Kibongobongo kumiliki milioni 100 kabla ya miaka 30

Kibongobongo kumiliki milioni 100 kabla ya miaka 30

Haya maneno husemwa na washkaji zangu wa Forex, NFT na crypto. Maneno kibao ila assets, cash in hand, cash at bank na spending vinawakataa.
Wanataja hela nyingi alafu mkipiga story wanapeana machimbo ya WiFi ya bure.
Wanakodisha magari na kukaa juu ya bonet huku wamening'iniza sandals na kuandika quotes za kina Pablo Escobar na 50 Cent.

Muache afiwe sasa uone maajabu. Nauli ya kwenda kwao hana[emoji23]

Staki hata kuwaskia watu wa forex aisee
 
Kuna jamaa mwaka 2013 alikuwa chini ya 35 akimiliki semi 2, fuso 1, prado 1. Jamaa ni mfano mzuri wa kuigwa na mpambanaji halisi maana alianguka mpaka 0 lakini sasa hivi anazisaka kwa udi na uvumba ingawa miloni 3 hazifiki. Kilichomwangusha alikuwa anasema alishindwa kulipa madeni baada ya kukopa na mwelekeo wa biashara kubadilika kabisa.
 
Unakuta kila mkuu wa kitengo wizarani alikatiwa Billion 5 hapo unapomchapa 200M ni kama kijiko tu kwenye mavumba.

ni wachache sana tena sana wenye utajiri ulionyooka kwenye hii nchi yetu. Yaani wenye 100M BENKI ambayo anaweza kuitolea maelezo? Wapo lakini ni wachache. Yaani mfano leo atokee Kiongozi afanye kuhakiki hela za bondholders pale BOT? Wengi watalia na kusaga meno. Ukweli ni kwamba wengi ni wezi tuu.

siku hizi wengi wanaiba hela za walipa kodi na kukimbiza kwenye Bond BOT na UTT. Ushauri wangu kuweni makini..…atakuja kiongozi kama JPM mtalaumiana bure tuu.
 
Mazingira ya kiafrika hayaruhusu hicho kitu,ndio maana unaona tajri wa kwanza Afrika dangote lakini kidunia ni wa 110 huko.sababu kubwa market share ni ndogo.
The only way uwe na kiasi hicho before 30 ni uwe umetokea familia tajiri au ulishia darasa LA 7/form 4 ukaanza biashara.
 
Miaka fulani nipo chuga tena kijana mdogo nilipata fursa ya kuingia kwenye biashara ya kitalii, kuuza tishet kwa order na vitu flan flan kwa watalii, Dah nilizikamata pesa sio poa nilishaanza kuuona ubilionea chini ya miaka 30,

dah kilichoniponza kuwafundisha na washkaji zangu iyo fursa, Walinipindua bila ya kutarajia mtaji ukaporomoka chali.
 
Mimi kwakweli sipendi kujipa stress,,, nikiwa tu na uhakika wa kula ninachokitaka, nauli kila ninakotaka kwenda mda wowote ipo,, king'amuzi nimelipia,, nguo zangu safi,, bundle la mwezi,, maji umeme vipo roho yangu nyepesii..nyie endeleeni tu kurushana roho maisha yenyewe mafupi haya 😅😅😅🙌
🤣🤣🤣Kuna mda unafika unavovitaja sio shida mawazo yana-extend utahitaji uwe na akiba, uwe na assets, ujenge, utafute usafiri hapo bado kunakuwashika Mkono wazazi wanapokwama
 
Chuo mwaka wa kwanza niliweka hela Forex nikasoma sana hadi kupoteza muda wa vipindi na kupata GPA ndogo, nikaacha kula mchana kile kipindi market imechanganya nikaambulia stress na kukonda.
Nikaamua kutafuta facts kwa wadau, nikawatajia mabilionea na mamilionea wa vyakula, mabasi, wamiliki wa viwanda na biashara nyingine kisha nikataka wanionyeshe mtu mmoja tu aliyefanikiwa kwa Forex.

Wakaanza kunitajia kina Sirjef na wenzake. Nikaulizia net worth yao, assets zao, madeni, spending, tax, premises na vitu vyote muhimu vya mwenye hela. Huwezi jua utajiri wote wa mtu ila hela hazijifichi especially za kijana, nikaambulia kuonyeshwa posts za Instagram nikawaacha na Forex yao.

Kama vipi ukitaka trader abadili mada mwambie akuonyeshe deposits na withdrawals upige total. Hata uweke hela atakataa, kuna loss anaificha. Stress zake huwezi kuwa na kitambi ukiwa trader, labda uwe muuza signals na tapeli.
Ulipouliza wadau wakuonyeshe mtu mmoja aliyefanikiwa kwa forex wakakuonyesha Ontario/sirjeff wa Twitter? Ahahaha.
 
Ni rahisi kama baba yako ni Jakaya au Rostam Azizi au ana affiliation na CCM Cartel ya mabilionea.

Kama umezaliwa pasipo na hela jiandae kuzeeka maskini mwenye nyumba ya 3 room na IST uwani. Wala sina haja ya kukupa moyo.
Inawezekana boss na vijana wapo labda kama haujafanikiwa kukaa nao
 
Khaaa jamani humu kuna watu waovyo sana,eti miaka 25 amiliki million 100,hii haiji kichwani kabisa je huyu kijana alimaliza chuo lini,jamani jamani tusilishane matango pori humu sisi sote tunajielewa huwezi miliki million 100 ukapoteza mda humu,kusema la kseli kwangu mimi namiliki nyumba 2,gari 1 pikipiki za boda boda 4 heka 50 huwa nashika million 30 tena nina miaka around 34
Usikariri kumiliki pesa mpaka uwe msomi, wajasiria mali wengi wameishia la saba na form 4 wanamiliki pesa kuzidi hao wasomi, kuna vijana wameishia form 4 wana maisha mazuri na biashara zao kuzidi wasomi
 
life start at forty hata serikari imeweka umri wa mtu kuajiriwa ni ukiwa ana miaka 40 na ndo maana mifuko ya pension ili uwe mstaafu inabidi uwe umechangia miezi 180 ambayo ni miaka 15 ndo maana umri wa kustaafu kwa hiari wakaweka miaka 55 maana yake utaajiriwa ukiwa na miak 40 kisha ushtaafu ukiwa na 55 au 60 lazima.
nb: Nawaza kimoyo moyo tu
 
Back
Top Bottom