Hivi umefika kweli Zanzibar? hao watanganyika 1000 ni nusu tuu ya wale wanaojiita wamasaai . Kwa taarifa yako watanganyika wanaoisha Zanzibar hawapungui laki moja (100,000)... Hawa ni raia tuu.

Hakuna mzanzibari anaesubiri kujengewa hoja na Dr,Slaa au Mtikila na wengine , hilo ilikuwa tu, kukumbusha kwamba sio wazanzibari tuu , wanaotaka serikali tatu. Na wewe na kundi lako mnaoshikilia serikali mbili nikidogo sana iwe kwa Tanganyika au kwa Tanzania kwa jumla. Mimi binafsi sitaki hata kuusikia muungano na wala sina haja ya kujenga hoja kwa hilo.

Wanachodai wazanzibar ni kurudushiwa kwa mamlaka ya serikali ya SMZ. Watu wamechoka na muungano wa serikalimbili "butu". Serikali tatu, Tanganyika, Zanzibar na Muungano. Hiyo formula mnayotumia kugawa mapato ya muungano ndio formula hiyo hiyo itumike kulipia gharama za muungano.

Mkuu Takashi heshima mbele, unaweza kuniambia kwa nini wanzazibar wanataka mamlaka ya serikali ya SMZ wakati hiyo serikali tayari ipo na nadhan ina mamlaka kamili? Kingine SMZ ilikaa madarakani kabla ya Muungano kwa muda wa siku kama 100, unaweza kuniambia SMZ ndani ya siku 100 za kwanza nje ya Muungano ilifanya nini cha maana na ilikuwa na mamlaka gani kabla ya Muungano na sasa mamlaka hayo hayapo baada ya Muungano?