Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,882
- 828,453
Nimepokea taarifa ya kusikitisha na ya kutia wasiwasi kutoka kwa Rais wa Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK), Wakili Faith Odhiambo, kuhusu kunyimwa kuingia nchini Tanzania kwa Mawakili Gloria Kimani (Mjumbe wa Baraza la LSK), Martha Karua, na Lyn Ngugi. Mawakili hawa walipanga kuhudhuria na kushuhudia mwenendo wa kesi inayoendelea dhidi ya Wakili Tundu Antipas Lissu katika Mahakama ya Mwanzo ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Kwa kujibu hali hii, nimechukua hatua za haraka kwa kumtuma Wakili Hekima Mwasipu kufuatilia kwa kina suala hili ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe.
Tunapenda kuwakumbusha mamlaka husika kwamba nchi hii inaongozwa kwa misingi ya utawala wa sheria na Katiba yake, na hakuna zuio lolote la kisheria linalokataza mtu yeyote kuhudhuria kesi ya wazi mahakamani kuhusu mashtaka yanayomkabili Wakili Tundu Antipas Lissu.
Tunaomba kwa dhati kwamba mawakili hawa waruhusiwe kuingia nchini, kwani uwepo wao ni ushahidi wa dhamira yetu ya kuendeleza haki na usawa mbele ya jumuiya ya kimataifa.
Yanayoendelea kwa sasa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na Katiba ya nchi. Kama Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), tunafuatilia kwa makini hali hii.
Aidha, pamoja na kupeleka mawakili kumuunga mkono Wakili Tundu Lissu katika kesi hiyo kesho, mimi binafsi nitahudhuria kikao cha mahakama kwa wakati uliopangwa.
Tunaziomba Idara ya Uhamiaji ijiepushe na matendo yanayoharibu taswira ya taifa letu kwa kuchochea migogoro isiyo ya lazima na isiyo na msingi wowote.
Tunalaani vikali na kudai kusitishwa mara moja kwa vitendo hivi visivyo halali vinavyoaibisha na kudhalilisha heshima ya nchi yetu.
BAK Mwabukusi
Rais, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)