MKALIKENYA
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,196
- 486
maamuzi aliyoyafanya zitto mwaka 2009 yakuamua kujitoa ndiyo yanayomgharimu leo hii,nadhani huu ni wakati wakuruhusu demokrasia iamue ndani ya vyama vyetu vya siasa.bila shaka zitto hayuko tayari kurudia makosa aliyokwisha yafanya.lets democracy decide.
If I were you, I would have never opened my big mouth any more and spit anything out more that what I have vomited kwenye kadamnasi ya jf, mpaka baada ya vikao vyenu vya nidhamu vya ndani!.maamuzi aliyoyafanya zitto mwaka 2009 yakuamua kujitoa ndiyo yanayomgharimu leo hii,nadhani huu ni wakati wakuruhusu demokrasia iamue ndani ya vyama vyetu vya siasa.bila shaka zitto hayuko tayari kurudia makosa aliyokwisha yafanya.lets democracy decide.
Kibanda kwenye makala hii umekuwa upande mmoja wa Mbowe,unasema kuwa Zitto ni kijana na unakubali amesimamia mambo makubwa ya kisiasa nchini, pia amekuwa naibu Katibu mkuu kwanini ashindwe kusimamia kazi ya uenyekiti wakati Mtendaji mkuu wa chama ni katibu mkuu? Zitto awe na subira kwani hujui kuwa muda uliopo ndio wako na muda ujao si wako? una maana vijana ni taifa la Kesho? JK amekuwa naibu Katibu mkuu wa CCM akiwa na miaka 25.
amekuwa naibu waziri kwenye wizara nzito ya nishati akiwa na miaka 33.kama ZITTO ana SHINE bungeni kwanini ashindwe uenyekiti wa Chadema?
Ahsante mkuu Pasco,
Niseme tu kwamba hakuna kijana aliweza kuvutia wengi ktk miaka ya hiv karibuni kama Zitto, binafsi bado sijaona Zitto alikosa nini CHADEMA mpaka aanze kubadilika, kipindi kile mzee wetu Edwin Mtei aliposema kwamba "WE CAN NO CHOOSE A MAN FROM NO WHERE"( if am not mistaken).
alikuwa amemaanisha kwani anajua changamoto za kiuongozi sasa hebu fikiri leo hii Zitto ndio angekuwa mwenyekiti wa CHADEMA na tabia zake hizi sijui chama kingekuwa wapi.
Zitto jua kwamba mpaka muda huu umekwisha poteza imani mbele ya watu wote makini hapa nchini.
Shardcole@Tabora1
mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe.
Hahahaaaa awaachie chadema yenu,eeh kumbe chadema ina wenyewe
zitto ana kadi moja atapotezaje imani kwa wananchi?
Pasco, huu ni ushauri mzuri sana, kuna kipindi ambapo watu wanafanya "re-organisation and re-construction", ni bora Juliana Shonza akae kimya na wajipande upya, ZZK ni mjanja sana, lazima atakuja na single ya kujiweka sawa ndani ya CDM, only time will tell, let us wait and see!
Mpaka sasa bado huamini?Du, kuna watu humu tumetoka mbali na ZZK!, nikukukmbuka nilivyomfagilia hapa, na hizi tuhuma zinazoelekezwa kwake saa hizi, naamini ni za uongo, na nitaendelea kusimama nae!.
naungana kabisa na Bw Kibanda. Zito ingawa katiba inakuruhusu pasi na shaka lakini wewe bado kabisa kukomaa kisiasa anahitaji takriban miaka mitano zaidi ya kujijenga kisiasa kabla ya kuamua kugombea uongozi wa juu kabisa wa chama.
Zito kama kweli unataka uongozi wa juu kabisa katika siasa unahitaji upate uzoefu zaidi. uwe na subra.
lakini ukiangalia kwa upande mwingine inaweza ikawa ni ujanja wa kisiasa wa chadema kuonyesha kuwa Mbowe nae kapata mpinzani.
Binti bado hujachelewa msamaha bado upo, nenda katubu kwa viongozi wako usamehewe.mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe.
Kwanini anang'ang'ania huko Chadema kama anahisi hawamtaki kwa sababu ya dini yake na mkoa wake?uchaguzi uliopita alipotaka kumtest mbowe kwenye position hii hii wazee wa chama walimwambia hayo maneno unayomwambia wewe leo,sasa atakua mtu wa kusubiri mpaka lini?mnyonge mnyongeni...mi naona tatizo la zitto ni dini yake na mahali atokako-kigoma
Macos
Naheshimu mawazo na mtazamo wako. Hofu yangu ni kuwa kama umekuja kumtetea sidhani kama umefaulu maana mtu mwenye akili akisoma maneno yako vizuri ataona unamwangamiza Zitto kwa utetezi huu.
Unazidi kuthibitisha tuhuma ambazo hazipo katika tuhuma zinazozunguka sasa. So sad!
Pasco, nadhani bandiko la kibanda lilihitimisha vizuri tu. Wengi tumekuwa tukimsihi kuwa na subira, apunguze jazba na awe more professional. Kwa bahati mbaya hasikii wala haoni.
Kwa tuhuma hizi za uhujumu, anguko lake kisiasa ni dhahiri kama halipo njiani.
Tuhuma zinazomkabili zinamuondolea sehemu kubwa sana ya sifa za uongozi hata kama ni kiongozi kwa mwonekano.
Nafasi aliyo nayo ya kujirudi au kuzuia uharibu ''damage control'' ni yeye kujitoa kimaso maso bila msaada wa vijana ambao kisiasa ni wachanga na kifikra ni weupe sana.
Zitto anapaswa kuachia ngazi katika uongozi kwa sasa ikiwa ni hatua ya kuwajibika na ku-reset the button.
Jitihada zake za kutaka kuona nyumba inaunguka kwa msemo wa 'namwaga mboga mwaga ugali'' zinaweza zizifanikiwe kwasababu washirika wake hawaonekani kuwa watu makini.
Ningemshauri Zitto awaase vijana wake wasimwage mpunga kwenye kuku wengi na kukaa kimya ni busara na msaada kwake
The only window of opportunity ni yeye kuachia ngazi katika uongozi.
Aachie ngazi kwa sababu amedhihirisha betrayal, amepoteza trust na moral authority yake imekuwa severely compromized. Hizi jitihada za kuwatumia immature political gangs kumsafisha zitahitimisha safari yake mapema sana.
Kiwango na umaarufu aliofikia Zitto halafu uangalie timu aliyokuwa anafanya nayo kazi kichini chini ni ushahidi kuwa pamoja na vision na mission anazoonekane kuwa nazo, politically ni immature na ameonyesha poor judgement kama kiongozi. Zitto anahitaji muda akomae kisiasa na hili litabaki kuwa donda ndugu.
Zitto, kama unakipenda chama chako na unapenda ustawi wa taifa hili, ni wakati muafaka kabisa uweke masilahi yako pembeni kwa kuachia uongozi ili uwe mfano wa vijana shupavu wanaokubali kuwajibika.
Kwasasa huna moral ya kumyooshea kidole Mizengo Pinda ajiuzulu kwa kutowawajibisha mawaziri maana wewe hujafanya hivyo.
maamuzi aliyoyafanya zitto mwaka 2009 yakuamua kujitoa ndiyo yanayomgharimu leo hii,nadhani huu ni wakati wakuruhusu demokrasia iamue ndani ya vyama vyetu vya siasa.bila shaka zitto hayuko tayari kurudia makosa aliyokwisha yafanya.lets democracy decide.
mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe.
Du, kuna watu humu tumetoka mbali na ZZK!, nikukukmbuka nilivyomfagilia hapa, na hizi tuhuma zinazoelekezwa kwake saa hizi, naamini ni za uongo, na nitaendelea kusimama nae!.