Kibongo bongo nyimbo ya Daz Nundaz “Kamanda” ni nyimbo ambayo ukiiskia inaweza kukutoa chozi

Nyimbo ni uwingi wa neno wimbo.
Wimbo ni umoja,
Nyimbo ni uwingi,
Ni vyema kuzingatia matumizi ya uwingi na umoja kwenye muktadha wa mazungumzo ili kupata mantiki sahihi...
hilo sio lengo la uzi mkuu
 
Huu ni ukweli wakuu hii ni nyimbo ambayo hata ukiiskia tu hisia za kulia inakujia hii nyimbo ni nyimbo ambayo haitowahi kutokea kwenye muziki wa bongo flava 🙌🥲 hakuna na haitowahi kutokea nyimbo ya kuhuzunisha kama hii
Kwa sasa hivi Sio nyimbo tu, hata ukiwaona walioimba, unatoa machozi
 
Ila zamani watu walikuwa hawana stress. Just imagine nyimbo kama kamanda, watu walicheza tena kwa kuenjoy kabisa.
Nakumbuka nikiwa tamsala mdogo wake na Ay, magdalena alikuwa ndio dancer wa huo wimbo😄
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
1.Ferooz ft Prof Jay_starehe
2.Daz Nundaz_kamanda
3.Daz Nundaz_barua
4.Matonya_dunia mapito
5.Mb Doggy_waja
Aisee Hz nyimbo walitumia IQ kubwa sn kuzitunga,binafsi ndo nyimbo zangu Bora za muda wote tangu kuzaliwa kwa Bongofleva.
 
Mstari wa Afande kwenye mkuki moyoni hua unasikitisha..

Hivi mama una kichaa, mwenyewe umenizaa alafu unanikataa
"Kweli nilishangaa mama yangu aliyenizaa, kuniacha kwenye mataa,takribani nusu saa sikuongea kama bubu,watu walinizunguka nikiinama chini kwa aibu,"

Chorus:
Mateso unayonipa mwilini,
vigumu we kuyatambua usoni,
Ushanichoma mkuki moyoni ,
siwezi Tena kuishi duniani na wewe,
Rudisha huruma yako we mama,
Rudisha huruma yako we mama,
Kabla Mimi sjafa kinyama!.

Afande sele alikuwa anamashairi makini na yenye vinaa na Mambo kibao.

Mpaka hivi sasa au kizazi Cha Leo ngumu kupata wimbo/nyimbo zinazo mhoji, challenge,Au kumpa vidonge Mzazi Wa kike MAMA...!

Sana Sana ziipo nyimbo za kumsifia Sana Sana mama Mzazi!! Na kumukweza Sana Juu mno...huku Mzazi Wa kiume baba akiachwa na kusakamwa mno.

Mfano:Mr nice-nakupenda mama!
Omg dimpoz-Nani kama mama!
Bon mwaitege-Mama.
Banana zoro-Mama yangu. Na nk.

Hii concept/Dhana ya Mzazi hakosei/Hatukanwu/Hahojiwi na mwanae Bado inamizizi Sana ! Dhana iiliyo na mapungufu kibao ikiitazama kwa makini.


Mzazi akiwa nje ya mstari awe kike au wa kiume lazima awekwe kati,
 
Ila zamani watu walikuwa hawana stress. Just imagine nyimbo kama kamanda, watu walicheza tena kwa kuenjoy kabisa.
Nakumbuka nikiwa tamsala mdogo wake na Ay, magdalena alikuwa ndio dancer wa huo wimbo😄
Hahaha!

Hili Huwa nikikutana na Jamaa zangu Huwa tunacheka na kufurahi kuhusu nyimbo za nyuma bongofleva!

Kisha tunaingia kwenye mjadala mkali,kuhusu Nini..??? Kuhusu Watu katika club au sherehe kucheza nyimbo za huzuni au maskitiko!!

Je,ulikuwa ni ukosefu wa nyimbo za amsha-amsha clubbenga au maisha hayakuwa na stress..???!

Afande sele akihojiwa na Baruani muhuza anasema Wasanii enzi zao walifanya kazi kubwa na yaziada kuwakimbiza/Kuwaondoa wacongo,bongo(Congo music's)..(Defao,Kofii, Extra music's,Wenge Musica,Yondo ssta na nk).

Watu kucheza Nyimbo kama kamanda,Inaniuma-Juma nature ,Ugali,Waaguzi-Wagosi wa kaya, nk...,katika sherehe au clubs...

Sababu zipo nyingi ilamojawapo pia na kubwa ni Jamii ilikuwa Bado Sana Sana katika vifungo vizito vya Mafundisho,kanuni na taratibu za Dini za kigeni(Ukristo na Uislamu) na Vifungo vizito pia vya Ujamaa/Socialism ya Jk Nyerere! ,Ubepari Bado ulikuwa haujapenya Sana!

Hivyo utunzi,utungaji wa Mashariki/Nyimbo viliaangukia katika vifungo au Mambo hayo Ujamaa na Dini,

Mfano:Sikiliza vizuri Mashairi ya wimbo wa kamanda,yamechota mawazo/Maoni na mtazamo wa kifo uliochakatwa na kuhubiriwa na Dini bila kusahau Ujamaa !

Hivyo msanii/MTU kuimba nyimbo za kushangweka na Bata,lazima ujitafakari marambili au ujilipue kama mpanzi,unapanda mbegu.

Nyimbo za Kujirusha na clubbenga zilikuwepo chache Sana Tena zilizohit Nchi nzima ndio zilikuwa chache mno. Mfano Pamba nyepesi-Insepcta haroun Babu,Mikasi-Ngwair,Jirushe-Ferouz ft jaymo,T-shirt na Jeans,Nicheki-Oten Nk...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom