Hamad M. Hamad: Zanzibar imefanya chaguzi 6, ni mbili tu hazikuwa na mauaji

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Dar es Salaam, Agosti 23, 2023 – Katika Mkutano wa kujadili demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD). Hamad M. Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Waziri wa zamani wa Miundombinu na Mawasiliano, amezungumzia hatua zilizofikiwa katika kufanikisha mazingira bora ya kisiasa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Hamad M. Hamad amesema kuwa Zanzibar imeshuhudia chaguzi sita na ni chaguzi mbili tu ambazo hazikusababisha ghasia za umwagaji damu, ambazo ni chaguzi za mwaka 2015 na 2010. Ameelezea makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa wakati huo, Karume na Maalim Seif, ambayo yalisaidia kuepusha ghasia.

Amesema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya uchaguzi unasimamiwa na CCM, na ameuliza ni kwa nini viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa, ambao hawatajwi katika sheria ya uchaguzi, wanashiriki katika usimamizi wa uchaguzi.

Kuhusu Zanzibar, Hamad amezungumzia umuhimu wa kutumia sheria ya uchaguzi iliyotumika mwaka 2010 na 2015 ili kuhakikisha mazingira bora ya kisiasa na kuzuia ghasia kutokea.
 
nyinyi mtajua wenyewe na mambo yenu.Kwanza sio sehemu ya tanzania
Mkuu kwani kwenye zile vurugu walikuwa Wazanzibar peke yao?

Hata Watanzania bara walifariki Mkuu, maana wengi ndiyo walienda kule kama Walinzi wa amani na wengine wasimamizi wa Uchaguzi bila kusahau wengine waliokuwa wanatafuta Mkate wao wa kila siku huko Zanzibar

Mungu asaidie chaguzi za amani
 
hao wabara wana kiherehere, kwani huko zenji walinzi hawana? si wana jeshi lao na hao wasimamizi wa uchaguzi kwani huko hamna watu??
 
Dar es Salaam, Agosti 23, 2023 – Katika Mkutano wa kujadili demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD). Hamad M. Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Waziri wa zamani wa Miundombinu na Mawasiliano, amezungumzia hatua zilizofikiwa katika kufanikisha mazingira bora ya kisiasa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Hamad M. Hamad amesema kuwa Zanzibar imeshuhudia chaguzi sita na ni chaguzi mbili tu ambazo hazikusababisha ghasia za umwagaji damu, ambazo ni chaguzi za mwaka 2015 na 2010. Ameelezea makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa wakati huo, Karume na Maalim Seif, ambayo yalisaidia kuepusha ghasia.

Amesema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya uchaguzi unasimamiwa na CCM, na ameuliza ni kwa nini viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa, ambao hawatajwi katika sheria ya uchaguzi, wanashiriki katika usimamizi wa uchaguzi.

Kuhusu Zanzibar, Hamad amezungumzia umuhimu wa kutumia sheria ya uchaguzi iliyotumika mwaka 2010 na 2015 ili kuhakikisha mazingira bora ya kisiasa na kuzuia ghasia kutokea.
Kwani Mkapa si aliandika?
 
hao wabara wana kiherehere, kwani huko zenji walinzi hawana? si wana jeshi lao na hao wasimamizi wa uchaguzi kwani huko hamna watu??
Nina jamaa zangu wawili walifia huko wakiwa wanatimiza majukumu

Jeshini ni amri tu, ikitoka Juu wewe ni kutekeleza
 
Dar es Salaam, Agosti 23, 2023 – Katika Mkutano wa kujadili demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD). Hamad M. Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Waziri wa zamani wa Miundombinu na Mawasiliano, amezungumzia hatua zilizofikiwa katika kufanikisha mazingira bora ya kisiasa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Hamad M. Hamad amesema kuwa Zanzibar imeshuhudia chaguzi sita na ni chaguzi mbili tu ambazo hazikusababisha ghasia za umwagaji damu, ambazo ni chaguzi za mwaka 2015 na 2010. Ameelezea makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa wakati huo, Karume na Maalim Seif, ambayo yalisaidia kuepusha ghasia.

Amesema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya uchaguzi unasimamiwa na CCM, na ameuliza ni kwa nini viongozi wa ngazi ya wilaya na mkoa, ambao hawatajwi katika sheria ya uchaguzi, wanashiriki katika usimamizi wa uchaguzi.

Kuhusu Zanzibar, Hamad amezungumzia umuhimu wa kutumia sheria ya uchaguzi iliyotumika mwaka 2010 na 2015 ili kuhakikisha mazingira bora ya kisiasa na kuzuia ghasia kutokea.
Safi sana bwana Hamad.
 
Back
Top Bottom