PreGE2025 Kibango cha "No reforms No election" chatua Club ya Small Planet, wamiliki wakikana

PreGE2025 Kibango cha "No reforms No election" chatua Club ya Small Planet, wamiliki wakikana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
13,792
Reaction score
39,377
Baada ya video iliyoonyesha bango mjongeo lilikokuwa na ujumbe wa no reforms no elections, uongozi wa Bar ya Small Planet iliyopo Sinza waibuka na kulaani vikali tukio hilo ukisema hawahusiki na kilichotokea.

---
Uongozi wa kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED ambayo ni miliki wa bar ya Small Planet - Sinza, umesikitishwa na unalaani vikali jambo ambalo limetokea katika usiku wa Jumamosi ya tarehe 07/06/2025 kuamkia Jumapili ya 08/06/2025 ambapo kumeonekana kuwa na Bango Mjongeo (Mobile Billboard) likiwa lina jumbe zenye viashiria vya kisiasa.

Kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED na Bar yake ya Small Planet - Sinza, inafanya shughuli zake chini ya sheria na hakuna namna yoyote inafungamana na upande wowote wa kisiasa hivyo jumbe iliyoonekana ikitembea katika mitandao ya kijamii ni njama tu za kikundi fulani kwa lengo la kuchafua taswira nzima ya Bar yetu kwenye upande wa ushindani wa kibiashara.

Kilichotokea ni kwamba, mmoja wa wahudumu wetu akiwa katika utendaji kazi wake alishinikizwa na moja ya mteja mwenye maslahi yake binafsi na kulazimisha kuandikwa kwa jumbe hiyo yenye viashiria vya siasa na kulazimisha itangazwe kwenye Bango Mjongeo la Bar yetu na kisha kurekodi na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kampuni ya SMALL PLANET ENTERPRISES LIMITED na Bar yake ya Small Planet - Sinza, imeshaanza kuchukua hatua za kisheria kufuatilia ni nani aliyelazimisha jumbe hizo za kisiasa kuandikwa na kutangazwa katika bar yetu ili sheria iweze kufuata mkondo wake.

1000039753.jpg
 
Baada ya video iliyoonyesha bango mjongeo lilikokuwa na ujumbe wa no reforms no elections, uongozi wa Bar ya Small Planet iliyopo Sinza waibuka na kulaani vikali tukio hilo ukisema hawahusiki na kilichotokea.
View attachment 3360861
Nchi hii siyo huru.kabida check wanavyolialia. Wana madudu kibaO YamefIchwa na CCM
 
Baada ya video iliyoonyesha bango mjongeo lilikokuwa na ujumbe wa no reforms no elections, uongozi wa Bar ya Small Planet iliyopo Sinza waibuka na kulaani vikali tukio hilo ukisema hawahusiki na kilichotokea.
View attachment 3360861
Ujumbe umefika

Hata hivyo uongozi wenu mnaakili kama za Viongozi wa No reforms no election
 
Back
Top Bottom