Kibonzo: Hali ya Profesa Lipumba ofisini Buguruni inatia "huruma"

Kibonzo: Hali ya Profesa Lipumba ofisini Buguruni inatia "huruma"

Hivi inakuwaje hata mke wake na watoto wake hawamsaidii kwa kumshauri hadi anajiaibisha namna hii? Je ana mke na au watoto kweli!! Mbona maajabu haya?
 
Hahaha. Pale Ofisini naamini hakuna mazingira ya kupata hizo huduma.
True!.pale yuko ngomeni askari watiifu wako nje,ameletewa tv set ana angalia matukio ya kushangaza ya waoga wa znz.
 
Namkumbuka leprofesseri alivoenda ikulu kumtembelea JPM shati likiwa limeoa majasho sijui alitembea kwa mguu!
 
Ilikuwa kama utani,lkn sasa ni ukweli kuwa Prof Haruna Lipumba habanduki Ofisi za Chama Buguruni kwa woga wa "kupoteza" kiti chake.Sasa Prof analala na kuamka humo humo bila kutoka.Ndani ya jengo la ofisi hizo,vyumba vingi vya ofisi kwa sasa si ofisi tena bali ni vyumba vya kulala walinzi na mabaunsa wa kulimlinda Professeri.Mlangoni kufuri lukuki kama geti la magereza

Buguruni haaingiliki,ni mwendo wa mundu,shoka na mapanga ndani ya ofisi.Hali hii viongozi wa Mpito wa CUF wanasema wametoa taarifa polisi na hakuna hatua zinazochukuliwa.Ujio wa Maalim Seif,Wabunge na viongozi wa muda umeshindikana baada ya kupata taarifa kuwa ndani ya jengo hili kuna kambi ya "karate",kunfuu na judo ya vijana ambao ni "walinzi" wa jengo na Profesa ambao wanasubiri kwa hamu wale waliomuondoa Lipumba wasogee wapate cha moto.

Sasa ni tetesi,CUF ya kina Mtatiro imerudisha jengo kwa mmliki ambae nae ametoa siku kadhaa kutaka jengo lake na hivyo Lipumba kutakiwa kuhamisha "makao" yake na kwenda sehemu nyingine kutafuta ofisi.

Ama hakika hali ya Buguruni bado si shwari...Lipumba analala na kuamka,anaoga na kupauka bila kutoka nje ya uzio wa ofisi hizo.Kweli kila siku Afrika,ajabu jipya huzaliwa.
View attachment 409660
Mkuu sijakuelewa kabisa! Kwamba, CUF wamerudisha jengo kwa mmiliki?
 
Hilo la Pango ndio kiboko yake, mimi sikulifikiria kabisa. Amchangishe Sakaya na wale mabaunsa ili alipe pango na aendelee kuwa M/Kiti kabla hajawa Mwenye Kigoda.

Joto la kanza ni pesa ya kulipa Luku, la pili hata akitaka kulipa Pango nasikia mwenye nyumba kashapandisha Dau mara 10. Chezea CUF!!!!!! WEEEEEEE. Pesa yote aliyoichota CCM itaishia hapo

Kama wewe Pro-Pesa Wenzako Pro-akili.
 
Sijui kama ni njaa tena nasema sijui lakini kama ni njaa basi tusiwalaumu wakina dada walioolewa na kuhungwa kijipesa kidogo tu na kusaliti familia.... Mwambie unaemjua njaa mbaya sana sio kosa lako (usimtukane matusi wala kumpiga) maneno hayo yanatosha kumfahamisha ujinga wake.
 
Haha,hivi profesa aliwataimu vipi akanyakua ofisi?,ina maana kina mtatiro hawana intelligence mpaka kawastukiza na kupora ofisi wao wakiwa wapi?
Walifunga akaingia kwa kuvunja milango
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom