WANATAKA IPHONE HALAFU KUITUMIA HAWAJUI.
IPHONE WATUMIAJI NI WACHACHE KWA NCH ZA KIAFRIKA. MFN TZ, UNAWEZA KWENDA WILAYA NZIMA IPHONE UKAZIKUTA MBILI AU 3
ILA TECNO HADI MTOTO WA SHULE ANAYO
Samsung zimezagaa kama nywele
Akina GIGY MONEY hao...wana IPHONE 6 lakini wanapo lala kama wapo STORE
kwahiyo wewe kwako kula ndio utajiri?Ishu sio kusave, hapa tunaangalia uwezo, unaponunua iPhone kwa pesa ya vizinga au kuhongwa kama ni mwanamke ili uonekane unayo na ukaishiwa mpaka kula unavizia na anayenunua Tecno kwa pesa yake na akabaki anakula ugali unazani nani tajiri hapo? Au nani anaishi kama Ng'ombe na nani ni mchunga Ng'ombe?
Mimi natumia IPhone
Moja ya Faida ya IPhone siazimwi Charger.
Nilihama Samsung kwa kero ya kuazimana charger na team techno
Lakini pia android huwazi wala kuumia kichwa ukisahau charger safarini.Mkuu unatumia kinywaji gani aisee, manake tecno na samsung ni kama spana malaya,kila dakika unaombwa charger.
Vertu umeenda mbali sana.Hayo ni maneno tu kiukweli iphone ina sound good ila sio kwamba ina bei kubwa kuna simu inaitwa vertu 2013, 2015 hii inatengenezwa UK gharama yake tu vitz mbili unabakiza na ya mfukoni
Zipo nyingi ila hili wengi wanapenda sifa tu kutumia big brand kama apple na samsung ila kuna simu zina hadhi zaidi ya hiyo sema majina ndio hakuna au saa nyingine upatikanaji na bei zakeVertu umeenda mbali sana.
Kwani kuna iphone ngapi za milioni 1.5,
Ambazo zinakwenda sawa na bei ya androids kibao tu,
Alafu simu sio kigezo cha kuoneka upo na high life sema ndio utaratibu uliopo kwa watz
Kama mie nokia kesha niteka kabisa na ile camera ya carl zesis yaani sio ile yenye window au android kama ina camera ya carl basi mie roho yangu inapoa kabisaWabongo utawaweza, mtu ukisema ujitafutie kitu chako cha kudumu kinachokuridhisha, utasikia wanakuita limbukeni, mi siwezi pangiwa lakufanya vile vile kupangiwa aina ya simu ya kutumia.
Mwisho wa siku kila mtu amiliki apendacho atumie apendacho