma maoni na angalia mentality za wale wachangiaji. kwa hivyo suala la ubaguzi lipo Zanzibar kwa pande zote mbili.. Nakumbuka Fatma magimbi alipotoka CUF jinsi watu walivyoanza kumkebehi na wakaanza kuidharau nasabu yake.. hivi leo Zanzibar ukiwa hukubaliani na mawazo ya CUF unaambiwa siyo mzanzibari..nenda kasome mzalendo.net(website ya CUF) na soma habari za Amina salum ali na utaona jinsi gani watu walivyotokwa na akili. kwa hivyo wacha uchochezi kama unaamuwa kukemea ubaguzi basi sema kwa pande zote mbili na moja usiwe unaifumbia macho kwani hao magozi kama unavyo waita wao pia ni binaadam kama wewe.
Nashukuru kwa maoni yake yalioenda shule.

Tunazoziona hapa ni siasa za kinafiki.

Tatizo la ubaguzi Zanzibar haliwezi kuondoka kwa sababu wale wanaojaribu kutuaminisha wanachukia ubaguzi ni wanafiki.

Unafiki wa aina huu ndio umepelekea uwepo wa kutoaminiana kisiasa.
 
Mkuu hebu kuwa muungwana...mada yako inahusu ubaguzi ni mada nzuri sana...lakini umeingiza ushabiki kwa kusema ccm Zanzibar haijashinda ...sielewi umetumia utafiti gani na kama ni sahihi kutumia utafiti kutangaza kuwa ccm haijashinda...labda ungesema kwa mujibu wa CUF ...CCM haijashinda nisingekutaka ufute hiyo kauli.

kuna muda tuweke ushabiki pembeni...hata mimi siwezi kusema mshindi kwa kuwa mwenye mamlaka hayo hajatangaza mshindi!!

Hata huku bara wafuasi wa UKAWA wanaamini wameshinda lakini NEC ndiye aliyetutangazia mshindi.

Nakushauri ufute hiko kipengele halafu turejee kwenye mjadala wa ubaguzi kulingana na ushahidi' ulioleta
Jingalao,
Mwaka wa 2011 nilishiriki katika kipindi cha Meza ya Duara kinachoendeshwa na
Sauti ya Ujerumani.

Washiriki wengine wenzangu walikuwa Salehe Feruzi wa CCM Zanzibar, Ahmed Rajab (London),
Dr. Harith Ghassany (Washington DC) na mimi nikizungumza kutoka Tanga.

Mwenyekiti alikuwa Othman Miraj kutoka Bonn aliyetuunganisha kwa simu.

Nilimwambia Salehe Feruzi hayo niliyoeleza hapa kuwa CCM Zanzibar hawajapatapo kushinda
uchaguzi.

Bwana Feruzi akaniomba ushahidi kama unavyoniomba wewe hii leo.
Nikamwambia kuwa inasikitisha kuwa yeye kiongozi wa juu wa CCM Zanzibar lakini hajui hilo.

Nikamuongozea kitu kingine.

Nikamwambia kuwa CCM Zanzibar wanaogopa uchaguzi na nikamweleza yale wanayofanya
kuwazuia wafuasi wa CUF kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.

Baada ya haya ndipo nikamkumbusha barua ya Ali Ameir katika uchaguzi wa mwaka wa 1995
baada ya CCM kushindwa waliyakataa matokeo.

Haya yote niliyosema hapa ni kweli wala si ushabiki.
Tujadili haya kabla hatujakwenda mbele katika chaguzi zilizofuatia.
 
Back
Top Bottom