Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
- Thread starter
- #21
Kuachana na wake zao!
Yalaaaaaaaaaah!!
Kuachana na wake zao!
kama yapi?
Woow!Kumbe hat si Tanzanians of the Indian origin?Mrs Kikwete, please do keep up the good job. On behalf of the Indian community in Tanzania, I'd like to thank you for all your efforts to make sure CCM is elected for another 5.
My two Cents...
Vote JK/CCM
Woow!Kumbe hat si Tanzanians of the Indian origin?
So kama ungekuwa nje ya Tanzania halafu unatoa ujumbe huo huo ungesemaje??"On behalf of Indian ommunity in UK....."?Ina maanisha nyir si watanzania?Weka sawa.....
Katika hali inayoonesha kuwa kweli suala la Urais wa JK ni la kifamilia zaidi, Bibie Salma Kikwete ameghadhabishwa na watu wanaoponda tabia yake ya kutumia mali za umma kumfanyia kampeni muumewe.
Bi Salma ametamka hayo katika moja ya kampeni zake za "Ndani Kwa Ndani" huko Bukombe na kuwataka watu hao kuwa waache tabia hiyo kwani watu hao wanataka kuharibu ndoa yake halali.
My Take:
==================================================================
Hii sasa ni kali. Kwa hiyo Salma ameagizwa na muumewe kupiga kampeni, la sivyo hakuna ndoa.
Hii familia ina lao jambo kwanini inataka kuingia ikulu kwa nguvu hivyo? tujiulize watanzania jamani hizi nguvu zinazotumika ni nyingi mno! maana hiki si chama tena ila familia yenye family friends kibao wanotaka kutawala nchi ili wajilimbikizie mali waishi vizuri na vitukuu vyao! ole wao maana anguko lao laja kuanzia baba hadi wajukuu zao. jamani huyo ridhwani kama mwenye anatawala nchi, juzi juzi kimwanamke chake cha nje kililewa kikapigwa makofi na polisi barabarani! lol polisi ndani wiki nzima! halafu eti oooh watakuwa waaadilifu hao wanataka madaraka waturarue!
MUNGU TUOKOE KUTOKA KWENYE UTAWALA WA JK NA FAMILIA YAKE NA CCM KWA UJUMLA .
AMEN!:amen:
Mimi siwezi kusema "On behalf of chagga community" Nitaseama On behalf of ma fellow countrymen...Upo?Mmeshauza nchi kwa ufinyu wa kuelewa.Kutamka 'Indian community' hajakana utanzania. Mbona hata nyie wachagga mna community zenu kila mahali? Zipo pia community za wakatoliki, waislamu nk. Pale chuo kikuu mlimani kulikuwa na community za kila kabila na walikuwa na viongozi wao wanaalika hadi wabunge kwenye sherehe zao. Kuna ubaya gani wakijitaja kama 'Indian community', kwanza kweli ni wahindi, sasa? Na nyie mbona ni wachagga? Acha mambo yako bwana Mushi
Ndoa ya JK na Salma tutainusuru kwa kuhakikisha ya kuwa tunawatimua Ikulu ili waweze kutumia muda mwingi pamoja. Kazi ya Uraisi yelekea inawatenganisha na muda mwingi hawapo pamoja na hiyo siyo dalili nzuri kwa wanandoa hao.