Kibanda aliteswa na majasusi!

Kibanda aliteswa na majasusi!

Gazeti la Mtanzania Jumapili leo limeibuka na habari moja kwenye ukurasa wake wa mbele yenye kichwa cha habari:"Kibanda aliteswa na majasusi".

Katika habari hii ya leo gazeti hili limegusa idara ya usalama wa Taifa kama ilivyokuwa kwa Mwanahalisi kabla ya kufungiwa.Aya moja katika habari hii inasema hivi:"Sasa kuna kila dalili zinazoonyesha kuwa utekelezaji wa mpango wa kumteka na kumtesa kinyama Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya New Habari(2006) LTD,Absalom Kibanda,ulifanywa na watu waliopata mafunzo wanayopewa maofisa usalama wa Taifa,Makachero wa Jeshi au wale wa Polisi,Mtanzania Jumapili linaripoti"

Sasa wadau kwa taarifa kama hii gazeti hili kweli litabaki salama?Gazeti halijatuhumu moja kwa moja idara hizo lakini limesema kitendo hicho kimefanywa na watu wanaopewa mafunzo ya maofisa usalama wa Taifa,Makachero wa Jeshi au Polisi.

Binafsi, sioni tatizo lolote katika taarifa hiyo kwani haijatuhumu moja kwa moja mtu yoyote wala idara yoyote ile ya serikali.

Swali,je hawataachwa kutishwa?

Idara husika za serikali ikiwemo Idara ya Habari na Maelezo zitakaa kimya?
 
Mtu yeyote anaeshabikia uovu nae ni mwovu. na adhabu yake ni hapahapa duniani

Wengi wao ni utoto na ulimbukeni! Bahati mbaya tumejenga mfumo wa watu kutowajibika kwa matendo na kauli zao kwa hiyo watu wanaona ni sawa tu kusema chochote!
 
kwan Rz1 alichafuaje hali ya hewa? nijuzeni tafadhali hiyo ilinipita. Pole kwa mhanga
 
ridhiwan na salma wasipodhibitiwa watalipelekea Taifa mahali pabaya sana, wanadhalilisha heshima ya urais kitu wanachosahau ni kuwa majina yao hayajawahi kutokea kwenye ballot paper wakati wa uchaguzi, washauri wa rais watekeleze wajibu wao kuzuia kadhia hii.

Mkuu.
Rais amejidhalilusha mwenyewe kitambo mbona
 
Acha kuota wewe, wapi umemsikia mwenyekiti wa madaktari akileta usumbufu baada ya kufanywa vibaya kule mabwepande? Zaidi zaidi Kibanda atakuwa na adabu ili hilo jicho lililobaki liendelee kuwepo..!
Ni Kweli tumewaona watekaji wakitamba wakiwa wameachiwa ofisi na KOva Kwa mfano Ahmed Msangi pamoja na kutajwa na Dr Ulimboka,Ramadhani Ignodu Kutajwa na Dr Ulimboka wameongezwa vyeo,Kamhunda anakula bata kwa mrija pale pale Iringa huku mke na watoto wa Mwangosi wakiendelea kulia machozi, hata mkuu wa kaya anadesa tu kusafiri dunia nzima akila kuku kwa mrija udikteta anaofanya kwenye nchi hii akumbuke yeye pia anawatoto hawajafika hata miaka kumi ka maana wana maisha marefu ya kuishi na doa analofanya baba yao
 
Una uhahkika na unayoyasema?
Na ile kampuni yake ya Caspian inayofanyafanya kazi kwenye migodi ya dhahabu kanda ya ziwa nayo iko Juba?

Kujitoa kwenye siasa za majukwaa haina maana kwamba ndo amejitoa siasa za Tanganyika, bado anahitaji sana kuendelea kudhibiti madaraka ya serikali ili kulinda mirija yake aliyowekeza Tanganyika.

Caspian ndiyo imepata tenda!! Nafikiri hujanielewa!! Nimesema hivi New Habari Corporation utaiona kazi yake hasa 2015 japo pia ndiyo inaanza rasmi baada ya Kibanda kuingia pale kuunganisha nguvu!! Si kwamba haina ndoa na serikali bali ndoa ile ni kwa mtu maalum kwa Chama hiki hiki tunachokizungumzia!!! Kwa kuwa ndoa hiyo haitakiwi na kundi lile lingine la mtandao basi kila kioja tutaona!! sasa umenielewa? Mafahali wanapigania jike!! Ha ha ha!!
 
Kuna watu wanataka kupotosha tukio la Kibanda

Jumapili, Machi 10, 2013 08:03 administrator

KUNA kila dalili ya baadhi ya watu fulani fulani kuanza kupotosha ukweli, kuhusu tukio la kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda.

Sisi Mtanzania Jumapili, tumesikitishwa na kufedheheshwa na watu ambao kwa sababu zao binafsi, wanataka kupotosha juu ya kile alichofanyiwa Kibanda wakati ambapo vyombo mbalimbali vya uchunguzi vinaendelea kufanya kazi yake.

Juzi, mtu aliyejitambulisha kwa jina la Ridhiwani Kikwete, alitumia mtandao wa kijamii wa facebook, kutoa maneno yenye mwelekeo wa kishabiki na kejeli kuhusu kushambuliwa kwa Kibanda, akihoji kama naye amefanyiwa unyama huo na Ikulu?

Kauli hii ya Ridhiwani, kama Mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, ni nzito na si ya kupuuza, hasa kwa wakati huu ambako vyombo vya dola vimetuaminisha kuwa vinafanya uchunguzi wenye nia ya kuwabaini na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika na tukio hilo.
.....simtetei mtu..lakini hapo kwenye red ..kunahitajika umakini mkubwa....bila hivyo nadhani upotoshaji utaweza kuwa mkubwa zaidi... ni wazo tu....
 
...............Katika uchunguzi huo, pia tumebaini kuwa aina ya mateso ya kung’oa watu kucha pia yamekuwa yakitumiwa na watu wa Usalama wa Taifa nchini Iran, ambako wao hutumia mashine kumnyofoa kucha............

mmmmhhhh....dah! ninajiuliza maswali mengi sana kufuatia hiyo statement.........anyway..tuendelee kupata habari mbali mbali.........
 
Huo utalaamu wa kung'oa kucha na meno huo unanitatiza.
 
Ni Kweli tumewaona watekaji wakitamba wakiwa wameachiwa ofisi na KOva Kwa mfano Ahmed Msangi pamoja na kutajwa na Dr Ulimboka,Ramadhani Ignodu Kutajwa na Dr Ulimboka wameongezwa vyeo,Kamhunda anakula bata kwa mrija pale pale Iringa huku mke na watoto wa Mwangosi wakiendelea kulia machozi, hata mkuu wa kaya anadesa tu kusafiri dunia nzima akila kuku kwa mrija udikteta anaofanya kwenye nchi hii akumbuke yeye pia anawatoto hawajafika hata miaka kumi ka maana wana maisha marefu ya kuishi na doa analofanya baba yao

....wamepanda vyeo!!?.......
 
Mkuu hao ni wale wale wanaojua ni kitu gani walifanya kwa hiyo wanakuja hapa ili kupindisha ukweli!!!! Wakati tukijadili ile thread ya kutekwa na kuumizwa kwake nilisema hivi "Adui yako mlete karibu ili ummalize kwa urahisi". Bado nasimamia maneno haya!!! Huwezi kuniambia kuwe leo hii nimekuandika kwa skendo kubwa za kifisadi withh evidence halafu eti nikuache!! Wahusika wana connect the dot!!! Kibanda pia ni mtu wa karibu sana na mwanamtandao wa Chama cha Mauaji na mtu huyo ni tishio kwa Rais ajaye!!!!! tulihofu ataendelea kumjenga kisiasa mtu huyo ili ifikapo 2015 aweze kuwa safi kwa Uhuru Kenyata!!!! Sasa tufanyeje kama si kummaliza!!! Ninaamini walijua wameshamuua!!! Kwa hakika ataendelea kuandika na kuandika na kuandika kwa jicho hilo hilo moja!!! Ila tu nimejifunza kuwa Uandishi wa Habari na Siasa ni hatari sana!! Ila kwa bahati mbaya ndivyo waandishi na wahariri wengi walivyo kwa Tanzania hasa inapokaribia uchaguzi!! Tuwe makini sana!! Jifunzeni toka uchaguzi wa Kenya uliopita walijirekebisha sana tofauti na 2007 ambapo walishabikia sana na mwishowe madhara waliyaona!!

Mkuu umeandika mengi mazuri lakini umekosea mahali pamoja tu!
Uchaguzi wa Kenya safari hii siyo kwamba waandishi waliuandika bila ushabiki, bali wasimamizi wa uchaguzi hawakuficha mambo yoyote yaliyohusu uchaguzi. Taratibu zote zilikuwa wazi kabisa na wananchi walipewa habari na kuelimishwa kuhusu ule uchaguzi kwa umakini mkubwa sana Sasa niambie kama tutakuwa na kamati ya uchaguzi ikawa na agenda za siri na mwanahabari akazigundua, je ni kosa kuziweka hadharani?? La hasha! waandishi wanao wajibu wa kuieleza jamii ukweli wa matukio yote nchini. Tunachotakiwa kuwaomba waandishi ni kutokuandika UWONGO.
La muhimu sana kwa waandishi wetu labda ni kuwaomba wawekeze zaidi kwenye utafiti wa kina kabla ya kuripoti au kuandika jambo. Wawekeze kwenye vifaa vya kisassa vya kukusanya habari ikiwemo kwa siri. Ilimradi kuwepo na ushahidi wa kutosha. Kwa kweli naipongeza IEBC ya Kenya wa kazi nzuri waliyoifanya.
 
Yaliotokea kwa Kidanda ni 'intimidation' and 'close call to death'. Tunachoshahuri ni kila msomaji wa hii habari ujue 'wewe' pia linakuhusu. The truth ni kwamba kazi za Kibanda na wengine wote (Everest Chahali, Erick Kabendera na hata Dr Ulimboka) ndizo zimewafanya wakawa targets na kujaribu kuwanyamazisha na kuwafunga midomo. Hii article ina links sources muhimu na inatoa sababu za muhimu na muhimu zaidi ni evidences kwanini serikali haiwezi kujikwepa kwa haya.

This is simple, waandishi wanaoandika habari za kushabikia ccm na kutojali upenzi wa Tanzania na wananchi hakuna 'intimidation wala death threats' kwao. Kama wanaofanya huu unyama ni foreign criminals au ujambazi hakuna basis yoyote ku-support this nonsense. Evidences and leads nyingi zinaonekana wazi wala hakuna kuanza kukuna kichwa, au tunahitaji FBI na hatuna wanaoupenda Utanzania.

We're so close and God is about to do wonders in Tanzania.

Tanzania Journalists Under Attack
Journalists in Tanzania are being intimidated by beatings, harassment and death threats. In the latest example, Absalom Kibanda, editor of the newspaper Mtanzania (The Tanzanian), was attacked outside his home and suffered serious head injuries.
He was taken to hospital in Dar-Es-Salaam but the gravity of his injuries may require him to be flown to South Africa for special treatment.
Kibanda, who is chairman of the Tanzania Editors Forum (TEF), is also the managing editor of the Swahile daily Tanzania Daima. The attack is thought to be related to his journalistic work.
TEF secretary general Meena Neville said: "They probably just want silence him through torture and intimidation".
The assault on Kibanda comes weeks after two other disturbing incidents. In the first, Scottish police informed a UK-based Tanzanian journalist, Evarist Chahali, that they had uncovered death threats against him.
In the second, journalist Erick Kabendera has been subjected to episodes of harassment apparently in retaliation for having testified against his former employer, the Tanzanian media mogul, Reginald Mengi, in a UK libel case in November last year.
His home in Tanzania has been burgled three times; officials have interrogated his elderly parents about their right to be Tanzanian citizens; and the couple were also told their son was under scrutiny for selling secrets to European powers.
Kabendera worked for a period in Britain in 2009 on The Times and The Independent through the David Astor journalism awards trust. His case has been highlighted by the former UK high commissioner to Kenya, Sir Edward Clay.
These three instances follow the murder of two journalists in separate incidents in late 2012 - Daud Mwangosi and Issa Ngumba - and last year's closure of the newspaper MwanaHalisi.
Sources: Article 19/African Arguments In Swahili: Raimwena
Tanzanian journalists under attack | Media | guardian.co.uk

kibanda.jpg
Look close to this picture?

Tanzania nchi ya amani na utulivu - give me a break
 
Katika uchunguzi huo, pia tumebaini
kuwa aina ya mateso ya kung’oa
watu kucha pia yamekuwa
yakitumiwa na watu wa Usalama wa
Taifa nchini Iran
, ambako wao
hutumia mashine kumnyofoa kucha.

Wakati uchunguzi wa Mtanzania
Jumapili ukibaini hayo, kumekuwa
na hali ya hofu kwa jamii kuhusiana
na matukio ya utekaji na utesaji
kinyama
yanayotekelezwa sasa kwa
baadhi ya watu maarufu hapa
nchini wanaotambulika kuwa na
misimamo inayokinzana na ile ya
serikali.

Je ni pamoja na kuruhusu uchapishaji wa habari za Markaz-Aljazeer?

Maana inaonyesha uwepo na utendaji kazi wa Markaz hiyo na nyingine mtindo huo zinajulikana ila zimeachwa tu makusudi zifanye kazi zake na wahusika wakuu ama wahusika wakuu hawajui lolote wanastahili kuachia madaraka yao. Wahusika wakuu ni Mkurugenzi wa UwT, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi.

Je! Ni kwasababu ya kuibua hili ndiyo maana wamem-Llimbokia nyumbani ili isifananefanane nau ya kwanza?

Hivi katika orodha ya Mwanahalisi, ile iliyolifanya gazeti kufungiwa, wangapi waliwahi kwenda China au Iran?
 
Mtanzania wanajaribu kuungaunga stori...ukweli utabaki pale pale kuwa kibanda ameteswa na mwajiri wake wa zamani

Ili iweje? Waliofanya hivyo nao walilenga kuwapata wenye upeo mdogo waamini kuwa kilichompata Kibanda ni kumhama mwajiri wake wa kwanza. Tena walifanya hivyo kuchonganisha wakijua watu watamhusisha Mbowe na CDM.
 
Kwa kawaida Majasusi ni kwa ajili ya watawala, mtawala akibadilika nao huhamia kwa mtawala mpya. Mtawala mpya akisema mteseni huyu , hata kama alikuwa mtawala Majasusi hawana maswali they have intuitive thinking.

Hilo neno Jasusi naona umelitumia/linatumika visivyo.........umeeleweka lakini
 
Back
Top Bottom