Kiama cha bomoabomoa Kibaha maili moja ni tar 23 January

Kiama cha bomoabomoa Kibaha maili moja ni tar 23 January

Kama wamelipwa fidia na wameridhika bila kinyongo basi hamna noma, ubomoaji uendelee, la sivyo...
 
Hakuna anaijua siku ya KIAMA

neno KIAMA ni neno zito!sasa najiuliza nilichoambiwa masjid kuhusu kiama na huyu bwana alivolitumia hili neno hivi anaelewa asemayo!
Je kwenye uandishi mbalimbali mimi ndio wa kwanza kulitumia?au akili zetu zimejielekeza kutumia umeme wa single phase?
 
Mshana neno kiama sio zuri kwani hamna hata mtu atayekufa wala kupata jakamoyo kwa kuwa watu wote wameshalipwa fidia. Linalofanyika hapo ni jema sana maana Kibaha ilikuwa mailimoja ilikuwa imechoka sana utadhani stendi za mikoani kumbe ni km 30 toka Ikulu. Mie ni mzawa wa Kibaha naunga mkono huo mpango
funzadume neno hilo hutumika zaidi ya maana moja kumbuka kiswahili ni lugha yenye neno moja lenye tafsiri zaidi ya moja
 
Kibaha is my home town,my all. Ni muda muafaka kubadilika
20170114_165159.jpg
20170114_165132.jpg
 
Zimebakia siku chache sana kabla matingatinga ya serikali kuingia ndani ya mji mdogo wa Kibaha maili moja kubomoa na kusafisha eneo lote tayari kwa ujenzi na uwekezaji wa kisasa ikiwemo mahoteli na majumba makubwa ya masoko stendi nk.

Watu wameshalipwa fidia na ubomoaji ulikuwa ufanyike tangu tarehe 23 November 2016 lakini ulichelewa kutokana na matatizo ya hapa na pale ambapo sasa yametatuliwa na maandalizi yote yameshakamilika na ubomoaji wa hiari kunusuru vinavyoweza kunusurika piga picha sasa ya maili moja kama kumbukumbu kwakuwa hutakaa uione Kibaha uliyoizoea.
Watu wamelipwa fidia wewe unaita kiama, sasa hicho kiama cha nini ikiwa hakuna anaeathirika na hilo zoezi.......Au ni kiama kwa serikali iloyolipa fidia.?
 
neno KIAMA ni neno zito!sasa najiuliza nilichoambiwa masjid kuhusu kiama na huyu bwana alivolitumia hili neno hivi anaelewa asemayo!
Huko masjid wanafundisha kuhusu 'kiama' au 'kiyama'?
 
Kiama sio neno dogo kwa wenye imani.
Ni kweli lakini bahati mbaya sikuandika kwa mlengo wa kiimani na kwakweli hili neno linatumika mahali pengi tu sijui kwanini limekuwa mjadala mimi kulitumia kwenye ishu ya bomoabomoa ya Kibaha
 
Watu wamelipwa fidia wewe unaita kiama, sasa hicho kiama cha nini ikiwa hakuna anaeathirika na hilo zoezi.......Au ni kiama kwa serikali iloyolipa fidia.?
Duu itabidi nifafanue kila reply inayohusu kiama
Kiama kinakuja kwenye hizo nyumba na uwekezaji wote wa zamani kwakuwa hakuna kuchagua pote panapigwa chini na kupangwa upya
 
Back
Top Bottom