Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.
Jamani Kibanda mwache dogo agombee uongozi si ni demokrasia? na vilevile kubadilishana vijiti? kuna ubaya gani nayeye mbowe akapumzika, aruhusu wengine? au yeye ni mwenyekiti wa maisha wa chadema?
 

Labda nikuambie wazi kuwa mimi si mwana-CHADEMA bali mwanaharakati wa demokrasia hivyo sina nyaraka/katiba/kanuni zao. Isipokuwa ninazo taarifa kuwa Msafiri Mtetemelwa ameondolewa ktk kazi ya kusimamia kutoa na kupokea fomu za wagombea kwasababu ya kuvuruga taratibu. Vurugu hiyo ni kumchukulia na kurudisha fomu ya mgombea mmoja wapo ambaye ni Zitto. Msafiri kama Afisa uchaguzi hakupaswa kufanya hivyo hii ni logi tu.
 

Miaka 10 asubiri nini?....muda huu chadema ishapata platform ndio muda wake...what if wakipigwa bao 2010 na kukosa hata kiti kimoja...like happened to CUF 2005....nguvu zao wote zitawaishia..si tu Zitto hata wapambe...!!!

Pia kwa mtaji wenu/wako wa Zitto asubiri 2014/15...Kizazi kingine hapo kitaibuka....

Pia kwa mtaji wenu/wako Tusimlaumu Kikwete maana JK ndie Kiongozi pekee wa CCM ambae Siasa ndani ya CCM kaianzia Mbali sana....kaanza Ngazi ndogo hadi kapanda juu...!!! Na nini anafanya sasa?...

Mwisho nawatakia Uchaguzi mwema...!!!
 

We unachokonoa tu watu waanze kusema mfaidike....Huu ni mpambano wa kisayansi kaka sio enzi za kina marandu na mrema...

Endelea kujifurahisha na hizi za KUSADIKIKA zako na wenzio kwenye mikakati yenu...

Na hatusemi ng'o mnayotaka tuseme. HATUDANGANYIKI.....

omarilyas
 
Sidhani kwamba Chadema ni wakosa ufahamu kiasi cha kumchagua Zitto awe Mwenyekiti kwa sasa. Wakifanya hivyo watakuwa wamepunguza hadhi ya Chama. Zitto hana uwezo wa kuwa kiongozi wa Chadema kwa sasa.
 
Zitto tunakupenda lakini angalia usiwe unatumika na maadui wa chadema bila kujua,chadema kwa sasa ina wapenzi wengi sana lakini msipokuwa makini uchaguzi huu utakuwa anguko lenu.
 

NA UNGEONGEZEA KUWA, ILI MBOWE NA WAHUSIKA KUJISAFISHA KANDA AOMBWE AJIUZULU UHARIRI WA GAZETI, AU APEWE ONYO BY THE WONER, BY THIS UN-ETHICAL BEHAVIOUR, BY BLUNTLY ATTACKING A MEMBER OF A POLITICAL PARTY WHO WANTS JUST TO PRACTICE HIS DEMOCRATIC RIGHTS! KIBANDA HAD THE OPPORTUNITY TO DISCUSS THIS MATTER PRIVATELY WITH ZITTO.

Ni kweli Mr. Kibanda ame "bleach" rights and "privacy" ya Mr. Zitto; and all other young Members; he need to apologize otherwise this is going to affect the morale of the party members.

Tungeongelea zaidi uwezo wa Zitto kuleta "Horoscope".
 
Uchaguzi ukimalizika Chadema inatakiwa ifanye kazi tatu...

1. watafanya nini wakipewa madaraka/dola... hapa inabidi waende au wazunguke kila kijiji na kuzitangaza sera zao kwa powerpoint presentation mfano wa yale matangazo ya ujenzi wa olympic London...
Nashauri kwamba watangaze kuijenga Tanzania katika nyanja ambazo zitakuza uchumi wetu , sera za kuifanya Tanzania kuwa na huduma bora za jamii za kuigwa ndani ya Afrika, na pia kuunganisha mikoa yote ya Tanzania kwa barabara za lami ije mvua ije masika, liwake au lisiwake. Pia kutangaza na kutekeleza kwa vitendo kwamba umeme utasambazwa vijijini kote na mgao utakuwa historia... Maji pia hivyo hivyo...
Kila kijiji kitakuwa na doctor wake ambaye atakuwa mahsusi kwa watu wa kijiji hicho kwa mtindo wa ki general practitiner wa nchi kama ya uingereza.

katika powepoint presentation hiyo waje na mchanganuo wa mahesabu ya ku-set up huduma za jamii... namna gani watapata mapato ya kuzianzisha au kuzilipia, kuzisimamia na namna gani au kwa kipindi gani huduma hizo zitakuwa zimeanza kutengenezwa sema ndani ya miaka 5 ya madaraka.
Kwa mfano... waseme kwamba kila nyumba vijijini Tanzania zitapewa mikopo ya bila Riba (Serikali italipia Riba) ili ziwekewe solar power na kuondokana na Tatizo la umeme... mfano wanaweza kutangaza mil 7 ambazo kwa uzoefu wangu zinaweza kutoa umeme wa solar guaranteed for 25 yrs by BP Tanzania (BP sio kampuni pekee na kuitaja sio kwamba naipigia debe)

2. Waseme kwamba Mafisadi wote waliojilimbikizia mali ya uma kwa tamaa watashughulikiwa kwa mtindo wa Ki-China kwa adhabu kali sana wasiporudisha mali ya umma wa Watanzania, ikiwa ni pamoja ni kifungo cha maisha na watarekebisha katiba au kutunga sheria ili kosa la ufisadi lipewe adhabu ya kifo na ikibidi watoe mfano wa adhabu kwa fisadi yeyote yule ili kutoa onyo au fundisho kwa mafisadi wa baadae...
Hii itaonesha kwamba wako serious na wanayoyasema na kwamba kuwatangaza mafisadi pekee haisaidii maana tayari jamii kubwa ya watanzania sasa tunakubali kwamba ufisadi upo na unatetewa kwa kiasi kikubwa na chama tawala hivyo kuwaimba pekee mafisadi haitoshi inabidi tuwaimbe (name and shame) na pia waseme watawafanya nini wakipewa madaraka...

3. Mwisho watangaze kwa vitendo kwamba njaa katika maeneo yote ya Tanzania itakuwa historia na kwamba nchi itaanza kutoa misaada ya chakula kwa nchi nyingine kama ethiopia, somalia na kwingineko kama Zimbabwe...
 
Hapana Shaka kuwa CHADEMA watachagua watu makini sana na hata kupeleka mbele mambo yote yalikwenda kinyume na matarajiao ya watu wengi
 
Yale yale ya CCM!
 
Sidhani kwamba Chadema ni wakosa ufahamu kiasi cha kumchagua Zitto awe Mwenyekiti kwa sasa. Wakifanya hivyo watakuwa wamepunguza hadhi ya Chama. Zitto hana uwezo wa kuwa kiongozi wa Chadema kwa sasa.

Wachaga hawawezi kukubali CHADEMA iondoke mikononi mwao. Labda Zitto aoe Mchaga mwenzao ndio watamwachia hicho chama.

Zitto ana uwezo wa kuongoza CHADEMA kuliko Mbowe; labda tatizo lenu hapa ni Uchaga tu.

Ni uwezo gani huo mnaoongelea kwamba Zitto hana?

Tumegundua janja yenu!
 
Ni funzo kubwa sana kwa CCM hata kama ni Mwakani apate mpinzani na wakati wa kupita bila kupigwa umepitwa na wakati!! Kuna haja kila mtu kupata mpinzania. tunataka kila upande watoke watu na kugombea na hivyo kufanya demokrasia ya kweli kabisa. Tunasubiri mwakani pia JK naye apate mpinzani
 
Salamu za NCCR-MAGEUZI kwa Chadema.

CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimemtaka Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kabwe Zitto kutoogopa wakati huu wa mchakato wa uchaguzi katika chama hicho na kwamba awe makini huku akiongeza mapambano.

Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Kampeni na Uchaguzi wa NCCR-Mageuzi, Faustin Sungura aliliambia gazeti hili jana Dar es Salaam kwamba wanamshauri mwanasiasa huyo kijana kutumia fursa hiyo kuondoa sura ya ukabila ndani ya vyama vya siasa nchini.

Alisema wakati huu ambao Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Zitto wanapambana kuwania uenyekiti, ni vyema akawa makini huku akiongeza kasi ya mapambano.

"Kwa kuwa Chadema ni chama chenye kujali demokrasia, hawana budi kuonesha umma jinsi ambavyo watachagua kiongozi wakizingatia hilo," alisema Sungura na kutahadharisha kuwa katika kipindi hiki, isijekutokea kukawa na kushuka kwa demokrasia ndani ya chama hicho.

Alisema wakati huu uwe ndio fursa ya kuondoa sura ya ukabila ndani ya chama kwa maslahi yao. "Inatubidi kusema hivyo kwa kuwa hakuna uwiano katika viti maalumu vya ubunge kwa wanawake kwa chama hicho ambapo kati ya viti hivyo vya ubunge, vitatu vinatoka katika familia moja," alidai Sungura.

Alidai kuwa katika hilo, hahitaji ushahidi mwingine kuwa kuna sura ya ukabila katika chama hicho, na kwamba viti hivyo vya ubunge vingegawanywa angalau katika jimbo lisilokuwa na mbunge.

Yamekuwepo madai ya Chadema kuwa na wabunge wengi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro hasa wale wa kuteuliwa wa Viti Maalumu ambao ni Grace Kihwelu, Lucy Owenya, Susan Lyimo na Halima Mdee. Wabunge wake wengine wa viti hivyo ni Mhonga Ruhanywa na Maulidah Komu.

Kiongozi huyo wa NCCR Mageuzi alisema kwa maslahi ya Taifa, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wanatakiwa kuona mbali zaidi na kuzingatia demokrasia iliyo wazi

Mkutano Mkuu wa Chadema utafanyika wiki ijayo. Kuhusu kuondoka kwa aliyekuwa Katibu Mwenezi wa NCCR Mageuzi, Joseph Selasini aliyehamia Chadema, Sungura alisema jambo la kujivunia.
source habarileo.co.tz
 
Last edited:
Pamoja na mapungufu ya Kibanda,
Waanzilishi na wachangiaji wengi wa thread hii ni wale wa chama cha kijani ..............😀
Chadema mpo??????????????????
Mwenye macho na masikio na asikie!
Aliyeanzisha mjadala huu Kibanda mimi nimeutoa kwenye gazeti lake.
 
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=282
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kabwe Zitto, amesema hana mpango wa kuondoa fomu yake ya kugombea uenyekiti wa chama hicho, kwa kuwa ni haki yake na ana sifa za kuwa Mwenyekiti.
Pia Zitto amekanusha taarifa kuwa fomu zake zilirejeshwa na watu wanaoshinikiza awanie nafasi hiyo kwa lengo la kukibomoa chama hicho na kusema kama ni shinikizo basi ameshinikizwa na wana Chadema na si mtu wa pembeni. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Zitto alikiri kuchukua fomu na kufuata taratibu zinazotakiwa na kama kuna tofauti ni mbinu za kisiasa.

"Hii ni staili tu, nisingeweza kuchukua mdundiko, kwanza nilikuwa jimboni kisha nilikuwa na safari ya Ujerumani hata fomu zenyewe nilijazia Uwanjani (wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere)," alisema.

Aliongeza kuwa yamesemwa maneno mengi kumhusu pamoja na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ambayo aliyaita ya siasa za kampeni na kuwa anatarajia yatakwisha baada ya uchaguzi, kwa kuwa wote lengo lao ni kuimarisha chama hicho.

"Chama hiki si changu, wala si cha Mbowe, sisi tutaondoka chama kitabaki hapahapa na uamuzi wangu kugombea, ni jambo la kawaida wala sihitaji mpasuko au mgawanyiko, mwaka 1998 Bob Makani na Philemon Ndesamburo waligombea nafasi hii wakatofautiana, lakini baada ya uchaguzi, waliungana na kuendeleza chama," alisema Zitto.

Alisema alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa na uwezo wa kukipeleka mbali chama hicho na hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi, ambapo inatarajiwa kuwapo vijana wapya wapiga kura wapatao milioni 6.3 hivyo ni vyema chama kijipambanue kwa kuongozwa na kijana.

Alitamba kuwa anajiamini kuwa na uwezo katika kukiongoza chama hicho hasa ikizingatiwa kuwa katika nafasi yake ya ubunge wa Kigoma Kaskazini, ameongoza kamati muhimu ya Bunge, ya Hesabu za Mashirika ya Umma, iliyo na mashirika yenye thamani ya zaidi ya Sh trilioni tano.

"Nikiwa kijana kama wanavyodai, kwa nini niweze kuongoza kamati hiyo ila nishindwe chama chenye mapato ya Sh bilioni 72 kwa mwezi? Hata hivyo binafsi sikupenda kugombea uenyekiti, lakini nimeombwa sana na wanachama na kujikuta najaza fomu hizi," alisema.

Alisema amekuwa kwenye chama hicho tangu akiwa na umri wa miaka 16 na kupitia ngazi mbalimbali za uongozi ndani na nje ya chama hicho, hivyo anaamini sifa za kushika wadhifa huo anazo kwa kuwa anakifahamu vyema.

"Na itakuwa ni ajabu kutumiwa kukiharibu chama hiki, haya ni maneno ya siasa na yatakwisha kampeni zikimalizika," aliongeza.

Aliwataka waliozusha na kutunga uongo dhidi yake, watambue kuwa yeye si mtu wa visasi, lakini pia uchaguzi unapita na maisha baada ya hapo yataendelea, lakini pia akasema haamini kama chama hicho kimetawaliwa na ukabila kama inavyodaiwa.

Hata hivyo, alionyesha masikitiko yake kwa gazeti linalotoka kila siku lililoandika habari dhidi yake ikionesha wazi kuwa linatumiwa, na hivyo kuleta dhana kwamba ukabila ndani ya chama hicho upo, kwa kuwa gazeti hilo mmiliki na mhariri wake ni Wachaga.

"Hata hivyo, nikichaguliwa kuwa Mwenyekiti dhana hiyo ya ukabila itaacha kuwa na nguvu," alisema. Alisema leo wazee wa chama hicho wanatarajia kukutana na wagombea hao wawili kujadili na kuangalia tofauti zilizojitokeza. Wanaotarajiwa kukutana ni Profesa Mwesiga Baregu, Bob Makani, Anthony Ngaiza na Edwin Mtei.
 
Last edited:
Kibanda,
Mkuu bado upo yaani ujerudi kweli kuelezea Ushahidi wako hata baada ya JF members kuamiwa to disregard ushidi wako kutokana na Conflict of Interest!..

Duh ama kweli sasa umetuchosha mkuu wangu, unaposhindwa kuelewa wakati wewe ni mwandishi mzuri inatia kinyaa ... samahani lakini.
Labda nikwambie kwa lugha ya Kidanganyika.
Mkuu hakuna mtu anayesema kuwa maelezo yako ni Uongo au hayana ukweli tatizo ni kwamba wewe ni mwajiriwa wa Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa chama Chadema hukutakiwa kuanzisha habari hii ktk gazeti hilo ukichukua ushindani dhidi ya mwajiri wako kuwa ni batili..Tanzania Daima sii Gazeti la chama na wala ujumbe ulotoa haukisaidii chama kwani kama kweli ulidhamiria kukisaidia chama ungepeleka malalamiko haya ktk vyombo husika vya chama na sheria za chama kuhusiana na uchukuaji form au uchaguzi zingetazamwa.
Bila shaka wewe ni mwanachama wa Cjhadema au sio?..
Halafu basi Ktk mchezo wa Siasa unaokubalika, mara zote zote Challenger kama Zitto aliyechukua form kugombea Kiti against Mbowe ndiye hutaklwa kutangaza na kusema ovyo badala yake tunaona wewe mshabiki ukichukua mkuki na kutumbukiza kabla hata mashindano hayajaanza..
Njia bora ulotakiwa kuitumia ilikuwa kwenda kumhoji Mbowe, jinsi gani amechukulia swala hili na nini sheria au taratibu za kugombea kiti hicho na maneno haya kama yangetoka mdomoni mwa Mbowe ungekuwa umeondokana na shuku za watu..
Yes ni kweli yawezekana Zitto hana uzoefu huo, hana sheria ya kumruhusu kugombea nammengineyo mengi lakini sidhani kaa hii ni kazi yako! Na kama angekuwa na mapungufu haya ulozungumza sidhani kama angeruhusiwa kuchukua Form na Kuijaza ikapokelewa kumruhusu kushindana na Mwenuyekiti..
Binafsi wala sioni Ubaya wa Zitto kugombea kiti cha Mwenyekiti wa chama kwa sababu sio tiketi ya kuchaguliwa kugombea Urais. Tumeona mwaka jana, juzi Mbowe akishindana na watu wenginektk kiti cha Urais hata baada ya kukabidhiwa Uenyekiti..CCM wao pia wana Utaratibu wao vile vile..Hivyo swlaa sio Uwezo wa Zitto isipokuwa ni upper cut ulojaribu kuingiza imekuwa belowa the belt ndio lugha ya wanan JF.. Wewe huwezi kuona kwa sababu umeshaelemewa lakini Ukweli utabakia kuwa Ukweli..Mkuu Ulichemsha na unaendelea Kuchemsha.. Mbowe wangu na kura yangu nitampa yeye lakini sii kwa maelezo ya watu kama wewe!.. unanipa kujiuliza zaidi kuhusu Mbowe kuliko Zitto!.. Nimemaliza..
 
Nimefatilia kwa karibu sana malumbano haya kwa kipindi kirefu,napenda kukiri kuwa Zitto ni mtu ambaye tunafahamina kwa karibu sana,aidha Kibanda najuana nae kwa karibu sana pia.Omary ni classmate wangu na Kitila ni kaka yangu....................kati ya hawa hakuna hata mmoja ni mjinga na wote ni wajuvi wa kutetea hoja zao.Mimi mawazo yangu ni kuwa Zitto Kabwe anafaa na hafai kuwa mwenyekiti wa Chadema:
1.Mimi kama mwana uvccm-anafaa kwa kuwa vijana wenye uwezo ndio wakati wao kujitokeza.
2.Mwanademokrasia-hatupaswi kuogopa haki za watu kugombea basi hakuna maaana ya kuwa na vyama vingi kama tunafinya demokrasia ya ndani ya chama
3.Mwana ccm-Zitto hafai kwa kuwa ana uwezo mkubwa a kupata influence za kimataifa ni itapelekea chadema kupata misaada mingi ya kimataifa na kutusumbua kwenye chaguzi zetu.
4.mzalendo-hasigombee kwa kuwa itakidhoofisha chadema kutokana na kushindwa kutibu majeraha baada ya uchaguzi,as mpaka leo ccm haijapona majeraha ya uchaguzi uliopita
5.Mtanzania-itafuta taswira kuwa chadema ni chama cha watu wa kaskazini
 
Someni gazeti la Mwananchi leo wazee wa Chadema wanataka kumpoza Zitto na ukatibu mkuu ili kumuokoa Mbowe.
Kibanda njoo ndugu yetu.
 
Mkuu Nchimbi mpaka hapo sijakwelewa unataka ueleze nini maana unajikanganya
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…