takashi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2009
- 905
- 188
Mkuu hilo suala la mafuta ni hoax tu, kuna mtu aliwadanganya wazenji kuwa kuna mafuta. Ukweli ni kuwa kuna mwamba wa mafuta Pemba, na kuna dalili za kuwepo kwa mafuta. Lakini hakuna uhakika kama mafuta yakichimbwa yanaweza kurudisha investement iliyowekwa kwenye uchimbaji, kwa hiyo ni hear say tu inayotumiwa na wanasiasa wenye lengo la kujitafutia madaraka. Hakuna lolote. Kama kweli mafuta yangekuwepo Zanzibar for sure makampuni malafi yangeshafika na kuanza kuchimba, mafuta ya Afrika ni many cases ni mazuri kuliko ya uarabuni, so kama kweli yangekuwepo yangechimbwa tu. Anayesema yapo anatakiwa kutuambia ni lini walifanya utafiti na ni nani na majibu ya utafiti huo yako wapi na yamefanyiwa kazi gani, na waseme ni kwanini hayajafanyiwa kazi.
Mkuu baadhi ya wazanzibar wa ile kauli ya chetu changu, changu changu. So wanajua kabisa wana maana gani. Sidhani kama kuna haja ya kuuliza kama muungano ukivunjika waliko hapa bara watafanya nini. Jibu ni rahisi kabisa walipo hapa bara watarudi kwao, wakitaka kukaa wanakaribishwa, watakaa kama wageni wengine. I am sure wanajua hilo, naona ni vizuri wakiruhusiwa kufanya wanachokitaka. Si kama wao hawajui itakuwaje muungano utakapovunjika, wanajua kabisa lakini wanaona ni heri uvunjike ili wapate mafuta.
wazanzibari wamekua wakidai haki zao kabla ya suala la mafuta kuibuka... Kutokuwepo kwa mafuta hakutamzuwia mzanzibari kudai haki zake, kamwe... Vile vile wazanzibari hawataacha kudai haki zao eti kwasababu kuna wapemba wanamaduka bara...you have invested in a failed strategy...Hao wapemba kama ikibidi watarudi ,na hayo maduka watafungua Zanzibar na nyinyi baadae mtafata bidhaa zanzibar.
kama kweli wanaume rudisheni Tanganyika !