Kibongo bongo iPhone ni taashira ya hadhi au?

Kibongo bongo iPhone ni taashira ya hadhi au?

Inategemea na mtazamo wa mtu. WaTz wengine yuko radhi atumie akiba yake yote kununua iPhone, mimi binafsi sinunui simu zaidi ya 300,000/- kwasabsbu nishamiliki latest phones before ambazo nilikuwa napata bure sasa sioni mantiki ya kutoa 2.5m ninunie simu!
Kwa upande mwingine ni priority, mfano naweza kutumia 2m kununua Tv lakini sio simu.
Kwa kumalizia kwangu mimi mtu akimiliki iPhone wala sioni kama kafanikiwa naona ana hobby tu na hio device.
Nothing to add......umemaliza mzee,
 
Aisee kuna siku nilikuwa pale shoppers plaza kwenye maduka ya simu, nilikuwa natafuta betri original ya simu yangu, akaja demu pale akacheki Apple nyeupe nikasikia anapiga simu baby ni milioni na laki mbili.. kidume kikajibu okay sawa nunua tu hiyo (nilikuwa karibu so speaker zilisikika) nikajisemea kimoyomoyo mwanaume mwenzangu keshalizwa huko..mtu yuko tayari ahongwe iphone ya zaidi ya milioni wakati yuko chuo au yuko nyumbani tu kazi hamna.. mbona huo ni mtaji tosha? tunaishi maisha artificial sana.. bora ununue kwa hela yako unajua yes, nafanya kazi, naspend hela yangu.. lakini mtu unataka uhongwe ili uonekane uko kwenye status fulani wakati ni kapuku tu..chaaaa.... nitaambiwa wivu
 
Haya wenye ma I phone, mi nnayo itel hata sijui ni toleo gani
 
Ukiwa na Mercedes Benz kwny harusi unaenda ku block Gari ya Bwanaharusi Halafu unajificha kwny Kundi la wasiokujua, utaskia mwny namba T 665 DCK Aina ya gari ni Mercdes Benz anaombwa atoke Nje kuna Tatizo kidogo sasa hapo ndo unaanza kutoka kwa kuzunguka mbele pale kwny keki huku unarekebisha Funguo kwny lux ya Mkanda kila Mtu a kutambue

Hahahaha......dah nimecheka sanaa
 
Umeona mkuu, unanunua simu ya 1m+ halafu matumizi yake ya kawaida kabisa, whatsap, call&sms, na ku browse tu, vitu vilivyomo ndani( program) hujawahi vitumia hata robo kwa nini usiwe na simu ya laki 2/3 tuu inatosha.

Ukijua kwanini kuna simu za milioni 2 na kuna simu za laki 2 hautoandika hivyo tena.
 
Uwiii hongera sana kitu unlocked kwa makonda huku wanauza sasa hiv milion kama 3 wengine mbavu za mbwa wanasubir atleast ikae kwenye 2.5m

Oh yeah?

Binafsi napenda zaidi zilizo unlocked kwa sababu zinatumika pretty much popote pale bila matatizo.
 
Ni ukweli kwamba iphone ndo simu zina bei mbaya sana, kama nikiona mtu ana iphone najua ametumia hela ndefu kununua hiyo iphone.

So, ninachofanya napiga hesabu za haraka haraka kwamba kama anaweza kutumia 1M+ lazima atakuwa na kipato kizuri sana, kwa sababu ninaamini hawezi kukopa kwenda kununua simu.

Mimi nina tecno w3 ya sh 180,000, siwezi kujilinganisha na mtu wa iphone.
Sio kweli mm natumia Galaxy S8+ nilinunuaga just zilivotoka tuu almost 1.8M bila VAT...lakini sina hata kazi!
Sometimes dont get twisted kua na simu ya bei ghali haimaanishi mtu anakipato kikubwa....unaeza kukuta kasevu mwaka mzima anunue kipendacho roho ili ale nyama mbichi!
 
Inategemea na mtazamo wa mtu. WaTz wengine yuko radhi atumie akiba yake yote kununua iPhone, mimi binafsi sinunui simu zaidi ya 300,000/- kwasabsbu nishamiliki latest phones before ambazo nilikuwa napata bure sasa sioni mantiki ya kutoa 2.5m ninunie simu!
Kwa upande mwingine ni priority, mfano naweza kutumia 2m kununua Tv lakini sio simu.
Kwa kumalizia kwangu mimi mtu akimiliki iPhone wala sioni kama kafanikiwa naona ana hobby tu na hio device.
Kweli Mkuu ...ni hobby ya mtu na sio kua eti ni mafanikio...
 
Uwiii hongera sana kitu unlocked kwa makonda huku wanauza sasa hiv milion kama 3 wengine mbavu za mbwa wanasubir atleast ikae kwenye 2.5m
Wajinga ndo wanauziwa bei izo....ukienda dukani tafuta bosi wa hapo mwambie akuuzie bila VAT...it's that simpo unapata kwa bei nzuri tuu....maana ukilipa kodi ujue inaenda kukomboa ile bombadia huko canada
 
Sio kweli mm natumia Galaxy S8+ nilinunuaga just zilivotoka tuu almost 1.8M bila VAT...lakini sina hata kazi!
Sometimes dont get twisted kua na simu ya bei ghali haimaanishi mtu anakipato kikubwa....unaeza kukuta kasevu mwaka mzima anunue kipendacho roho ili ale nyama mbichi!

Kuna mtu hata asevu mwaka mzima hawezi kutimiza hiyo 1.8 m, mfano mtu mwenye kipato net laki 4, hiyo ni basic salary ya laki 5 na nusu.

Unadhani anaweza ku-afford kusave 150,000 kwa mwezi ili aje anunue simu ya 1.8M?

Na hao ndo waliojaa humu JF (50%+ members humu wana kipato cha gross chini ya 1M).
 
Wengi ni fuata mkumbo.

Si kwamba wanazitaka sana au kuzijua sana. Mpe hiyo Iphone uone, week nyingi anatafuta kuiuza...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom