Kibweko cha Mbwa Koko, hata Sisimizi huchekelea na hakitishi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibweko cha Mbwa Koko, hata Sisimizi huchekelea na hakitishi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, May 27, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Hivi; Ana lia, ana lalamika, ana nung'unika, ana huzunishwa, ana chukizwa, ana tahayari, ana sikitika, ana ghafilika, ana kata tamaa au kwa kifupi hajielewi?

  Yaani miaka yote hii ya majaribio na takwimu zote na ripoti zote, makabrasha ypte na matusi yoote leo hii ana uwezo wa kutoa sauti eti ana kerwa?

   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Anachukizwa na nani
  Na akichukia nini
  Hasira zake kwa nini
  Wenye kumuudhi nani?
  Hasira zake mkizi, furaha huenda kwa nani?

  Mwenzetu huyu wa wapi
  Anafikiria yapi
  Msimamamo wake upi
  Achukizwapo ni vipi?
  Hasira zake mkizi, furaha huenda kwa nani?

  Ati leo achukia
  Na jana kawanunia
  Kesho awabwatukia
  Mtondogoo arudia
  Hasira zake mkizi, furaha huenda kwa nani?

  Ngumi anawakunjia
  Na nditi kawapangia
  Kejeli awamwagia
  Wenyewe washangilia
  Hasira zake mkizi, furaha huenda kwa nani?

  Majina anawajua
  Ati atawaumbua
  Tena atawashushua
  Wananchi watajua
  Hasira zake mkizi, furaha huenda kwa nani?

  Hivi simba wa kuchora
  Humpiga nani mkwara
  Kama siyo masikhara
  Nani atakula ngwala
  Hasira zake mkizi, furaha huenda kwa nani?

  Maneno ayatumia
  Ati watamkimbia
  Mwenyewe ajisikia
  Ukweli kawapashia
  Hasira zake mkizi, furaha huenda kwa nani?

  Maswali yameingia
  Ya yule alochukia
  Yale yale arudia
  Miaka inapatia
  Hasira zake mkizi, furaha huenda kwa nani?


  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  May 27, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  He should just shut the hell up
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  OPP, umefanya nini tena..?
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  May 27, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sijafanya chochote....change is good sometimes....
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  May 27, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  huyu ni mwepesi tu, sema nchi hii inakosa mtu wakutuunganisha, tunatamani utokee moto wa gharika kisiasa, tumuone anavyolanda na njia , sijawahi kumfikiria kuwa yeye ni kiongozi legelege kama alivyo leo....Kikwete mimi nikimchagua nifie kwenye kibanda cha kura, amka Tanzania, huyu anatudanganya. hakika tunahitaji mabadiliko, hatuhitaji joka la kibisa kwenye utawala wa nnchi, tunataka Kiongozi mwajibikaji na mpambanaji.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I agree, he must shadd'up! I mean JK.
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  May 27, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  hata simuelewi.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  May 27, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  JK ni Mwanasiasa msanii na siasa kwa ujumla wake ni Uongo unaokubaliaka. Makosa yetu ni kumpa msanii mcheza sinema nafasi, swaga lake litawapumbaza wengi.
  Hivi kweli mtu unasikitika na viongozi wasiokuwa responsible, yet unawaacha ktk nafasi zao!
  Unataka mkaguzi mkuu atoe taarifa mapema hali akitoa hazifanyiwi kazi kwa sababu wahusika ni vigogo wa chama.
  Toka EPA, Bank Kuu, mashirika mengine hadi wizara tumeona makosa ya wazi, huyo Utouh kasema wee hadi sauti imemkauka, na viongozi wabovu wameendelea kupeta kwa miaka minne.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Mkuu naunga mkono hoja. Huyu bwana ndio top most. Ana mamlaka ya kufanya kweli. Sasa anategemea nani mwingine atafanya jambo la ziada kama yeye anapiga story tu na kudanganya watu kila kukicha.
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nadhani saa nyingine Kikwete anasahau kwamba yeye ndiye rais. Naona kama anajiona kama vile yeye ni Denzel Washington na Tanzania
  ndiyo Hollywood yake, kwa hiyo ni mchezo wa kuigiza tu, unapigiwa makofi na kupanda gari la ving'ora na kazi imeisha. Akiambiwa achukue
  maamuzi anapata kigugumizi. Nadhani wakati umewadia aambiwe kuwa Tanzania si Hollywood na tumechoka kusikia tunataka kuona vitendo.
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Huyu kakaetu sindibadi ni msanii tu atakudanganya kwamba hafahamu chochote kumbe anafahamu kila kitu. He is always double faced, smiles apparently but curses inside, pretends to be serious but inward joking and mocking. It's your time buddies msifanye kosa come october!
   
 13. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  • Alifungua Hotel pale Arusha, kesho yake manispaa wakapomoa.... ipo wrong sites....
  • Aliitwa kukabidhi gari la wagonjwa kwa viongozi wa sehemu A wakaja wa sehemu B kupokea.....
  • Akaitwa kupewa zawadi kwa kijitoa kimasomso michezoni, akapewa Jezi ya Ronaldo.....
  As a leader hustuki tu........., wala huhisi kama wanakudharau......., unakenua meno tuuu.........

  Hivi huu ni utahira, Wehu au Ukatuni. Still you are telling me to call him a president. Over my dead body.
   
 14. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hata alishawahi kutoa hundi ya sh. laki tano akidhani ya milion 5! kazi kwelikweli!!!
   
Loading...