Kibanda aliteswa na majasusi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibanda aliteswa na majasusi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Mar 10, 2013.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26,955
  Likes Received: 44,884
  Trophy Points: 280
  SASA kuna dalili zinazoonyesha kuwa utekelezaji wa mpango wa kumteka na kumtesa kinyama Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, ulifanywa na watu waliopata mafunzo wanayopewa maofisa Usalama wa Taifa, Makachero wa Jeshi au wale wa Polisi, Mtanzania Jumapili linaripoti.

  Duru za uchunguzi za Mtanzania Jumapili zimebaini kuwa ni watu wenye mafunzo maalumu ya kutesa na kuua, waliyopata katika vyuo vya kijasusi wenye uwezo wa kutekeleza kwa ufanisi utesaji wa aina aliyofanyiwa Kibanda au ule wa awali uliotekelezwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka.

  Makachero kadhaa waliobobea, waliozungumza na gezeti hili kuhusu aina ya mateso ambayo yamepata kutolewa kwa baadhi ya Watanzania (akiwemo Kibanda) na kundi la watu ambalo hadi sasa halijafahamika, walieleza kuwa kwa ufahamu wa kazi yao ya ukachero, watu waliomteka na kumtesa Kibanda ni ama maofisa usalama, Makachero wa Jeshi au Polisi au watu waliopata mafunzo yanayolingana na watu wa kada hizo.

  Walisema wanaamini hivyo kwa sababu staili iliyotumika kumteka na kisha kumtesa, muda uliotumika kutekeleza utekaji na utesaji ni ule unaofundishwa katika vyuo vya kijasusi vilivyoko katika nchi za Magharibi na Asia ambavyo ni maalumu kwa ajili ya maofisa wa kijeshi na wale wa usalama.

  Kachero mwingine mstaafu aliyeulizwa kuhusu aina hiyo ya kuteka na kutesa alisema ni jambo lililo wazi kuwa watu ambao wamekuwa wakitekeleza unyama huo wana mafunzo ya kazi hiyo ambayo hutolewa kwa watu maalumu hususan maofisa usalama na wanajeshi.

  Alisema staili iliyotumika kumteka na kumtesa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Steven Ulimboka, ndiyo iliyotumika kwa asilimia 95 kwa Kibanda, ambayo kwa mwana usalama yeyote, akisimuliwa au kumuona mtu aliyeteswa kwa namna hiyo, anajua kazi hiyo imefanywa na watu wa aina gani.

  "Jambazi wa kawaida au mtu mwingine tu aliyeamua kufanya unyama siyo rahisi kwake kung'oa meno, kunyofoa kucha, kukata vidole, kuvunja mishipa na kutoboa macho bila kuwa na utaalamu wa kufanya kazi hiyo kwa wepesi na ufanisi kama inavyotokea sasa.

  "Anaweza akafanya hivyo lakini si kwa ufanisi kama ilivyo kwenye matukio ya Kibanda na Ulimboka. Unajua, kuna mambo ambayo yako wazi, kazi za kitaalamu zinajulikana kuwa zimefanywa kitaalamu na za kienyeji nazo zinajulikana. Haya mambo yanafanywa na watu wenye ujuzi wa kazi hiyo, sasa hatujui ni akina nani, lakini ukweli unabaki hivyo kuwa watu hawa wana utaalamu wa kutesa na kuua," alisema.

  Utafiti iliofanywa na Mtanzania Jumapili umeonyesha kuwa makachero wa mashirika makubwa ya kijasusi duniani na hasa wa Nchi za Magharibi na zile za kikomunisti, hutesa watu waliowakusudia kwa sababu mbalimbali kwa staili kama aliyoteswa nayo Kibanda na Ulimboka.

  Mateso ya aina hii hutolewa kwa watu wanaolazimishwa kutoa taarifa za siri au kukiri jambo walilolificha moyoni.

  Kwa mujibu wa mtandao wa plisonplanet.com, utesaji wa kukata viungo vya binadamu hutekelezwa ili kumlazimisha mtu atoe taarifa au akiri jambo analolificha na kwamba hata baadhi ya mataifa ya Asia na Afrika hutumia mbinu hizi yalizozipata kutoka Nchi za Asia na Magharibi.

  Taarifa za utesaji wa aina hiyo zilizo katika mitandao mbalimbali inayofuatilia mienendo ya kiintelijensia zinaeleza kuwa staili hiyo ya kinyama kutekelezwa kwa binadamu (slow slicing) na ilianzia nchi ya China katika miaka ya 600 AD hadi mwaka 1905 ilipokatazwa. Hata hivyo, inabainishwa kuwa mateso ya aina hiyo bado yapo katika baadhi ya nchi, zikiwemo za Afrika zinazotajwa kuongozwa kidikteta.

  Sehemu ya taarifa iliyo katika tovuti hiyo inasomeka kuwa; ‘katika mateso ya aina hii, mtesaji hutumia kisu chenye ncha kali kutoa jicho, kung'oa au kukata masikio, pua, ulimi, vidole, na kabla ya kuendelea na hivyo hukata vipande vidogo vya nyama kutoka sehemu za mapaja na mabega.

  ‘Mchakato mzima wa mateso ya namna hii huendelea kwa karibu siku tatu ili kumlazimisha mteswaji kueleza au kukiri jambo na inakadiliwa kuwa mteswaji hukatwa karibu mikato 3,600 kabla ya kufariki dunia.'

  Katika uchunguzi huo, pia tumebaini kuwa aina ya mateso ya kung'oa watu kucha pia yamekuwa yakitumiwa na watu wa Usalama wa Taifa nchini Iran, ambako wao hutumia mashine kumnyofoa kucha.

  Wakati uchunguzi wa Mtanzania Jumapili ukibaini hayo, kumekuwa na hali ya hofu kwa jamii kuhusiana na matukio ya utekaji na utesaji kinyama yanayotekelezwa sasa kwa baadhi ya watu maarufu hapa nchini wanaotambulika kuwa na misimamo inayokinzana na ile ya serikali.

  Tukio la kwanza lililoibua hofu ya kuwepo kwa kikundi maalumu chenye mafunzo ya kutesa na kuua ni lile la Dk. Ulimboka, ambaye akiwa katikati ya mzozo mkali na serikali kwa wadhfa aliokuwa nao wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, alitekwa, akateswa vibaya na kwenda kutupwa katika msitu wa Pande, akiwa nusu maiti.

  Dk. Ulimboka aliteswa kwa kupigwa mateke, ngumi, kung'olewa meno, kunyofolewa kucha na kuvunjwa baadhi mifupa ya mwili wake, zikiwemo mbavu. Mateso kama hayo ndiyo aliyoteswa nayo Kibanda.

  RAIS KIKWETE AMJULIA HALI KIBANDA

  Katika hatua nyingine, juzi Rais Jakaya Kikwete alimtembelea Kibanda katika hospitali aliyolazwa ya Mill Park, iliyopo mji wa Johannesburg, nchini Afrika Kusini kwa lengo la kumjulia hali.

  Rais Kikwete alikuwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana.

  Habari zinaeleza kuwa Rais Kikwete alitumia fursa ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukoloni na ubaguzi wa rangi, unaofanyika nchini humo, kwenda kumuona Kibanda.

  Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa; Kikwete ambaye alizungumza na Kibanda kwa takribani dakika tano, alisema aliongea na Mwajiri wa Kibanda, ambaye alimueleza kuwa suala la matibabu alikuwa akilishughulikia, hivyo kwa upande wao serikali, itaendelea na uchunguzi na kuhakikisha wale wote waliohusika katika tukio hilo wanakamatwa.

  KIBANDA AFANYIWA OPERESHENI

  Madaktari bingwa watatu, wakiwemo wa kichwa na jicho, jana walimfanyia operesheni Kibanda, iliyochukua takribani masaa matano na nusu.

  Katika operesheni hiyo ya kurekebisha taya na mishipa inayozunguka jicho, hata hivyo madaktari hao walishindwa kuokoa jicho lake na hivyo kuliondoa kwa ajili ya kumuwekea jingine la bandia.

  Ripoti ya madaktari kuhusu kile kilichofanyika ndani ya chumba cha operesheni itatolewa leo.

  Kibanda alivamiwa na watu wasiojulikana wakati anajiandaa kufunguliwa lango la kuingia nyumbani kwake, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam Machi 5 mwaka huu na kumjeruhi sehemu kadhaa za mwili wake na kisha kumng'oa meno, kucha na kumjeruhi vibaya jicho lake la kushot

  CHANZO:MTANZANIA JUMAPILI.
   
 2. mukizahp2

  mukizahp2 JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2013
  Joined: Jul 28, 2012
  Messages: 639
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  [h=2] Kuna watu wanataka kupotosha tukio la Kibanda [/h] Jumapili, Machi 10, 2013 08:03 administrator

  KUNA kila dalili ya baadhi ya watu fulani fulani kuanza kupotosha ukweli, kuhusu tukio la kuvamiwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda.

  Sisi Mtanzania Jumapili, tumesikitishwa na kufedheheshwa na watu ambao kwa sababu zao binafsi, wanataka kupotosha juu ya kile alichofanyiwa Kibanda wakati ambapo vyombo mbalimbali vya uchunguzi vinaendelea kufanya kazi yake.

  Juzi, mtu aliyejitambulisha kwa jina la Ridhiwani Kikwete, alitumia mtandao wa kijamii wa facebook, kutoa maneno yenye mwelekeo wa kishabiki na kejeli kuhusu kushambuliwa kwa Kibanda, akihoji kama naye amefanyiwa unyama huo na Ikulu?

  Kauli hii ya Ridhiwani, kama Mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, ni nzito na si ya kupuuza, hasa kwa wakati huu ambako vyombo vya dola vimetuaminisha kuwa vinafanya uchunguzi wenye nia ya kuwabaini na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika na tukio hilo.

  Kwa muktadha huo, Ridhiwani kwa kauli yake inaonyesha wazi kwamba wapo watu ambao anawafahamu waliohusika na tukio la kumtesa vibaya Kibanda.

  Hivyo basi Ridhiwani ana wajibu wa kulisaidia Jeshi la Polisi katika suala zima la kuwatambua watu hao na si vinginevyo.

  Asipofanya hivyo, tutaamini pasipo shaka kabisa kwamba Ridhiwani ana agenda ya siri katika tukio zima la kuteswa kwa Kibanda kutokana na kauli yake hiyo.

  Vyombo vya dola kama kweli viko huru vinapaswa kuifanyia kazi kauli hii ya Ridhiwani na visipofanya hivyo, basi watakuwa wanajipotezea imani kwa Watanzania na itakuwa ni kiashiria kimojawapo cha kuwaandaa wananchi siku moja kwenda katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kushitaki.

  Kibanda ni miongoni mwa Watanzania kadhaa waliofanyiwa unyama wa kutisha.

  Tunaamini wapo Watanzania au wenye ndugu zao waliowahi kukumbana na kadhia kama hii ya Kibanda, na yumkini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, hawa sidhani kama wanapenda kusikia lugha za kejeli wakati wana vidonda mioyoni mwao.

  Mbali na Ridhiwani, pia wapo wanasiasa ambao nao wameonekana kutumia tukio la Kibanda kama daraja lao la kisiasa, hawa nao wasiachwe.

  Wapo baadhi ya watu ambao si rahisi kuwabaini majina yao halisi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii, kutoa maoni yenye lengo ya kuunusuru upande fulani Fulani, hao nao watazamwe.

  Mwisho tunavishauri vyombo vya usalama vifanye kazi yake kwa umakini, na hatutarajii kuona mambo kama haya yakijirudia tena.

  SORCE MTANZANIA JUMAPILI
   
 3. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2013
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,851
  Likes Received: 889
  Trophy Points: 280
  ridhiwan na salma wasipodhibitiwa watalipelekea Taifa mahali pabaya sana, wanadhalilisha heshima ya urais kitu wanachosahau ni kuwa majina yao hayajawahi kutokea kwenye ballot paper wakati wa uchaguzi, washauri wa rais watekeleze wajibu wao kuzuia kadhia hii.
   
 4. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26,955
  Likes Received: 44,884
  Trophy Points: 280
  Haya sasa wale "wanafiki" waliokuwa wakizusha upuuzi wao kuhusu mwajiri wake wa awali, watafakari taarifa hii!.
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2013
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,746
  Likes Received: 987
  Trophy Points: 280
  Kweli nchi inajifanya kuwa iko mstari wa mbele kwa demokrasia kumbe ni kandamizi na udikteta tu!! Kwa nini tubake demokrasia? Waandishi wa habari wakiwemo editors ambao walitokea huko huko kwenye uandishi wa habari wanasaidia sana kuelimisha jamii, kuibua maovu ili mtu au nchi ijirekebishe, kutoa burudani, n.k. Sasa pale ambapo mtu anakosolewa tena kwa ushahidi badi hataki ila anachotaka ni kubaka demokrasia kwa ama kuua, kutesa au kutishia maisha ya mwandishi. Shujaa Kibanda, hata kama utabaki na jicho moja lakini bado utaandika na kuhariri habari!! You are a hero na historia itabaki kuwa historia. Pole sana mkuu Kibanda.
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2013
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,746
  Likes Received: 987
  Trophy Points: 280
  Mkuu hao ni wale wale wanaojua ni kitu gani walifanya kwa hiyo wanakuja hapa ili kupindisha ukweli!!!! Wakati tukijadili ile thread ya kutekwa na kuumizwa kwake nilisema hivi "Adui yako mlete karibu ili ummalize kwa urahisi". Bado nasimamia maneno haya!!! Huwezi kuniambia kuwe leo hii nimekuandika kwa skendo kubwa za kifisadi withh evidence halafu eti nikuache!! Wahusika wana connect the dot!!! Kibanda pia ni mtu wa karibu sana na mwanamtandao wa Chama cha Mauaji na mtu huyo ni tishio kwa Rais ajaye!!!!! tulihofu ataendelea kumjenga kisiasa mtu huyo ili ifikapo 2015 aweze kuwa safi kwa Uhuru Kenyata!!!! Sasa tufanyeje kama si kummaliza!!! Ninaamini walijua wameshamuua!!! Kwa hakika ataendelea kuandika na kuandika na kuandika kwa jicho hilo hilo moja!!! Ila tu nimejifunza kuwa Uandishi wa Habari na Siasa ni hatari sana!! Ila kwa bahati mbaya ndivyo waandishi na wahariri wengi walivyo kwa Tanzania hasa inapokaribia uchaguzi!! Tuwe makini sana!! Jifunzeni toka uchaguzi wa Kenya uliopita walijirekebisha sana tofauti na 2007 ambapo walishabikia sana na mwishowe madhara waliyaona!!
   
 7. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26,955
  Likes Received: 44,884
  Trophy Points: 280
  Ni vigumu kuficha ukweli na ni vigumu kugeuza uongo kuwa ukweli!

  Yetu macho na masikio!
   
 8. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26,955
  Likes Received: 44,884
  Trophy Points: 280
  Mkuu wataishia kuumbuka tu!
   
 9. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2013
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,873
  Likes Received: 3,208
  Trophy Points: 280
  1. Ridhiwani Kikwete
  2. Pascal Mayala
  3. Nape Nnauye
  4. Christopher Lukosi
  5....
  6....
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2013
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 207
  Trophy Points: 160

  Rafiki yangu Pasco Mayala nadhani atasoma hili Uandishi wa Habari na Siasa ni hatari sana!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2013
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,155
  Likes Received: 605
  Trophy Points: 280
  Nahisi wafuasi wengi wa cdm wana mafunzo hayo kulingana na inavyosemwa. Sasa sijui walifundishwa kwa lengo gani! Wafuasi wa cdm wenyewe hata jkt hawajaenda ndo sembuse kujifunza utesaji wa kijasusi! Mimi mtu akinyofoa kucha au jino la mtu anapomtesa najua kabisa kwamba alikuwa anatafuta siri alizonazo mtu. Mhuni wa mtaani tungekuta kibanda kavunjika miguu na mikono yote maana wanapigapiga tu.
   
 12. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2013
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 14,068
  Likes Received: 1,395
  Trophy Points: 280
  Time will tell, 2015 si mbali
   
 13. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2013
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,446
  Likes Received: 295
  Trophy Points: 180
  mi nimeshaogopa hadi kutoa coment hapa naona kama wataniua na mimi.
   
 14. P

  Pwaaaa JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2013
  Joined: Feb 16, 2013
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ndo hivyo, majasusi hawa ipo siku watamteka na JK akiwa angani
   
 15. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2013
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,746
  Likes Received: 987
  Trophy Points: 280
  Mkuu Masanilo, si Pasco Mayala tu ongeza na Denis Msacky ya Mwananchi!! Kaka kuwa makini unatumika na umekubali kutumika!! Watangazaji wengine kama Kibonde hana sababu kabisa ya kushabikia Siasa au niseme kujipendekeza!! Sema hawa wanajipendekeza kwa mtandao ule mwingine ambao Kibanda alikuwa ule mwingine!! ha ha ha!! Sasa kuweni makini!!
   
 16. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2013
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,746
  Likes Received: 987
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha nimecheka mno!! Yaani sina hakika kama unaweza kumteka baba yako!! Ni jana tu maskini kijana kichaa aliweze kumuua bibi yake na ndugu wengine wa ukoo na mama yake alipiga nondo na spring akajua ameua!!! Ila huyu kijana ni kichaa!!! Sasa kwa hiyo hao nao watakuwa kichaa? Tanzania ile amani na upendo vimeishia wapi? Kwa hiyo vimekuwa historia? Askofu Mokiwa naye kakoswa koswa juzi na issue iko polisi kwa upelelezi!! Ha ha ha!! Kama wa ulimboka aliletwa wa maigizo na wa Kibanda hawajakamatwa je hawa wa Mh. Mokiwa ambao hawakufanikiwa kumng'oa memo, kucha, kuvunja taya, mbavu, fuvu la kichwa kuharibu, etc je watakamatwa?? Siri kali!!
   
 17. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2013
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,907
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Bahati mbaya sana haya MACHO na MASIKIO inaonekana ndiyo wanajitahidi kuyanyofoa (kama sio uhai wenyewe). MUNGU saidia nchi hii na WANANCHI WAKE.
   
 18. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2013
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,746
  Likes Received: 987
  Trophy Points: 280
  Usiogope Marire, unaisemea jamii yako ili angalao wakipita hapa wajue tunashindwa kuishi kwa amani kwa sababu ya kulea udini, ukabisa (hapa wanautumia kisanii ili kuangamiza Siasa za ukanda). Wajue kuwa Kenya nao wameamua kuwa na county na Governors wao!!!! Nasi tunahitaji hivyo kwa Tanzania maana nchi nzima Marais wote walishindwa kuleta maendeleleo sawia!!! Na itasaidia sana hata uchaguzi badala ya kutumia kodi za wananchi basi kila chama kitagigharamia kwa kutafuta hela zake. Imagine miaka ya uchaguzi shughuli za serikali zinasimama kwa kuwa pesa inapelekwa kwa uchaguzi!! Uchaguzi ukimalizika basi inaendelea kulipa madeni ya uchaguzi maana incidentals zinazidi bajeti ya awali!! sasa tutaendeshaje majukumu kwa ufanisi bila bajeti ya kutekeleza majukumu?
   
 19. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2013
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,579
  Trophy Points: 280
  Rafiki yangu na ndugu yangu leo nilipokea ujumbe huu kutoka kwa rafiki,japo mimi ni mkristu ningependa nishirikiane na wewe ili upate kujua kuwa usilolijua usiliseme.

  Kwenye hadithi za quran kuna mtu kwa jina la Luqman alipewa ujumbe huu"Anapokuwa na watu ahifadhi ulimi wake,na akumbuke mambo mawili wema wake kwa watu na ubaya wa watu kwake.Na awe kama ardhi kwa udhalili,na awe kama bahari kwa ukarim na awe kama usiku kwa kuhifadhi siri na amuogope mola wake aliyemuumba'.

  Sasa rafiki ni vizuri kuzuia neno la kuhisi mtu ubaya ukiwa huna uhakika.Tujifunze na tutafakari,kwa nini aliambiwa hivyo na tunajifunza nini kwa neno hilo.
   
 20. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2013
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,746
  Likes Received: 987
  Trophy Points: 280
  Tayari la Kidanda limeshaondoka na macho mawili ya mwanaharakati na mwandishi hodari Kubenea waliyamwagia Tindikali India wakayaokoa japo anavaa miwani!! Pamoja na yote aliendelea kuweka ukweli hadharani hadi walipolifungia Mwanahalisi na kufukuza kazi wale vijana 30 wa tigo waliohusika kutoa taarifa za uhakika za wale majasusi waliomteka Ulimboka!! Kweli tuache vitisho na tukubali ukweli.
   
Loading...