Kibanda aliteswa na majasusi!

sielewi hizi sympathy za kibanda zinatoka wapi? off course mtu kuteswa siyo kitu kizuri, lakini was this guy a vanguard of good journalism in Tz? NO. no. this is a biased, subjective journalist, who is there for sectional interests of the few (angalia jinsi alivyokua anawashambulia kambi ya Mwakyembe, sitta na kutetea kila kitu cha RA na EL). I dont say he deserved to be tortured, but our sympathy should be measured in relation to truly what Kibanda stand for, what he has done, and who Kibanda is.

kama hatuwezi kua hivyo basi sisi ni taifa la wanafiki, tukiongozwa na viongozi wanafiki wakiwemo hao akina Kibanda na wenzake.
 
sielewi hizi sympathy za kibanda zinatoka wapi? off course mtu kuteswa siyo kitu kizuri, lakini was this guy a vanguard of good journalism in Tz? NO. no. this is a biased, subjective journalist, who is there for sectional interests of the few (angalia jinsi alivyokua anawashambulia kambi ya Mwakyembe, sitta na kutetea kila kitu cha RA na EL). I dont say he deserved to be tortured, but our sympathy should be measured in relation to truly what Kibanda stand for, what he has done, and who Kibanda is.

kama hatuwezi kua hivyo basi sisi ni taifa la wanafiki, tukiongozwa na viongozi wanafiki wakiwemo hao akina Kibanda na wenzake.
hii sympath imetokea wapi?Tena haohao wanaotoa sympath hapa wakati jamaa anahamia Habari corp ndo walikua mbele kumsema na kumtakia mambo mabaya.

Hizi ni siasa,kila oppotunity inayotokea watu wanaangalia itawanufaisha vipi kisiasa.
 
SASA kuna dalili zinazoonyesha kuwa utekelezaji wa mpango wa kumteka na kumtesa kinyama Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, ulifanywa na watu waliopata mafunzo wanayopewa maofisa Usalama wa Taifa, Makachero wa Jeshi au wale wa Polisi, Mtanzania Jumapili linaripoti.

Duru za uchunguzi za Mtanzania Jumapili zimebaini kuwa ni watu wenye mafunzo maalumu ya kutesa na kuua, waliyopata katika vyuo vya kijasusi wenye uwezo wa kutekeleza kwa ufanisi utesaji wa aina aliyofanyiwa Kibanda au ule wa awali uliotekelezwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka.

Makachero kadhaa waliobobea, waliozungumza na gezeti hili kuhusu aina ya mateso ambayo yamepata kutolewa kwa baadhi ya Watanzania (akiwemo Kibanda) na kundi la watu ambalo hadi sasa halijafahamika, walieleza kuwa kwa ufahamu wa kazi yao ya ukachero, watu waliomteka na kumtesa Kibanda ni ama maofisa usalama, Makachero wa Jeshi au Polisi au watu waliopata mafunzo yanayolingana na watu wa kada hizo.

Walisema wanaamini hivyo kwa sababu staili iliyotumika kumteka na kisha kumtesa, muda uliotumika kutekeleza utekaji na utesaji ni ule unaofundishwa katika vyuo vya kijasusi vilivyoko katika nchi za Magharibi na Asia ambavyo ni maalumu kwa ajili ya maofisa wa kijeshi na wale wa usalama.

Kachero mwingine mstaafu aliyeulizwa kuhusu aina hiyo ya kuteka na kutesa alisema ni jambo lililo wazi kuwa watu ambao wamekuwa wakitekeleza unyama huo wana mafunzo ya kazi hiyo ambayo hutolewa kwa watu maalumu hususan maofisa usalama na wanajeshi.

Alisema staili iliyotumika kumteka na kumtesa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Steven Ulimboka, ndiyo iliyotumika kwa asilimia 95 kwa Kibanda, ambayo kwa mwana usalama yeyote, akisimuliwa au kumuona mtu aliyeteswa kwa namna hiyo, anajua kazi hiyo imefanywa na watu wa aina gani.

“Jambazi wa kawaida au mtu mwingine tu aliyeamua kufanya unyama siyo rahisi kwake kung’oa meno, kunyofoa kucha, kukata vidole, kuvunja mishipa na kutoboa macho bila kuwa na utaalamu wa kufanya kazi hiyo kwa wepesi na ufanisi kama inavyotokea sasa.

“Anaweza akafanya hivyo lakini si kwa ufanisi kama ilivyo kwenye matukio ya Kibanda na Ulimboka. Unajua, kuna mambo ambayo yako wazi, kazi za kitaalamu zinajulikana kuwa zimefanywa kitaalamu na za kienyeji nazo zinajulikana. Haya mambo yanafanywa na watu wenye ujuzi wa kazi hiyo, sasa hatujui ni akina nani, lakini ukweli unabaki hivyo kuwa watu hawa wana utaalamu wa kutesa na kuua,” alisema.

Utafiti iliofanywa na Mtanzania Jumapili umeonyesha kuwa makachero wa mashirika makubwa ya kijasusi duniani na hasa wa Nchi za Magharibi na zile za kikomunisti, hutesa watu waliowakusudia kwa sababu mbalimbali kwa staili kama aliyoteswa nayo Kibanda na Ulimboka.

Mateso ya aina hii hutolewa kwa watu wanaolazimishwa kutoa taarifa za siri au kukiri jambo walilolificha moyoni.

Kwa mujibu wa mtandao wa plisonplanet.com, utesaji wa kukata viungo vya binadamu hutekelezwa ili kumlazimisha mtu atoe taarifa au akiri jambo analolificha na kwamba hata baadhi ya mataifa ya Asia na Afrika hutumia mbinu hizi yalizozipata kutoka Nchi za Asia na Magharibi.

Taarifa za utesaji wa aina hiyo zilizo katika mitandao mbalimbali inayofuatilia mienendo ya kiintelijensia zinaeleza kuwa staili hiyo ya kinyama kutekelezwa kwa binadamu (slow slicing) na ilianzia nchi ya China katika miaka ya 600 AD hadi mwaka 1905 ilipokatazwa. Hata hivyo, inabainishwa kuwa mateso ya aina hiyo bado yapo katika baadhi ya nchi, zikiwemo za Afrika zinazotajwa kuongozwa kidikteta.

Sehemu ya taarifa iliyo katika tovuti hiyo inasomeka kuwa; ‘katika mateso ya aina hii, mtesaji hutumia kisu chenye ncha kali kutoa jicho, kung'oa au kukata masikio, pua, ulimi, vidole, na kabla ya kuendelea na hivyo hukata vipande vidogo vya nyama kutoka sehemu za mapaja na mabega.

‘Mchakato mzima wa mateso ya namna hii huendelea kwa karibu siku tatu ili kumlazimisha mteswaji kueleza au kukiri jambo na inakadiliwa kuwa mteswaji hukatwa karibu mikato 3,600 kabla ya kufariki dunia.’

Katika uchunguzi huo, pia tumebaini kuwa aina ya mateso ya kung’oa watu kucha pia yamekuwa yakitumiwa na watu wa Usalama wa Taifa nchini Iran, ambako wao hutumia mashine kumnyofoa kucha.

Wakati uchunguzi wa Mtanzania Jumapili ukibaini hayo, kumekuwa na hali ya hofu kwa jamii kuhusiana na matukio ya utekaji na utesaji kinyama yanayotekelezwa sasa kwa baadhi ya watu maarufu hapa nchini wanaotambulika kuwa na misimamo inayokinzana na ile ya serikali.

Tukio la kwanza lililoibua hofu ya kuwepo kwa kikundi maalumu chenye mafunzo ya kutesa na kuua ni lile la Dk. Ulimboka, ambaye akiwa katikati ya mzozo mkali na serikali kwa wadhfa aliokuwa nao wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, alitekwa, akateswa vibaya na kwenda kutupwa katika msitu wa Pande, akiwa nusu maiti.

Dk. Ulimboka aliteswa kwa kupigwa mateke, ngumi, kung’olewa meno, kunyofolewa kucha na kuvunjwa baadhi mifupa ya mwili wake, zikiwemo mbavu. Mateso kama hayo ndiyo aliyoteswa nayo Kibanda.

RAIS KIKWETE AMJULIA HALI KIBANDA

Katika hatua nyingine, juzi Rais Jakaya Kikwete alimtembelea Kibanda katika hospitali aliyolazwa ya Mill Park, iliyopo mji wa Johannesburg, nchini Afrika Kusini kwa lengo la kumjulia hali.

Rais Kikwete alikuwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana.

Habari zinaeleza kuwa Rais Kikwete alitumia fursa ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi wa Vyama vilivyokuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukoloni na ubaguzi wa rangi, unaofanyika nchini humo, kwenda kumuona Kibanda.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa; Kikwete ambaye alizungumza na Kibanda kwa takribani dakika tano, alisema aliongea na Mwajiri wa Kibanda, ambaye alimueleza kuwa suala la matibabu alikuwa akilishughulikia, hivyo kwa upande wao serikali, itaendelea na uchunguzi na kuhakikisha wale wote waliohusika katika tukio hilo wanakamatwa.

KIBANDA AFANYIWA OPERESHENI

Madaktari bingwa watatu, wakiwemo wa kichwa na jicho, jana walimfanyia operesheni Kibanda, iliyochukua takribani masaa matano na nusu.

Katika operesheni hiyo ya kurekebisha taya na mishipa inayozunguka jicho, hata hivyo madaktari hao walishindwa kuokoa jicho lake na hivyo kuliondoa kwa ajili ya kumuwekea jingine la bandia.

Ripoti ya madaktari kuhusu kile kilichofanyika ndani ya chumba cha operesheni itatolewa leo.

Kibanda alivamiwa na watu wasiojulikana wakati anajiandaa kufunguliwa lango la kuingia nyumbani kwake, Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam Machi 5 mwaka huu na kumjeruhi sehemu kadhaa za mwili wake na kisha kumng’oa meno, kucha na kumjeruhi vibaya jicho lake la kushot

CHANZO:MTANZANIA JUMAPILI.[/QUOTE


haya yote yanatokana na udhaifu ulioonekana tangu 2005.ni namna ya kukwepa majukumu na kutisha watu ili wasiweke wazi madhaifu ya dhaifu.na huyu dogo RIZI asubiri babake atoke madarakani lazima..................................... .ngoja nikajimwagie maji hasira iishe nisije andika vibaya hapa
 
No suala hapa lazima liwe clear. Huyo RZ1 anao uhuru wa kusema kama ambavyo nyie pia mnasema.mbona hamkutaka wote waliojifanya wanajua ikulu ilivyomtesa ulimboka wakaisaidie polisi kiushahidi? Jambo sikubaliani na unyama aliofanyiwa kibanda lakin pia sitaki uhuru wa maoni udhibitiwe,watu waachwe waseme kama walivyosema ktk matukio mengi mengi yaliyopita.


nenda kaache uharo wako chooni ndo uje humu jamvini.au Umeolewa na RIZ mwanaume weye?
 
Masuala ya uislamu na ukristu hayahusiki hapa, ishia hapohapo.

sio suala la uislam ama ukristo tunazungumzia kuteswa na watu walio fundishwa na hawa bila shaka ndio wale walio fundishwa kuwatesa wasilam kwa kisingizio cha ugaidi..sasa wakikiosa nyama yao wanakula nyengine..nadhani umeelewa..
kama kukataa askari wetu kufundishwa kutesa basi iwe kwa aina yoyoyte ya jamii..
 
Back
Top Bottom