Kibanda: Kinana ni Kimbunga

Kibanda: Kinana ni Kimbunga

hivi wewe mzee wa kudekeza ubongo undhani kuongea kwa stahili hii itabibadilisha?Hembu changamsha hiyo akili uniambie unanishutumu kwa lipi ktk ya niliyosema?

Nania kakuambia mimi ni tegemeo la chadema?Au tayari fikra zako zimependa hivyo.Umbea utakumaliza mzee wa kudekeza ubongo.

Mbona unenda mbali sana mzee wa puumba! Mwambie Dr Slaa ajiuzulu afuate mfano wa aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA David Patreaus. Au Waziri Silvio Berlusconi.
 
Ndugu Kibanda Absalom UKIIJUA KWELI NAYO KWELI ITAKUWEKA HURU!
 
Mbona unenda mbali sana mzee wa puumba! Mwambie Dr Slaa ajiuzulu afuate mfano wa aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA David Patreaus. Au Waziri Silvio Berlusconi.

Mbona upo random sana kiakili, probabbility ya wewe kuongea kitu kinachofuata consistently ni zero .Hata hitimisho la vitu unavivianzisha huwa hujui kuwa ni muhimu.Sishangai watu kama nyie ndio kizazi cha CCM , jamii ya dhaifu.Ndio maana hamna malengo ya muda mrefu.Halafu baadaye mnakuja lalamika kuwa wengine walipendelewa kumbe ni nyinyi tuu msio na mawazo yanayoweza kwenda mbali hata kwa second moja baada ya neno kukotoka mdomoni.Ndio maana hamkuona mbalia mlipokimbilia kuchoma makanisha ili uovu unaowaka mioyoyoni mwenu itoke haraka.

Sasa inahusika vitpi na habari uliyodandia ya wasomali?
 
Dah!,Tanzania viongozi wake wamepinda kweli.mafisadi(wahujumu uchumi)ndio imekuwa kimbilio la nchi?Nimesikia leo kkt usomaji wa magazeti kuwa askofu Mokiwa akimsifisia Kinana kwa kusema ni kiongozi alietukuka.
 
Mbona upo random sana kiakili, probabbility ya wewe kuongea kitu kinachofuata consistently ni zero .Hata hitimisho la vitu unavivianzisha huwa hujui kuwa ni muhimu.Sishangai watu kama nyie ndio kizazi cha CCM , jamii ya dhaifu.Ndio maana hamna malengo ya muda mrefu.Halafu baadaye mnakuja lalamika kuwa wengine walipendelewa kumbe ni nyinyi tuu msio na mawazo yanayoweza kwenda mbali hata kwa second moja baada ya neno kukotoka mdomoni.Ndio maana hamkuona mbalia mlipokimbilia kuchoma makanisha ili uovu unaowaka mioyoyoni mwenu itoke haraka.

Sasa inahusika vitpi na habari uliyodandia ya wasomali?

Mzee wa puumba umeishakimbilia mambo ya kuchoma makanisa...wewe kizazi ya Chadema ulivyokuwa na akili fupi unadhani Watanzania wote ni mateka wa Chadema. Tanzania haiwezi kutawaliwa na Sheikh wala Padri umenipata.
 
Ukweli ni kwamba tayari kachukuliwa na Rostam Aziz ambaye pamoja na kuiponda CCM bado anaisaidia. Keep your ears on the ground...before long you will confirm this
 
Mzee wa puumba umeishakimbilia mambo ya kuchoma makanisa...wewe kizazi ya Chadema ulivyokuwa na akili fupi unadhani Watanzania wote ni mateka wa Chadema. Tanzania haiwezi kutawaliwa na Sheikh wala Padri umenipata.

hata hujui tena unachoongea.Hembu soma posting 3 za juu halafu ujiulize kama uanchojibu ni sahihi.
 
Niliwahi kushuhudia mtu mmoja tu aliyechaguliwa kuwa mbunge bila kutumia pesa hata senti moja, kwanza hakuwa nazo aliwekwa nafasi hiyo na nguvu ya wananchi huyu alikuwa Ngugu Pharece Kashemeza Kabuye Biharamulo(sasa hivi marehemu) wengine awe wa CDM, CCM, TLP NCCR nk walitoa rushwa 2010 mbona mnaisakama CCM peke yake CCM iliwazidi kete tu lakini ninyi wote wadhambi. mfumo ndo unaleta shida bila kurekebisha mfumo wa tume ya uchaguzi mambo yatakuwa yaleyale 2015
 
Mhariri Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda baada ya wiki iliyopita kuibuka na Makala isemayo NAMUOGOPA KINANA iliyokuwa ikimwagia kila aina ya Sifa, leo hii ameibuka na makala nyingine ya kumsifu Katibu mkuu huyo wa CCM huku akiponda mashabiki na wanachama wa CHADEMA kwamba ni walevi wa Fikra na anatabiri Kimbunga cha Kinana kwa CHADEMA kitakuwa 2015....Endelea.........

YAKO mambo ya msingi katika maisha ya kitaaluma katika fani zote za kielimu ambayo mtu yeyote anayetambua na kujali vyema wajibu wake anapaswa kuyasimamia na kuyalinda hata kama atafanya hivyo kwa gharama ya kupoteza maisha, kuchukiwa, kudharauliwa au kupuuzwa.

Moja ya mambo ya namna hiyo ni miiko ya kitaaluma ambayo aghalab huongoza na kujenga misingi ya uwepo na kustawi kwa kila fani iwe ni sheria, elimu, uaskari, uhandisi na hata ukachero.

Uandishi wa habari ni moja ya taaluma ambazo zina miiko na maadili yake. Zaidi ya hayo uandishi wa habari na waandishi wa habari wanaishi kwa kufuata na kuzingatia miongozo yao ya kikazi na kitaaluma.

‘Ukweli’ ni moja ya misingi mikuu ya uandishi wa habari. Huu unaweza ukawa msingi mama katika taaluma hii adhimu. Ni kwa kuzingatia hilo ndiyo maana uandishi wa habari unatajwa na magwiji wa taaluma hii kuwa ni ‘noble profession’.

Naandika maneno haya huku nikitambua kwa dhati kwamba, mara kadhaa wanahabari wa hapa nchini na kwingineko duniani tumekuwa mstari wa mbele katika kukiuka msingi na muongozo huo muhimu kitaaluma kwa kujua au kutojua, kwa kukusudia ama kwa bahati mbaya.

Pamoja na mapungufu hayo ya kibinadamu katika taaluma hii ambayo siku zote nitabakia kuwa mwanafunzi wake, uandishi wa habari unaendelea na utaendelea kubakia kuwa mhimili wa nne wa dola baada ya serikali, Bunge na Mahakama.

Iwapo hivyo ndivyo, uandishi wa habari ni taaluma ambayo inao wajibu wa kusimama juu ya taaluma zote nyingine ambazo aghalab kwa nafasi zao hakuna hata moja ambayo imepata kuchukua taswira ya mhimili kama ilivyo kwa uandishi wa habari.

Kwa sababu hiyo basi, kama ilivyo kwa mihimili mingine ya dola, taaluma hii inao wajibu wa kukubali changamoto zinazoelekezwa kwake na wakati mwingine kuchukua maamuzi ambayo yanaipa mamlaka na taswira halisi ya kuonekana kuwa ni mhimili unaojitegemea kifikra, kimatendo na hata kimaadili.

Nimelazimika kuyasema yote haya katika utangulizi wa makala yangu ya leo kutokana na kile ambacho kilitokea wiki iliyopita baada ya safu hii kuwa na makala iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho: “Namuogopa Abdulrahman Kinana”.

Makala ile ilibeba ujumbe rahisi kabisa. Kwanza mbali ya kueleza kwa sehemu tu kuhusu wasifu wa Kinana kwa mtazamo wa mwandishi wa safu hii ambaye ni mimi mwenyewe, ilieleza kwa muhtasari tu sababu ambazo zilimfanya Rais Jakaya Kikwete hatimaye akubali yaishe kwa kumfanya mwanasiasa huyo abebeshwe jukumu la kuwa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kama hiyo haitoshi, makala ile ilieleza kwa maneno yaliyo wazi kabisa kwamba, CCM ilikuwa ikichungulia kaburi na kimsingi mwenendo wa mambo katika kipindi cha miaka michache tu iliyopita hadi sasa ilikuwa ikichukua mwelekeo wa wazi wa kupoteza madaraka ya dola.

Ni kwa bahati mbaya sana kwamba, mashabiki wa vyama vya upinzani ambao siku zote wamekuwa hodari kushangilia hoja zetu za kuikosoa serikali au kuisuta CCM na viongozi wake kwa kuwaangusha Watanzania katika maeneo kadha wa kadha walipatwa na hasira kali waliposoma makala ile na kuona ikiwa na harufu ya kumsifu au kueleza uwezo wa kimikakati, kiutawala, kisiasa na kiintelijensia aliokuwa nao Kinana na pengine safu ya uongozi mpya wa chama hicho tawala iliyoundwa wiki mbili zilizopita.

Kwa sababu tu ya kulemewa kwao na ulevi wa chuki walizoijengea CCM na viongozi wake pasipo hata kuangalia muktadha wa makala ile, wadakuzi hao wa mambo kupitia katika mitandao ya intaneti, majukwaa ya jamii, ujumbe wa maandishi na kwenye simu yangu ya kiganjani na hata kwa njia ya ana kwa ana wakanisuta na kunitukana kila aina ya matusi ili kukidhi matakwa yao.

Lile kosa la wanasiasa na wapambe wao kukosa ustahimilivu ambalo tumekuwa tukiwahusisha nalo watawala, likachukua sura na mwelekeo tofauti.

Siri zikafichuka kwamba ndani ya mioyo ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani, wafuasi na mashabiki wao kulikuwa na hulka za hatari za udikteta ambazo ama zinalingana na zile walizonazo baadhi ya wana CCM na viongozi kadha wa kadha wa kiserikali.

Niseme wazi na kwa kujiamini kabisa kwamba, sikutishwa wala kubabaishwa na matukio hayo ambayo kwangu hayakuwa mageni hata kidogo kwani yalifanya kile ambacho nimekuwa nikikabiliana nacho tangu mwaka 1993 wakati nilipoanza kushiriki kikamilifu kuandika makala katika magazeti mbalimbali nchini na wakati mwingine kutoa maoni na mawazo yangu kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa.

Haraka haraka hoja za kishabiki zilizokosa weledi ambazo zilikuwa zikivurumishwa na manazi hao wa kisiasa zilinikumbusha ujasiri niliokuwa nao mwaka 1995 wakati niliposimama imara kupinga mhemko wa kitaifa wa “Homa ya Augustine Mrema” ambayo ililitikisa taifa kwa kiwango cha kumchanganya akili Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Nilikuwa na ujasiri aliokuwa nao Jenerali Ulimwengu wa kumpinga Mrema katika maandishi na hata katika majukwaa ya mijadala.

Bado nakumbuka vyema namna nilivyosafiri kwa daladala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nilikokuwa nikisoma hadi Kariakoo zilizokuwa ofisi za NCCR Mageuzi na nikapata fursa ya kuwafikia Mabere Marando na Ndimara Tegambwage nikiwaomba watafakari upya uamuzi wao wa kumpa Mrema dhamana ya kuongoza harakati ghali za mageuzi katika taifa hili.

Makala nilizoandika katika magazeti ya Rai, Mtanzania, Wakati Ni Huu, Nipashe na kwingineko katika kipindi hicho cha 1995 na 1996 ambazo aghalab zilikuwa zikiwaasa Watanzania kupima mambo kwa kina badala ya kutukuza na kuendekeza ushabiki wa kisiasa ni ushahidi wa wazi wa kile ambacho nilikuwa nikikisimamia na nimeendelea kukisimamia siku zote.

Haikupita hata miaka miwili kabla ukweli wa kile nilichokuwa nikikizungumza na kukitetea kwa njia ya maandishi kuthibitika.

Mrema alifanya kile nilichokiona mapema, akawaangusha aliowaongoza na kuwaporomosha wale waliofikia hatua ya kumuabudu kwa kiwango cha kumuona mkombozi wao wa kisiasa.

Kama ilivyokuwa kwa Mrema mwaka huo huo wa 1995, nilikuwa miongoni mwa wanahabari ambao tulimpinga kwa hoja Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika harakati zake za kulazimisha aliyekuwa mgombea wake, Benjamin Mkapa, ateuliwe na kuwa mgombea wa urais wa CCM.

Katika hili, sikukubaliana na kile ambacho Jenerali Ulimwengu na wenzake walikitetea. Ingawa nilikuwa mpinzani mkubwa wa Mrema, sikufurahishwa hata kidogo na uamuzi wa Baba wa Taifa kupandikiza hulka za kidikteta katika kuchakachua mchakato wa urais kupitia katika tanuri la chama hicho tawala.

Kilichotokea miaka 10 baada ya Mkapa kustaafu urais mwaka 2005 ni ushahidi wa wazi wa kile ambacho baadhi yetu, japo hatuna majina makubwa tulikiona mapema.Rais huyo pamoja na kuonekana kwamba alikijengea heshima kiti cha urais na kuinunua harufu ya maendeleo ya kiuchumi, alifisha hata ndoto za ‘mentor’ wake Mwalimu Nyerere. Hili linahitaji mjadala unaojitegemea.

Sikuishia hapo, mwaka 2005 wakati taifa na fani nzima ya habari ikiimba wimbo wa Kikwete, Kikwete Kikwete katika misingi ya ushabiki unaofanana na ule unaotokea leo, nilikuwa miongoni mwa waandishi wachache ambao tulikataa kuimba wimbo huo huku tukitoa tahadhari za waziwazi kuhusu hatari ambayo ilikuwa ikilinyemelea taifa.

Ingawa wakati huo nilikuwa Mhariri wa gazeti la Mwananchi Jumapili ambalo mmoja wa wakurugenzi wake alikuwa Rostam Aziz aliyekuwa katikati ya kitovu cha kampeni za Kikwete, nilikataa kuwa bendera fuata upepo na nikaandika mada kadha wa kadha kuhoji kuhusu uwezo wa mwanasiasa huyo kupewa dhamana ya kuongoza nchi.

Ushahidi wa kile nilichoandika kuhusu hilo uko wazi kabisa. Nilitenda na kutoa msimamo tofauti kabisa na ule waliokuwa nao baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wa zama hizo kuhusu nafasi ya Kikwete katika kuliongoza taifa hili.

Hata yeye mwenyewe alipotangaza uamuzi wa kugombea urais kule Chalinze nilikuwa miongoni mwa wahariri na wanahabari ambao tulikwenda na kumuuliza maswali magumu kuhusu kugombea kwake.

Alipoteuliwa na chama chake kuwa mgombea kama ilivyotarajiwa na wengi, nilitafuta fursa na nikafanya naye mahojiano nyumbani kwake Dodoma nikiwa nimeongozana na mwanahabari mwenzangu, Nyaronyo Kicheere, aliyekuwa Mhariri wa Habari wa gazeti dada la The Citizen on Sunday.

Niliendelea na msimamo ule juu ya Kikwete kabla na baada ya kuteuliwa kwake kuwa mgombea urais. Waandishi na wahariri waliokuwa pale ni mashahidi wazuri kwamba, msimamo wangu huo ulipata kusababisha Rostam afikie hatua ya kueleza waziwazi kukerwa nao.

Mara kadhaa aliniita nyumbani kwake akijaribu kunishawishi na kuniaminisha kwamba Kikwete alikuwa ni mwanasiasa hodari na anayeweza kuliongoza taifa hili pengine kuliko mwingine yeyote.

Kilichotokea baada ya hapo kila mtu anakijua, Kikwete alishinda kwa kishindo na baadhi yetu ambao tulionekana kuwa vimbelembele kuhoji uwezo wake tukasutwa kweli kweli kwa kiwango cha baadhi ya wanahabari wenzetu kutuona wendawazimu.

Kwa sababu ya kuendekeza hulka za kishabiki, wanahabari tulishindwa kumuandaa Kikwete kuwa rais bora, tulimnyima fursa ya kujipanga kifikra na kifalsafa na tukaiacha ajenda ya urais iandaliwe kimkakati na kiintelijensia zaidi. Hiki tunachokiona leo ni matokeo ya kuendekeza ushabiki wa namna hiyo.

Ni jambo la bahati mbaya kwamba kile kilichotokea mwaka 1995 na baadaye mwaka 2005 bado kinaonekana kutofundisha Watanzania. Hulka za kinazi na kishabiki katika masuala ya msingi bado zinaendelea kutafuna vichwa vyetu.

Taifa zima linaimba wimbo mmoja tu, Slaa, Slaa, Slaa. Halitaki kusikia lolote. Ukimgusa Dk. Slaa tena kwa hoja za kumtahadharisha, kumuonya au hata kwa minajiri ya kumfanya ajiandae kukabiliana na kimbunga kama hiki cha Kinana, mashabiki wake wanalipuka kwa jazba na kwa hamaki kubwa.

Ukithubutu kuikosoa CHADEMA au kumgusa yeyote miongoni mwa viongozi wake kama nilivyofanya miaka mitatu au minne iliyopita wakati nilipopinga uamuzi wa Zitto Kabwe kugombea uenyekiti wa taifa wa chama hicho kwa sababu muda wake ulikuwa bado, idadi ya matusi utakayovurumishiwa kama ni mtu ambaye una moyo mwepesi unaweza ukaacha kuandika.

Hivi ndivyo ilivyokuwa wiki iliyopita wakati nilipowaonya wapinzani kukaa chonjo na Kinana kwani kimbunga ambacho alikuwa akielekeza kukipuliza kuelekea upande wa kambi ya upinzani kinaweza kusababisha upepo unaovuma sasa kubadili njia.

Sitaki kujifanya mimi ni nabii wa siasa za Tanzania. Hata hivyo bado naendelea kuamini na kusisitiza kwamba, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana si mtu mwepesi, si mwanasiasa wa kumbeza wala kumpuuza.

Kama CHADEMA na mashabiki wanataka kupima kina cha maji kwa sababu tu ya ulevi wa fikra, basi wanao uhuru wa kufanya hivyo. Tusubiri fainali 2015. Huko ndiko tuendako.

Alichosema ni kweli tupu, na hili ni gazeti la CDM lazima maji yamewafika shingoni sasa wameamua bora hadhara ielewe. Hongera Kibanda kwa kuwa mkweli historia itakuenzi daima
 
Alifanikishaje? Aliratibu vipi na kupanga ushindi? Kupanga ushindi? Aliwadanganya wapiga kura? Honestly, do you really think that Mr. Kinana ana ushawishi kiasi hicho kwa Watanzania? Kwamba ushindi wa CCM unamtegemea yeye? Au ninashindwa kukuelewa. Labda unamaanisha yeye ni mtaalamu wa wizi wa kura?

Point ni Kwamba CCM wanaamini kama asingekuwa Kinana kusimamia Kampeni za Kikwete na kuratibu ushetani wa wizi wa kura bila hofu wala uoga wa namna yoyote ile CCM ingekuwa njia ya KANU hivi sasa sababu uchakachuaji wa kawaida usingemuwezesha mtu yoyote kutangaza kwamba Jakaya kashinda sababu alishindwa vibaya sana.

Pia hili ni tangazo rasmi kwamba CCM wanajiandaa na uchaguzi wa 2015, swali la msingi ni Je wametekeleza kwa kiwango gani ahadi zao za 2010.

At least sasa tumepata mtu wa kumuuliza kuhusu ahadi zao za Mwanzo sababu JK aliishaachana na sisi siku anaapishwa for the second term.
 
Kweli hii nchi inaendeshwa kwa matukio,UVUAJI GWANDA UMEISHIA WAPI??????
 
Alichosema ni kweli tupu, na hili ni gazeti la CDM lazima maji yamewafika shingoni sasa wameamua bora hadhara ielewe. Hongera Kibanda kwa kuwa mkweli historia itakuenzi daima
Ni kweli kama mnavyomuenzi Tambwe Hiza sasa hivi.
 
hiyo misimamo ya waandishi kama Kibanda isiyokuwa na tija kwa maendeleo ya watanzania haitusaidii.bora mngekuwa mnaandika na mnashauri serikali na watendaji wake juu ya UCHUMI na MAENDELEO..Kibanda umekuwa ukipata negative impact hizo kwa sababu tangu uanze kukosoa hujasikilizwa,yaani tangu enzi za mkapa,kikwete na sasa kinana cjui na yupi.namshauri aanzishe chama chake awe anasema vizuri.huwezi ukamponda au kumpa angalizo kikwete wakati unaandikia gazeti la uhuru.hata uwe na uzalendo,ujasiri na umakini wa hali ya juuu kiasi gani manazi hawatakuelewa na misimamo yako
 
hata hujui tena unachoongea.Hembu soma posting 3 za juu halafu ujiulize kama uanchojibu ni sahihi.

Hata sikuelewi anachoandika unaandika kama vile mtoto wa Kindergarten.
 
Mtu kama huyu eti ndio tegemeo la Chadema...ukitaka kujua upumbavu wa mtu upo kiwango gani msome mabandiko yake...wewe jamii ambayo unaiheshimu ni Wachaga tu. Mtu makini hawezi kuandika maneno haya.

wewe siyo mtanzania ... wewe ni msomali
 
Hata sikuelewi anachoandika unaandika kama vile mtoto wa Kindergarten.

Kwani huwa unaelewa kitu siku yoyote?unajua Ritz kuna kipindi unachekesha sana.Usidhani watu kukuzoea na ku ignore your ugly side usidhani kuwa kunaondoa ukweli kuwa ubongo wako haujatumika kabisa.Yaani kwa jinsi ulivyo kituko hata kindergarten kids wanaweza kuon ajinsi ulivyo funny.
 
Mhariri Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda baada ya wiki iliyopita kuibuka na Makala isemayo NAMUOGOPA KINANA iliyokuwa ikimwagia kila aina ya Sifa, leo hii ameibuka na makala nyingine ya kumsifu Katibu mkuu huyo wa CCM huku akiponda mashabiki na wanachama wa CHADEMA kwamba ni walevi wa Fikra na anatabiri Kimbunga cha Kinana kwa CHADEMA kitakuwa 2015....Endelea.........

YAKO mambo ya msingi katika maisha ya kitaaluma katika fani zote za kielimu ambayo mtu yeyote anayetambua na kujali vyema wajibu wake anapaswa kuyasimamia na kuyalinda hata kama atafanya hivyo kwa gharama ya kupoteza maisha, kuchukiwa, kudharauliwa au kupuuzwa.

Moja ya mambo ya namna hiyo ni miiko ya kitaaluma ambayo aghalab huongoza na kujenga misingi ya uwepo na kustawi kwa kila fani iwe ni sheria, elimu, uaskari, uhandisi na hata ukachero.

Uandishi wa habari ni moja ya taaluma ambazo zina miiko na maadili yake. Zaidi ya hayo uandishi wa habari na waandishi wa habari wanaishi kwa kufuata na kuzingatia miongozo yao ya kikazi na kitaaluma.

‘Ukweli' ni moja ya misingi mikuu ya uandishi wa habari. Huu unaweza ukawa msingi mama katika taaluma hii adhimu. Ni kwa kuzingatia hilo ndiyo maana uandishi wa habari unatajwa na magwiji wa taaluma hii kuwa ni ‘noble profession'.

Naandika maneno haya huku nikitambua kwa dhati kwamba, mara kadhaa wanahabari wa hapa nchini na kwingineko duniani tumekuwa mstari wa mbele katika kukiuka msingi na muongozo huo muhimu kitaaluma kwa kujua au kutojua, kwa kukusudia ama kwa bahati mbaya.

Pamoja na mapungufu hayo ya kibinadamu katika taaluma hii ambayo siku zote nitabakia kuwa mwanafunzi wake, uandishi wa habari unaendelea na utaendelea kubakia kuwa mhimili wa nne wa dola baada ya serikali, Bunge na Mahakama.

Iwapo hivyo ndivyo, uandishi wa habari ni taaluma ambayo inao wajibu wa kusimama juu ya taaluma zote nyingine ambazo aghalab kwa nafasi zao hakuna hata moja ambayo imepata kuchukua taswira ya mhimili kama ilivyo kwa uandishi wa habari.

Kwa sababu hiyo basi, kama ilivyo kwa mihimili mingine ya dola, taaluma hii inao wajibu wa kukubali changamoto zinazoelekezwa kwake na wakati mwingine kuchukua maamuzi ambayo yanaipa mamlaka na taswira halisi ya kuonekana kuwa ni mhimili unaojitegemea kifikra, kimatendo na hata kimaadili.

Nimelazimika kuyasema yote haya katika utangulizi wa makala yangu ya leo kutokana na kile ambacho kilitokea wiki iliyopita baada ya safu hii kuwa na makala iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho: "Namuogopa Abdulrahman Kinana".

Makala ile ilibeba ujumbe rahisi kabisa. Kwanza mbali ya kueleza kwa sehemu tu kuhusu wasifu wa Kinana kwa mtazamo wa mwandishi wa safu hii ambaye ni mimi mwenyewe, ilieleza kwa muhtasari tu sababu ambazo zilimfanya Rais Jakaya Kikwete hatimaye akubali yaishe kwa kumfanya mwanasiasa huyo abebeshwe jukumu la kuwa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kama hiyo haitoshi, makala ile ilieleza kwa maneno yaliyo wazi kabisa kwamba, CCM ilikuwa ikichungulia kaburi na kimsingi mwenendo wa mambo katika kipindi cha miaka michache tu iliyopita hadi sasa ilikuwa ikichukua mwelekeo wa wazi wa kupoteza madaraka ya dola.

Ni kwa bahati mbaya sana kwamba, mashabiki wa vyama vya upinzani ambao siku zote wamekuwa hodari kushangilia hoja zetu za kuikosoa serikali au kuisuta CCM na viongozi wake kwa kuwaangusha Watanzania katika maeneo kadha wa kadha walipatwa na hasira kali waliposoma makala ile na kuona ikiwa na harufu ya kumsifu au kueleza uwezo wa kimikakati, kiutawala, kisiasa na kiintelijensia aliokuwa nao Kinana na pengine safu ya uongozi mpya wa chama hicho tawala iliyoundwa wiki mbili zilizopita.

Kwa sababu tu ya kulemewa kwao na ulevi wa chuki walizoijengea CCM na viongozi wake pasipo hata kuangalia muktadha wa makala ile, wadakuzi hao wa mambo kupitia katika mitandao ya intaneti, majukwaa ya jamii, ujumbe wa maandishi na kwenye simu yangu ya kiganjani na hata kwa njia ya ana kwa ana wakanisuta na kunitukana kila aina ya matusi ili kukidhi matakwa yao.

Lile kosa la wanasiasa na wapambe wao kukosa ustahimilivu ambalo tumekuwa tukiwahusisha nalo watawala, likachukua sura na mwelekeo tofauti.

Siri zikafichuka kwamba ndani ya mioyo ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani, wafuasi na mashabiki wao kulikuwa na hulka za hatari za udikteta ambazo ama zinalingana na zile walizonazo baadhi ya wana CCM na viongozi kadha wa kadha wa kiserikali.

Niseme wazi na kwa kujiamini kabisa kwamba, sikutishwa wala kubabaishwa na matukio hayo ambayo kwangu hayakuwa mageni hata kidogo kwani yalifanya kile ambacho nimekuwa nikikabiliana nacho tangu mwaka 1993 wakati nilipoanza kushiriki kikamilifu kuandika makala katika magazeti mbalimbali nchini na wakati mwingine kutoa maoni na mawazo yangu kwa viongozi mbalimbali wa kisiasa.

Haraka haraka hoja za kishabiki zilizokosa weledi ambazo zilikuwa zikivurumishwa na manazi hao wa kisiasa zilinikumbusha ujasiri niliokuwa nao mwaka 1995 wakati niliposimama imara kupinga mhemko wa kitaifa wa "Homa ya Augustine Mrema" ambayo ililitikisa taifa kwa kiwango cha kumchanganya akili Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Nilikuwa na ujasiri aliokuwa nao Jenerali Ulimwengu wa kumpinga Mrema katika maandishi na hata katika majukwaa ya mijadala.

Bado nakumbuka vyema namna nilivyosafiri kwa daladala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nilikokuwa nikisoma hadi Kariakoo zilizokuwa ofisi za NCCR Mageuzi na nikapata fursa ya kuwafikia Mabere Marando na Ndimara Tegambwage nikiwaomba watafakari upya uamuzi wao wa kumpa Mrema dhamana ya kuongoza harakati ghali za mageuzi katika taifa hili.

Makala nilizoandika katika magazeti ya Rai, Mtanzania, Wakati Ni Huu, Nipashe na kwingineko katika kipindi hicho cha 1995 na 1996 ambazo aghalab zilikuwa zikiwaasa Watanzania kupima mambo kwa kina badala ya kutukuza na kuendekeza ushabiki wa kisiasa ni ushahidi wa wazi wa kile ambacho nilikuwa nikikisimamia na nimeendelea kukisimamia siku zote.

Haikupita hata miaka miwili kabla ukweli wa kile nilichokuwa nikikizungumza na kukitetea kwa njia ya maandishi kuthibitika.

Mrema alifanya kile nilichokiona mapema, akawaangusha aliowaongoza na kuwaporomosha wale waliofikia hatua ya kumuabudu kwa kiwango cha kumuona mkombozi wao wa kisiasa.

Kama ilivyokuwa kwa Mrema mwaka huo huo wa 1995, nilikuwa miongoni mwa wanahabari ambao tulimpinga kwa hoja Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika harakati zake za kulazimisha aliyekuwa mgombea wake, Benjamin Mkapa, ateuliwe na kuwa mgombea wa urais wa CCM.

Katika hili, sikukubaliana na kile ambacho Jenerali Ulimwengu na wenzake walikitetea. Ingawa nilikuwa mpinzani mkubwa wa Mrema, sikufurahishwa hata kidogo na uamuzi wa Baba wa Taifa kupandikiza hulka za kidikteta katika kuchakachua mchakato wa urais kupitia katika tanuri la chama hicho tawala.

Kilichotokea miaka 10 baada ya Mkapa kustaafu urais mwaka 2005 ni ushahidi wa wazi wa kile ambacho baadhi yetu, japo hatuna majina makubwa tulikiona mapema.Rais huyo pamoja na kuonekana kwamba alikijengea heshima kiti cha urais na kuinunua harufu ya maendeleo ya kiuchumi, alifisha hata ndoto za ‘mentor' wake Mwalimu Nyerere. Hili linahitaji mjadala unaojitegemea.

Sikuishia hapo, mwaka 2005 wakati taifa na fani nzima ya habari ikiimba wimbo wa Kikwete, Kikwete Kikwete katika misingi ya ushabiki unaofanana na ule unaotokea leo, nilikuwa miongoni mwa waandishi wachache ambao tulikataa kuimba wimbo huo huku tukitoa tahadhari za waziwazi kuhusu hatari ambayo ilikuwa ikilinyemelea taifa.

Ingawa wakati huo nilikuwa Mhariri wa gazeti la Mwananchi Jumapili ambalo mmoja wa wakurugenzi wake alikuwa Rostam Aziz aliyekuwa katikati ya kitovu cha kampeni za Kikwete, nilikataa kuwa bendera fuata upepo na nikaandika mada kadha wa kadha kuhoji kuhusu uwezo wa mwanasiasa huyo kupewa dhamana ya kuongoza nchi.

Ushahidi wa kile nilichoandika kuhusu hilo uko wazi kabisa. Nilitenda na kutoa msimamo tofauti kabisa na ule waliokuwa nao baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wa zama hizo kuhusu nafasi ya Kikwete katika kuliongoza taifa hili.

Hata yeye mwenyewe alipotangaza uamuzi wa kugombea urais kule Chalinze nilikuwa miongoni mwa wahariri na wanahabari ambao tulikwenda na kumuuliza maswali magumu kuhusu kugombea kwake.

Alipoteuliwa na chama chake kuwa mgombea kama ilivyotarajiwa na wengi, nilitafuta fursa na nikafanya naye mahojiano nyumbani kwake Dodoma nikiwa nimeongozana na mwanahabari mwenzangu, Nyaronyo Kicheere, aliyekuwa Mhariri wa Habari wa gazeti dada la The Citizen on Sunday.

Niliendelea na msimamo ule juu ya Kikwete kabla na baada ya kuteuliwa kwake kuwa mgombea urais. Waandishi na wahariri waliokuwa pale ni mashahidi wazuri kwamba, msimamo wangu huo ulipata kusababisha Rostam afikie hatua ya kueleza waziwazi kukerwa nao.

Mara kadhaa aliniita nyumbani kwake akijaribu kunishawishi na kuniaminisha kwamba Kikwete alikuwa ni mwanasiasa hodari na anayeweza kuliongoza taifa hili pengine kuliko mwingine yeyote.

Kilichotokea baada ya hapo kila mtu anakijua, Kikwete alishinda kwa kishindo na baadhi yetu ambao tulionekana kuwa vimbelembele kuhoji uwezo wake tukasutwa kweli kweli kwa kiwango cha baadhi ya wanahabari wenzetu kutuona wendawazimu.

Kwa sababu ya kuendekeza hulka za kishabiki, wanahabari tulishindwa kumuandaa Kikwete kuwa rais bora, tulimnyima fursa ya kujipanga kifikra na kifalsafa na tukaiacha ajenda ya urais iandaliwe kimkakati na kiintelijensia zaidi. Hiki tunachokiona leo ni matokeo ya kuendekeza ushabiki wa namna hiyo.

Ni jambo la bahati mbaya kwamba kile kilichotokea mwaka 1995 na baadaye mwaka 2005 bado kinaonekana kutofundisha Watanzania. Hulka za kinazi na kishabiki katika masuala ya msingi bado zinaendelea kutafuna vichwa vyetu.

Taifa zima linaimba wimbo mmoja tu, Slaa, Slaa, Slaa. Halitaki kusikia lolote. Ukimgusa Dk. Slaa tena kwa hoja za kumtahadharisha, kumuonya au hata kwa minajiri ya kumfanya ajiandae kukabiliana na kimbunga kama hiki cha Kinana, mashabiki wake wanalipuka kwa jazba na kwa hamaki kubwa.

Ukithubutu kuikosoa CHADEMA au kumgusa yeyote miongoni mwa viongozi wake kama nilivyofanya miaka mitatu au minne iliyopita wakati nilipopinga uamuzi wa Zitto Kabwe kugombea uenyekiti wa taifa wa chama hicho kwa sababu muda wake ulikuwa bado, idadi ya matusi utakayovurumishiwa kama ni mtu ambaye una moyo mwepesi unaweza ukaacha kuandika.

Hivi ndivyo ilivyokuwa wiki iliyopita wakati nilipowaonya wapinzani kukaa chonjo na Kinana kwani kimbunga ambacho alikuwa akielekeza kukipuliza kuelekea upande wa kambi ya upinzani kinaweza kusababisha upepo unaovuma sasa kubadili njia.

Sitaki kujifanya mimi ni nabii wa siasa za Tanzania. Hata hivyo bado naendelea kuamini na kusisitiza kwamba, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana si mtu mwepesi, si mwanasiasa wa kumbeza wala kumpuuza.

Kama CHADEMA na mashabiki wanataka kupima kina cha maji kwa sababu tu ya ulevi wa fikra, basi wanao uhuru wa kufanya hivyo. Tusubiri fainali 2015. Huko ndiko tuendako.

Its quite an interesting article.Sikuweza changia kwa nilikuwa na thread yangu iliyopotea baada ya mods kuunganisha kwa style iliyofanya nishindwe jua nachangia nini na kilianzia wapi.(Hapa huwa nalia sana na mods kwa kukimbilia unganisha threads wakati haziendani kihivyo ingawa title inaweza kuwa inakaribiana ila goals na approaches ni tofauti sana ukiachilia )

Huyu mwandishi kaanza kuji boast kidogo huku akiacha masalia ya kujisifia ktk utumwa kuwa alikuwa mwajiriwa wa Rostam Aziz.Hiyo pekee ni shida kubwa ya aina yake.Wakati hajatuambia kama Rostam alipochukia yeye alifuat anjia gani, tayari anaonekana kuwa jinamizi linamfuata na kumewekea "guilty consciousness".Anathibitisha kwa kusema kuwa aliposhinda Kikwete sijui kwa kishindo basi akapata akaumbuliwa na kupata aibu kubwa na kuonekana kama mwendawazimu.Naona kweli nimwite mwendawazimu na niendelee mwona kuw ani mwandishi tuu kwa vile anaaccess na media na pia na basic skills za kupangilia maneno kama alivyosoma shule.Huyu mwandishi kwanza ni mtu wa mashaka, pili hajui mambo ya msingi kabisa ktk issues anazoandika au kushabikia.Sioni kwanini anashindwa andika siasa kwa usahihi, ikiwa hatoweza mahali pengine popote zaidi ya siasa na matukio ya kurecord kama unavyoona.Hatoweza andika mambo ya kiuchumi na sayansi kwa kiwango cha kumweka mtu makini ktk hiyo makala.Hapa ndipo napata picture kwa nini magazeti ya Tanzania nia ya hovyo sana.Mhariri anajiona laikosea kwa vile mgombea urais aliyempinga alishinda na si alipokuwa rais Rais kuonyesha uwezo wa kuongoza?Its like Kilaini Kushindwa simamia tamko la maaskofu kuwa Kikwete ni Chaguao la Mungu kwa vile wanaona madudu yake makubwa.

Kikwete atabaki chaguo la Mungu kwa vile Kwanza Mungu ndiye anayeruhusu watu kupata kiongozi , na Pia Kikwete anavyokwenda ni wazi anakwenda angusha CCM, kitu ambacho ndicho watu wamakuwa wakiomba kwa miaka mingi huku wakitumia maneno kama ukombozi.

Mwandishi wa kashindwa elewa kuwa Dr. Slaa anahitaji Lindwa si toka kwa honest critics ila kwa mamluki na hila nyingine za CCM.Hii ni crucial element kwa ukombozi.Mwandishi huyu duni kasahau kuwa uandishi wake na wenzake usio responsible ndio ulipelekea Mrema kujikuta kuwa anayo option ya kuwauza watu bila kuwa na shinikizo toka kwa walio nyuma yake.Mwandishi hajui kuwa wanachama wanahitajia mweka mwanasiasa ktk mazingira ya kujifikiri amara mbili kama ni worth it kubadili njia kwa watu waliojitolea mengi ili wafike mwisho wa barabara.Ni aina ya check anad balance laiyokosa Mrema kwa vile hakuwa na waandishi wenye upeo wa kushape watu in a positive ways wakati waki keep references zao ktk usitawi na ulinzi wa taifa.

Mwandishi kaandika mengi huku akiacha gap ya kuandika makala nyingi zaidi kama laivyoacha kwa habari ya Mkapa.Sijui alidhani kuwa uzoefu wake na pengine nafasi alizowahi pata zinamfanya automatically kuwa mtu makini na mwenye uelewa mkubwa.Sijui atajisikiaje Kinana naye akitoka kama makamba ktk zoezi la liliozoeleka ktk CCM (kubadili betri zinazochagiwa kwa kuanikwa juani).Mwandishi kaanadika kama vile hajui ushindi wa CCM hauna tena maana ktk kuwakilisha mitazamo ya wananchi na hivyo si kipimo cha kukubalika au ufanishi tena.CCM wanatumia kila machinery na dirt games kujishikilia hapo.

Nahofia waandishi kama hawa, ni waandishi wanaofanya watu wa mataifa mengine kutuona kama genetically tumebeba madhaifu haya, wakati wengine ktk majirani zetu wakituona tuu kuwa wajinga wa kawaida.

Hizi ni nafasi adimu kwa watanzania kuwa to ktk public watu wote waliokaa muda mrefu ktk jamii zetu huku wakiwa useless and damaging. Wawe ni wasomi wenye PHDs, wawe ni waandishi na wahariri wa vyombo vikubwa, wawe wanasiasa na wengine maarufu na walioshika nyadhifa ,halafu wakajidanganya kuwa wana uzoefu na heshima isiyoguswa na jamii, na kila waongeacho au wafikiricho ni sahihi.Nadhani CDM ni chama makini kwa hiyo business, Lowasa alionda nyumbani kwakwe kwa Pili Arumeru, mkapa, wasira, na wengine wameshainia ktk hayo machinjio, sasa ni Kinana na wandishi duni kama haw awneue akili mgando huku wakitaka ingiza kalamu zao ktk duni ampya mabayo kuandika si lazima tena kujaza makaratasi, kuonyesha chenti na lobbying nyingine ili uweze andika habari, now people tween, people step in forums like JF.Soon wakizidi tuboa Tanzania itakuwa sehemu ya kwanza ondoa mainstrem papers, na kubakiwa na magazeti kama ya shigongo kwa ajili ya wanafunzi na mabinti wa nyumbani, na akina dada wa saluni.Siku nyingi tuu zaidi ya mwanahalisi sijapata gazeti la kusoma 15mins, yamejaa junks, hawawezi andika zaidi ya kureport kitu kama kilivyo (ten amara nyingine wanandika chini ya walichoona au tofauti).Ktk sehemu ya kufanya analysis wanaonyesha wasiwasi wao, ushsbiki wao, kutojua kwao na mengine ya kipuuzi.
 
Kibanda Absalom again. come on guys give me a break bora nihame jukwaa kuliko kumfuatilia na kumjadili huyu jamaa
 
Huyu jamaa kumbe alishawahi kuitwa kwa Rostamu AKAENDA!! Hajasema aliahidiwa nini labda na akakataa!?

Sijawahi kuona mwandishi mkongwe anaependa kuongelea watu badala ya Hoja, Aibu!
 
Back
Top Bottom