Kiboko ya Lowassa Afariki Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiboko ya Lowassa Afariki Dunia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Mar 12, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  MKUU wa Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza, Serenge Mrenge, amefariki nchini India alikokuwa akitibiwa maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
  Kifo cha mkuu huyo wa wilaya ya Ilemela kimetokea juzi nchini India ambapo alikuwa akitibiwa ugonjwa wa tumbo uliokuwa ukimtatiza kwa kipindi kirefu sasa.
  Akithibitisha jana kifo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, aliiambia Tanzania Daima: “DC Mrenge amefariki jana (juzi), nchini India, alikokuwa akipatiwa huduma za kitabibu za ugonjwa wa tumbo uliokuwa ukimsumbua.”
  RC Kandoro alisema mkuu huyo wa wilaya ya Ilemela alipelekwa nje ya nchi zaidi ya wiki tatu zilizopita, baada ya Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya jijini Mwanza, kushindwa kumtibu na kutoa kibali cha kupelekwa nchini India kwa matibabu ya tumbo ambapo mauti yamemkua huko.
  Kifo cha mkuu huyo wa wilaya kimekuja miezi michache baada ya mkuu wa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Creophat Rugarabamu, kufariki nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya shinikizo la damu.
  Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, mwili wa marehemu Mrenge atasafirishwa kutoka nchini India na kufika katika uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Dar es Salaam siku ya kesho Jumapili na baadaye kusafirishwa hadi nyumbani kwao jijini Tanga kwa ajili ya mazishi.
  “Mwili wa marehemu Mrenge utafika Dar es Salaam Jumapili wiki hii ukitokea India...na baada ya hapo shughuli za kiserikali za kumsafirisha hadi Tanga nyumbani kwao zitafanyika. Mungu alitwaa na Mungu ametoa...Amina,” alisema Kandoro akionekana kugubikwa na majonzi.
  Awali ilielezwa kwamba Mrenge alipelekwa nchini India akisumbuliwa na ugonjwa wa figo, huku taarifa nyingine zikidai anasumbuliwa na shinikizo la damu.
  Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu Serenge Mrenge, Amina.
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  DC Ilemela afariki

  na Sitta Tumma, Mwanza


  MKUU wa Wilaya ya Ilemela Jijini Mwanza, Serenge Mrenge, amefariki nchini India alikokuwa akitibiwa maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.


  Kifo cha mkuu huyo wa wilaya ya Ilemela kimetokea juzi nchini India ambapo alikuwa akitibiwa ugonjwa wa tumbo uliokuwa ukimtatiza kwa kipindi kirefu sasa.


  Akithibitisha jana kifo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, aliiambia Tanzania Daima: "DC Mrenge amefariki jana (juzi), nchini India, alikokuwa akipatiwa huduma za kitabibu za ugonjwa wa tumbo uliokuwa ukimsumbua."


  RC Kandoro alisema mkuu huyo wa wilaya ya Ilemela alipelekwa nje ya nchi zaidi ya wiki tatu zilizopita, baada ya Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya jijini Mwanza, kushindwa kumtibu na kutoa kibali cha kupelekwa nchini India kwa matibabu ya tumbo ambapo mauti yamemkua huko.


  Kifo cha mkuu huyo wa wilaya kimekuja miezi michache baada ya mkuu wa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Creophat Rugarabamu, kufariki nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya shinikizo la damu.


  Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, mwili wa marehemu Mrenge atasafirishwa kutoka nchini India na kufika katika uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Dar es Salaam siku ya kesho Jumapili na baadaye kusafirishwa hadi nyumbani kwao jijini Tanga kwa ajili ya mazishi.


  "Mwili wa marehemu Mrenge utafika Dar es Salaam Jumapili wiki hii ukitokea India...na baada ya hapo shughuli za kiserikali za kumsafirisha hadi Tanga nyumbani kwao zitafanyika. Mungu alitwaa na Mungu ametoa...Amina," alisema Kandoro akionekana kugubikwa na majonzi.


  Awali ilielezwa kwamba Mrenge alipelekwa nchini India akisumbuliwa na ugonjwa wa figo, huku taarifa nyingine zikidai anasumbuliwa na shinikizo la damu.


  Mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu Serenge Mrenge, Amina.


  Source:Mtanzania Daima
   
 3. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 3,193
  Trophy Points: 280
  Poleni wafiwa. Lakini hiyo ya kuwa na taarifa tofauti ya ugonjwa inakuwaje tena!
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Poleni ndugu, jamaa na marafiki.
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Lakini,............ Hivi ni kwa nini wanasiasa wote lazima wapelekwe india kwa matibabu?............. tena utakuta maradhi yenyewe ya kawaida tu............... Any way huu ni msiba, tusizame kwenye kuhoji mambo ya gharama za kuuguza nje ya nchi na kusafirishia maiti............ After all TZ kwa sasa inaendeshwa kama haina mwenyewe vile........... Ukizungumza haya waweza kuitwa mhaini ............. Unachochea vurugu nchi isitawalike....................

  Rip mh. Na poleni wafiwa wote..........
   
 6. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poleni wafiwa,lakini c wakati anapelekwa india babu wa loliondo alishaanza tiba?au dharau?
   
 7. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #7
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa babu angekubali/serikali ingekubali kufuata mstari/foleni?
  Pia nahisi ni kupuuza .
   
 8. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Poleni wafiwa.
  Lakini mbona wakuu wa wilaya za Mwanza ambako CCM ilipoteza kwenye Ubunge (Nyamagana na Ilemela) ndio wakuu wake wa Wilaya wamekufa? Kunani?
   
 9. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kupunguza gharama viongoz wote wakiumwa waache zarau waende loliondo Tsh 500 tu. Mkuu wa mkoa wa Mara aliumwa akaenda kwa babu loliondo sasa hv afya yake ipo ngangari huyu mkuu wa wilaya ameenda india akiwa hai karud no uhai, RIP BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
   
 10. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Poleni wafiwa!
   
 11. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  may he rest in peace!
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  rip mkuu wa wilaya
   
 13. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  RIP mh.......hivi angewahi kwa babu si angepona jamani au kwa vile tunaamini kila kifo ni Mungu ndio anapanga?.
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mungu ailaze roho ya marehemu, Ameeen.
   
 15. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza Luteni Kanali Mstaafu Serenge Mrengo amefariki Dunia.
  Source; Habari Leo:hug:
   
 16. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nafikiri Muhimbili wangeweza kumtibu.Ndiyo hypocricy ya hawa elites wa SISIEM na Serikali.
   
 17. s

  smz JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bibikuku,

  Kama kumbukumbu zangu zinanipa vizuri kauli hiyo ilitolewa na Col Madaha aliyekuwa DC wa Nymagana wakati huo. Siyo Serenge(RIP).

  Pengine mwenye uhakika 100% atusaidie.
   
 18. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Yah. Aliyepambana na Lowasa pale chuo cha benki kuu mwanza ni Kanali Madaha.
   
 19. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  jamaa kakurupuka tuu
   
 20. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  owassa blasts District Commissioner

  JOHN KULEKANA, Mwanza
  Daily News; Friday,September 28, 2007 @00:02

  THE Prime Minister, Mr Edward Lowassa, yesterday rejected the Nyamagana District development report, saying it had false information.

  "This is the worst report I have ever seen since becoming Prime Minister. It is a shame and in my opinion there is no leadership here," Mr Lowassa told the District Commissioner, Mr Peter Madaha.

  The prime minister is on a week-long tour of Mwanza region. The premier disagreed with the report on secondary school progress in the district. Pressed, the DC disowned the report saying education officials had misled him.

  The DC again told the prime minister that there was no cultivation of cotton in the district. However, officials from the agricultural department had told the premier that cotton is cultivated in two wards.

  "You are wasting my time by coming with this embarrassing report which you are disagreeing amongst yourselves," Mr Lowassa said angrily, adding: "it appears that you are not working collectively."

  "I'm very sorry Mr Prime Minister; it is a problem of my experts who came up with this misleading report. I'm a good leader with 24 years experience as a district commissioner but I repeat that I'm very sorry," Mr Madaha said.
  Source: Daily News/HomeNews.
   
Loading...