fikiria watz wote tunaji-tune kuwa 2015 ndio final, kuwa hakuna nchi baada ya hapo!? Imeandikwa wapi kuwa ujinga huu, unafiki huu, kutowajibika kwa watawala, rushwa iliyokithiri, incompetence ya watz nk vinaishia hapo!?Tusubiri fainali 2015
haya ndo yale anayayaongelea kibanda kwani viongozi na pro CDM mnakera sana pale ukweli ukisemwa juu yenu kwanini kama kweli mnajiamini mnapenda kusifiwa kila siku? kukosolewa na kuambiwa uwezo wa adui yako ni njia moja wapo ya kuweza kujipanga kwaajili ya mapambano,au ndo yale mkishapigwa chini 2015 mrudi na kutuambia wamechakachua? jua uwezo wa adui yako.So mlitaka aandike Kinana ni kilaza then mfurahi na kusherekea kutumia ruzuku hiyo ni challenge mnatakiwa mlifanyie kazi.
kwa hili Big up Kibanda.
Acheni kumpa huyu kanjanja umaarufu asio stahili; please ignore him with all the contempt he desreves. anapalilia ukuu wa wilaya; but he is in for a rude shock.
Karibuni tutaona makala zake nyingi zenye titles kama: Kinana dume la mbegu au Kinana mwanaume wa shoka! au Kinana muarobaini wa wapinzani!
Kwa wenye akili wameshaelewa hamasa na motisha Kibanda kuandika makala hizo unatokana na nini! Huyo ni mchumia tumbo mwingine huyo in the making.
ccm ilikofikia imebakiwa na mbinu moja tu ya kuwabakisha madarakani, ambayo ni kutumia vyombo vya dola, Polisi, usalama wa Taifa na JWTZ. Kama ni kimbunga basi kimbunga pekee kinachoweza kuwakumba na kuwasomba wanamageuzi na wapinzani kwa ujumla ni hivyo vyombo vya dola na si vinginevyo.
Hizi ndoto za Kibanda kwamba kinana ni kimbunga wacha aendelee kuota mwenyewe sisi huko tulishaondoka siku nyingi. Huwezi kumfananisha hata kidogo Augustine Mrema na Dr. Slaa, hawa ni watu wawili walio mbali sana kiuwezo na kwa muono. Yeye aendelee tu kula matunda ya kumsafisha Lowasa na sasa kumjenga Kinana kwakuwa si haba anajipatia ujira wake na kuweza kusukuma mbele gurudumu la maisha na familia yake, lakini atambue kitu kimoja kwamba ccm ilipofikia hakuna mganga yeyote anayeweza kuinusuru na anguko kuu mwaka 2015, si kinana wala vinana!!
Kitila, Mimi nakubaliana na Kibanda kuwa Kinana ni kimbunga (ndani ya CCM) ila sikubaliani na mawazo yake kuhusu viongozi na washabiki wa Chadema.Kipimo cha uvumilivu wa uongozi wa CHADEMA ni yeye kuendelea kuwa katika kampuni anayotaka kuikimbia hadi dakika hii atapoandika makala rasmi ya kumsifia Kinana na kukandia viongozi wa CHADEMA.
Tutashuhudia mengi kuelekea 2015.
Kipimo cha uvumilivu wa uongozi wa CHADEMA ni yeye kuendelea kuwa katika kampuni anayotaka kuikimbia hadi dakika hii atapoandika makala rasmi ya kumsifia Kinana na kukandia viongozi wa CHADEMA.
Mwita, na huo ndio ubaya wa viongozi wa vyombo hivyo kuwa wateule wa Rais (ambaye ni mkuu wa CCM pia). Hakuna cha CDF,IGP au wa TISS anayeweza kusimama hadharani na kusema watu wangu wasitumiwe na chama tawala.wewe na kibanda akili zenu zinafanana kama si kulingana.
Nimesema hivi na narudia, ccm ilikofikia sasahivi imebakiwa na mbinu moja tu ya kuwabakisha madarakani, ambayo ni kutumia vyombo vya dola, Polisi, usalama wa Taifa na JWTZ. Kama ni kimbunga basi kimbunga pekee kinachoweza kuwakumba na kuwasomba wanamageuzi na wapinzani kwa ujumla ni hivyo vyombo vya dola na si vinginevyo.