Moja ya kanuni muhimu sana ya Uandishi wa Habari/ journalism kama profession ni OBJECTIVITY; Katika muktadha huu, OBJECTIVITY ni pamoja na mhusika kuwa FAIR, DISINTERESTED, FACTUAL & NON-PARTISANSHIP/Neutrality (asiye egemea chama au itikadi fulani); Katika haya, Kibanda anafeli kwenye mengi kama sio yote;
Kwa mfano, katika maelezo yake, anatumia dhana ya UKWELI kuhalalisha anachokifanya, lakini anasahau kwamba kuna tofauti kubwa baina ya Jambo la Hakika (FACT) na Ukweli (TRUTH);
Jambo la hakika au Fact, kimantiki, haiwezi kukataliwa au kupingwa; Kwa mfano, nikisema kwamba MOTO UNAUNGUZA, haijalishi wewe ni bingwa au hodari au nguli kiasi gani katika reasoning skills, ukigusa moto UTAUNGUA; Hivyo, FACTS ni concrete realities na haziwezi badilishwa/badilika hata kaam una kipaji cha 'Reasoning' cha namna gani. Muhimu kwenye hili ni kwamba: Facts are not discovered, and they are not created, instead, Facts are simply acknowledged, na habari huishia hapo.
Tukija kwenye dhana ya UKWELI ambayo Kibanda ndio anaitumia kuhalalisha hoja yake ya msingi, ni muhimu atambue kwamba UKWELI ni kitu tofauti sana pengine ni kinyume kabisa na FACT; Kwa mfano, tofauti na FACT ambayo ina sifa ya kuwa acknowledged moja kwa moja na bila ya mjadala, Sifa kubwa ya Ukweli ni Mjadala, lakini muhimu zaidi ni kwamba UKWELI ni lazima Utengenezwe, au Ugundulike; Ukweli hauwi acknowledged kama ilivyo kwa FACT; Kwa mfano, nikisema kwamba MUNGU YUPO, na nikaja na reasoning to support msimamo wangu, wapo wataokubali kwamba ni KWELI MUNGU YUPO, na hii inageuka kuwa Reality lakini kwa wale wanaokubaliana na reasoning yangu; Lakini akija mtu mwingine na kusema kwamba MUNGU HAYUPO na akaja na reasoning to support hiyo position, wapo pia watakaokubaliana nae na hivyo kuwa reality kwa kundi hili; Kikubwa hapa ni kwamba kila upande utakuwa na arguments zake kuhusu reality kwa jinsi wanavyoona wao, lakini mwisho wa siku, iwapo reasoning ya upande mmoja (kwa mfano kwamba MUNGU YUPO), itaishinda ya upande wa pili, ni rahisi kwa upande husika kuhamia kwenye Reality mpya;
Tukirudi kwa Kibanda, yupo sahihi kwamba ana haki ya kusimamia anacho amini, lakini anajisahau kwamba kwa vile hapa he is dealing with truth na sio facts, hawezi kulazimisha wengine waamini anachoamini yeye, na mbaya zaidi ni kwamba anatumia muda mwingi na nguvu nyingi sana kufanya kitu SIO, yani kutetea haki yake kuamini anachokiamini na kwanini huo ndio ukweli, badala ya kutumia muda zaidi kuwa aminisha wanaoamini upande wa pili kwanini upande wake upo sahihi kwa kumtumia huyo huyo KINANA; Vinginevyo, ni muhimu atambue kwamba, kama yeye alivyokuwa na haki ya kuamini anachosimamia, hata wale wanaompinga wana haki ya kuamini wanachosimamia, kwani pande zote mbili zina TRUTHS wanazoamini kutokana na creation and development of certain concepts and constructs, experiences etc;
Mwisho, ni muhimu Kibanda atambue kwamba mjadala wake hauna moja ya sifa kubwa za uandishi wa habari kama taaluma - yani kuwa ‘FACTUAL' – na ndio maana anachojadili lazima kwanza kiwe discovered, created then kikubalike as Truth, na kitaishia hapo, kwani kamwe hakitafikia kiwango cha kuwa acknowledged as a ‘FACT'; vinginevyo ingekuwa ni FACT, toleo lake la wiki jana lingeishia pale pale kwa kuwa ACKNOWLEDGED bila ya majadiliano yoyote;
Vinginevyo, ategemee kukumbana na mgongano wa mawazo mpaka liamba na kwa vile amesha washa mjadala, kama hatobadilisha hoja yake iwe TRUTH na kukubali sio FACT, he is the one to loose;