Kiboko Albino agunduliwa Masai Mara

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
ImageUploadedByJamiiForums1451733689.915002.jpg

Gazeti la Uingereza Daily Mali limesema, mtalii kutoka Ufaransa Bibi Laurent na mume wake Dominique Renaud wamegundua kiboko wa rangi ya waridi kwenye mbuga ya wanyamapori ya Masai Mara nchini Kenya.
Utafiti unaonesha kuwa ngozi ya waridi ya kiboko huyo inatokana na kuwa albino.
 
Waligundua ziwa Victoria na wasukus wapo hapo hapo yaani hawa wazungu ni watu wa ajabu sana yaani kumuona ndo kugundua?
 
Wazungu wanapenda sifa za kijinga,Rebman agundua Mlima Kilimanjaro wakati wachagga wapo eneo hilo wakiamka asubuhi wanauona mlima wakitaka kuni wanakwenda mlimani,wakitaka dawa za miti shamba wanapanda mlima lakini mzungu toka Ulaya anadai kaugundua.
 
ugunduzi wa wazungu huwa hauishi, wanaweza kusema wamegundua panya akitaga mayai
 
Waligundua ziwa Victoria na wasukus wapo hapo hapo yaani hawa wazungu ni watu wa ajabu sana yaani kumuona ndo kugundua?

Yaani wenyewe wanajua Dunia ni wazungu tu, kwahyo kama kitu hakijaonwa na mzungu inamaana watu wote hawajawahi kukiona. Ndo maana wanasema wamegundua mlima Kilimajaro wakati wachaga wapo, victoria wakati wasukuma, wahaya, waganda, wajita n.k walikuepo tangia zamani. Kwahyo ukute kuna wenyenyi wa maeneo hayo walishamuona huyo kiboko tangu zamani lakini ikaishia hapo. Huku Afrika hata ukipiga picha ukapela kwenye vyombo vya habar ikajulikana kwa watu hakuna utakachokipata. Hivyo wanaothamini watu wanaogundua vitu kwao wakathaminiwa acha waendelee kugundua.
 
Mkuu
Usemacho Ni Kweli Tupu
Halafu Unaweza Kukuta Kiboko Huyo Mgonjwa Wao Wanasema Albinos
Sema huyo kiboko ana bahati wakenya wana elimu, ingekuwa hapa bongo hiyo ilikuwa bonge la dili na sidhani kama angeendelea kuishi kwa zaidi ya siku mbili
 
View attachment 314365

Gazeti la Uingereza Daily Mali limesema, mtalii kutoka Ufaransa Bibi Laurent na mume wake Dominique Renaud wamegundua kiboko wa rangi ya waridi kwenye mbuga ya wanyamapori ya Masai Mara nchini Kenya.
Utafiti unaonesha kuwa ngozi ya waridi ya kiboko huyo inatokana na kuwa albino.
Samahani mkuu @Kibo10,hivi waweza kunipa hiyo linki ya hii habari niisachi maana nimeitafuta nimeikosa au niambie hilo gazeti lilikuwa la lini.
 
Waligundua binadamu alikuwa sokwe akapitia mabadiliko hadi kuwa binadam kamili sasa masokwe yapo tele maporini hko cjui yatabdilika lini... na cjui wenyew wametokea sayar gan manak masokwe waliopo ni wa kiafrika tu..
 
Mkuu achana nao hao. Siku zote wanatufanya sisi wajinga sana, cha ajabu ni kwamba huko makwao tumesoma nao darasa moja, hamna kitu kabisa ni weupe, wengine walikuwa wanapiga chabo wapuuzeni na tufuate yetu.
 
Kwani nyie waafrika mlishindwa vipi kumgundua huyo kiboko na kumtangaza?! Tunajifanya tuna uchungu wakati hata kutembelea mbuga au hifadhi zetu ni msamiati. Acheni unafiki!
 
Kwani nyie waafrika mlishindwa vipi kumgundua huyo kiboko na kumtangaza?! Tunajifanya tuna uchungu wakati hata kutembelea mbuga au hifadhi zetu ni msamiati. Acheni unafiki!

Mkuu hilo si suala la ugunduzi, mifano hai umepewa Ziwa Victoria, Mlima Kilimanjaro hivi vyote vipo siku nyingi na wàtu wanaishi maeneo hayo kwa miaka Dahar leo anazuka mtu na kusema amegundua hivyo vitu, hivi kweli inaingia akilini, kwa taarifa tu huyo hippopatamus sp. kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na ugonjwa wa ngozi.
 
Back
Top Bottom