Kesi ya Uhaini ya Lissu: Jamhuri yakosa mashahidi!

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
11,797
Reaction score
18,038
Baada ya Tundu Lissu kukiri kutamka maneno ya uasi na kukinukisha Jamuhuri imekosa mashahidi. Mawakili wa Serikali walidhani kuwa Lissu angekanusha matamshi yake kwa hiyo wakaandaa mashahidi, video na clips lukuki ambazo zingeonyesha hotuba alizozitoa kwa watia nia wa Chadema, mikutano ya hadhara aliyofanya katika Kanda zote alizotembelea na mazungumzo yote aliyofanya na vyombo vya habari.

Kwa mshangao wa Mawakili wa Serikali Lissu amekubali yote na sasa wana jukumu la kuchimbua katika vitabu vya sheria kama je matamshi yake ni uhaini? Hapo nawaona Mawakili wa Serikali jasho jembamba likiwatoka na misuli ya vibofu vya mikojo na utumbo mnene inayobana vinyesi ikilegea!

Kazi kwao Mawakili wa Serikali, na kwa hakika Lissu ni Big Brain Defender!
 
Kilaza Katuga wa mama anasema Lissu asielezee historia yake wakati ni moja ya vitu vya msingi katika utetezi.

Hawa vilaza wanasema eti Lissu ni askari wa akiba maana ana kiapo cha JKT hivyo anatakiwa kumtii amiri jeshi mkuu.

Hawa vilaza hata basics za uraia hawajui tofauti ya utii na uzalendo?
 
Baada ya Tundu Lissu kukiri kutamka maneno ya uasi na kukinukisha Jamuhuri imekosa mashahidi. Mawakili wa Serikali walidhani kuwa Lissu angekanusha matamshi yake kwa hiyo wakaandaa mashahidi, video na clips lukuki ambazo zingeonyesha hotuba alizozitoa kwa watia nia wa Chadema, mikutano ya hadhara aliyofanya katika Kanda zote alizotembelea na mazungumzo yote aliyofanya na vyombo vya habari.

Kwa mshangao wa Mawakili wa Serikali Lissu amekubali yote na sasa wana jukumu la kuchimbua katika vitabu vya sheria kama je matamshi yake ni uhaini? Hapo nawaona Mawakili wa Serikali jasho jembamba likiwatoka na misuli ya vibofu vya mikojo na utumbo mnene inayobana vinyesi ikilegea!

Kazi kwao Mawakili wa Serikali, na kwa hakika Lissu ni Big Brain Defender!
Utakua mweupe wa sheria lakini
 
Utakua mweupe wa sheria lakini
Screenshot_20250725-185609~2.png
 
Back
Top Bottom