Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,791
- 31,803
Mabango ya kampeni Uchaguzi Mkuu Mji Mkongwe Zanzibar 2015
Nimeileta "lakini," kwa sababu moja tu nayo ni kuwa ikiwa fikra zako zimeathirika na siasa za ubaguzi wa rangi utamwaona mwandishi ni "Mwafrika," na hao waliokuwa nyuma yake ni ''Machotara.''
Bango la ''Machotara''
Bango la CUF
Mwandishi muonekano wa rangi yake kwa hakika ni "nyeusi," na hao nduguze nyuma yake kwa muonekano wao ni "weupe."
Tunakabiliwa na siasa za kibaguzi.
Kuna swali litafuatilia hapa kwa upande wa CCM.
Ikiwa chama hicho hakitaki "Machotara," imekuwaje akina Mughery wakafikia hadi ngazi ya kuaminiwa kuwa wagombea wa uongozi katika Zanzibar ilhali hawa si katika ''wao?''
Lakini ni kweli kuwa hawa akina Mughery na Said si Waafrika?
Jibu linalokuja kwa haraka ni kuwa hapana.
Bango la Dr. Shein na Maalim Seif
Hawa ni Waafrika kwa kuwa wana damu za Waafrika kutoka upande wa bibi zao nenda nyuma vizazi na vizazi kutoka makabila tofauti yaliyokuwa Zanzibar karne kwa karne kuanzia Wamanyema hadi Wanyamwezi.
Swali lingine litakuja.
Sasa imekuwaje haya yakaingizwa katika siasa za Tanzania?
Wazanzibari
Inawezekana taharuki ya kushindwa uchaguzi Zanzibar umeifanya CCM Zanzibar ipoteze kwa muda uwezo wa kutafakari na hii ndiyo ikawa sababu ya wao kutoa kauli ambazo kwa hakika zimefedhehesha Tanzania kama nchi.
Ingia hapa kutazama mwandishi akifanya kipindi Azam TV:
Mohamed Said: Kumbukumbu ya Mapinduzi Zanzibar Azam TV 2016