PostGE2025 Kesi ya Viongozi wa CHADEMA kuidharau amri ya Mahakama yatupiliwa mbali

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam kesi ya kudharau amri ya Mahakama iliyokuwa imefunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake dhidi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake wa Tanzania Bara John Heche yametupiliwa mbali

Akisoma uamuzi wa Mahakama hiyo leo, Ijumaa Novemba 28.2025 Jaji Awamu Mbagwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuwa imefunguliwa kwa hati ya dharura amesema, Mahakama imekubaliana na pingamizi lililokuwa limewekwa na Wakili wa utetezi Hekima Mwasipu kuwa maombi hayo yameletwa Mahakamani hapo nje ya muda

Jaji Mbagwa amesema kesi ya msingi namba 8960/2025 iliyoko chini ya Jaji Hamidu Mwanga ndio iliyokuwa msingi wa kesi iliyokuwa mbele yake, na kwamba amri ya Mahakama kuzuia shughuli za kisiasa za CHADEMA ilitolewa na Mahakama Juni 10.2025

Aidha, Jaji Mbagwa ameendelea kufafanua kuwa kesi ya kudharau amri ya Mahakama ililetwa Mahakamani hapo Oktoba 03 mwaka huu takribani siku 106 jambo ambalo halikubaliki kisheria, Sheria inataka maombi ya aina hiyo yaletwe ndani ya siku 60.

Chanzo: Jambo TV
 
Akisoma uamuzi wa Mahakama hiyo leo, Ijumaa Novemba 28.2025 Jaji Awamu Mbagwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuwa imefunguliwa kwa hati ya dharura amesema, Mahakama imekubaliana na pingamizi lililokuwa limewekwa na Wakili wa utetezi Hekima.Mwasipu kuwa maombi hayo yameletwa Mahakamani hapo nje ya muda

Jaji Mbagwa amesema kesi ya msingi namba 8960/2025 iliyoko chini ya Jaji Hamidu Mwanga ndio iliyokuwa msingi wa kesi iliyokuwa mbele yake, na kwamba amri ya Mahakama kuzuia shughuli za kisiasa za CHADEMA ilitolewa na Mahakama Juni 10.2025

Aidha, Jaji Mbagwa ameendelea kufafanua kuwa kesi ya kudharau amri ya Mahakama ililetwa Mahakamani hapo Oktoba 03 mwaka huu takribani siku 106 jambo ambalo halikubaliki kisheria, Sheria inataka maombi ya aina hiyo yaletwe ndani ya siku 60.

Chanzo: Jambo TV
Hao majaji ni mafala hawana kazi za.kufanya
 
Hakuna chombo huru hapa Tanzania,kila kitu kinaendeshwa kwa maelezo
 
Kwa hiyo kina heche waendelee na shughuli za siasa? Kama ndivyo malengo yao(ccm) yamefanikiwa. Kuzuia ule moto wa NRNE, mpaka uchaguzi ukaaisha.
 
Wale jamaa wa memo toka juu wako busy na maazimio ya Bunge la Ulaya. Wakasahau leo kuna jambo Mahakamani. Wangetuma memo kama kawaida yao kwa Hakimu kuahirisha kesi mpaka January next year.
 
Safi sana, wafutilie mbali na kesi ya Lissu, huenda upepo mkali ukabadilika na tuone mjuba Lissu ana impact gani na hawa gen z wanaokinukisha wanapata wapi jeuri
 
Hizo kesi zilikuwa kuzuia cdm kufanya shughuli zake wakati wa uchaguzi, hakuna lolote la maana hapo. Kesi zote zitatupiliwa mbali, maana yalikuwa ni maagizo ya hila, na mahakama zikapewa maagizo.
 
Wale jamaa wa memo toka juu wako busy na maazimio ya Bunge la Ulaya. Wakasahau leo kuna jambo Mahakamani. Wangetuma memo kama kawaida yao kwa Hakimu kuahirisha kesi mpaka January next year.
Mambo mengi wako busy sanaaa haahhahahahahahhqhq mwisho wa siku Mtoto Tundu wanamshuhudia akihutubia wananchi bila wao kujua katokaje.
 
Shimboni Makamanda

Leo, Ijumaa Novemba 28.2025, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi yaliyokuwa yamewasilishwa Mahakamani hapo na Said Issa Mohamed (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar) na wenzake wawili (2) dhidi ya Viongozi waandamizi na makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake wa Tanzania Bara John Heche

Maombi hayo yaliyofunguliwa Oktoba 03 mwaka huu yalikuwa yanadai kuwa washtakiwa wamekiuka amri ya Mahakama Kuu iliyotolewa Juni 10.2025 kupitia kesi ya madai namba 8960/2025 inayosikilizwa chini ya Jaji Hamidu Mwanga, ambapo washtakiwa wake ni Katibu Mkuu na Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA

Pamoja na mambo mengine, katika uamuzi wake Jaji Awamu Mbagwa amesema Mahakama imekubaliana na moja ya mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi ikiwemo lile lililokuwa linaeleza kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kisheria wa kusikiliza maombi hayo kutokana na kwamba yamewasilishwa nje ya muda uliotajwa kisheria

Amesema amri inayohusu marufuku kwa CHADEMA kujihusisha na shughuli zozote za kisiasa na kiutendaji imetolewa Juni 10 mwaka huu, lakini kwa mujibu wa waleta maombi wanasema mshtakiwa wa kwanza John Heche 'alihutubia' Juni 17 mwaka huu, na maombi ya kudharau amri ya Mahakama yamewasilishwa Mahakamani hapo Oktoba 03 mwaka huu, ambapo siku 106 baadaye suala ambalo linakinzana na matakwa ya sheria inayotaka maombi ya aina hiyo yawasilishwe ndani ya siku 60,
 
Kesi iliyotupiliwa mbali, ni ile ya kudharau amri ya mahakama tu.

Kesi ya mgawanyo wa mali bado haijatolewa uamuzi(dalali mbowe atarudishiwa ghorofa yake tu!) kwa maana yuko upande wa kuume wa mtesi.
 
Hakukuwa na kesi boss, bali dola ilifungua kesi ili kuzuia nguvu ya NRNE. Lengo ilikuwa ni kuhakikisha wizi huu wa kura October 29 unafanyika bila kipingamizi. Hata Lisu ataachiwa muda wowote maana tayari lengo limeshatimia. Nadhani anacheleweshwa maana ni kama hakubaliani na terms za kulamba asali.
 
Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam kesi ya kudharau amri ya Mahakama iliyokuwa imefunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake dhidi ya viongozi waandamizi wa CHADEMA wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake wa Tanzania Bara John Heche yametupiliwa mbali

Akisoma uamuzi wa Mahakama hiyo leo, Ijumaa Novemba 28.2025 Jaji Awamu Mbagwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuwa imefunguliwa kwa hati ya dharura amesema, Mahakama imekubaliana na pingamizi lililokuwa limewekwa na Wakili wa utetezi Hekima Mwasipu kuwa maombi hayo yameletwa Mahakamani hapo nje ya muda

Jaji Mbagwa amesema kesi ya msingi namba 8960/2025 iliyoko chini ya Jaji Hamidu Mwanga ndio iliyokuwa msingi wa kesi iliyokuwa mbele yake, na kwamba amri ya Mahakama kuzuia shughuli za kisiasa za CHADEMA ilitolewa na Mahakama Juni 10.2025

Aidha, Jaji Mbagwa ameendelea kufafanua kuwa kesi ya kudharau amri ya Mahakama ililetwa Mahakamani hapo Oktoba 03 mwaka huu takribani siku 106 jambo ambalo halikubaliki kisheria, Sheria inataka maombi ya aina hiyo yaletwe ndani ya siku 60.

Chanzo: Jambo TV
Upepo upepo umekua mkali sana
 
Hatutaki mahakama za ccm nchi hii, tuandamane D9 kuzikataa.
 
Back
Top Bottom