Kesi ya Tundu Lissu sio ya kushangilia

Kesi ya Tundu Lissu sio ya kushangilia

Kwani huyu mwakibinga yupi? Unasema amewahi kuwa huku, lini na alitokea wapi?

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Alikuwaha Rais wa wanafunzi UDOM, enzi hizo migomo kibao alikua kamanda haswaa yaani aliwapa muda mgumu sana CCM kwa nondo zake. Then alikuwa nominated apewe uenyekiti BAVICHA taifa ila hakufanikiwa, then 2015 akawa amejiandaa kugombea jimbo la Lupa huko mbeya, alikatwa akahamia ACT na alianguka vibaya mno naona akaamua kusahau yote CCM waliomtendea akaenda kujiunga nao.

Kinachohuzunisha alipokua CHADEMA alikua anaongea nondo mno kuhusu uwajibikaji wa serikali lakini toka amerudi CCM kazi yake ni kutukana,kukosoa upinzani ilimradi apate uteuzi.

Inasikitisha sana
 
Si anaumwa au unadhan alikuwa disco kama wew mbinua sembe
Mkuu hata sisi tunajua kabisa kesi hii bado kabisa.
Ukiwasikiliza mawakili hata Tundu mwenyewe. Husikii yeyote akielezea hoja mbili za Ndugai
yaani
-kwa nini hakumtaarifu Bosi wake RASMI
- Kwa nini hakujaza form ya maadili.
Kwa sasa tunajiandaa kudai "mahakama zetu hazipo HURU" iwapo Lissu akishindwa.
Si UNATUFAHAMU?
 
Mimi nina swali dogo,wakati hii kesi inaendelea hadi iishe huyu mteule si atakuwa ameapishwa kama hakuna zuio?Pointi yangu ni kwamba hizi kesi zaaina hii aghalabu huchukua muda mrefu.
Hapana kesi ilipangwa isikilizwe kwa mfululizo na kutolewa maamuzi ila CCM kwa kufahamu hilo wananunua muda kwa technicalities ili kesi iweze sogea hata kwa mwaka!!
Ila nachofahamu kma mahakama ikiona Lissu katolewa kimakosa itatakiwa nafasi yake irudishwe bila kujali kuna mtu kaapishwa au lah.
 
Alikuwaha Rais wa wanafunzi UDOM, enzi hizo migomo kibao alikua kamanda haswaa yaani aliwapa muda mgumu sana CCM kwa nondo zake. Then alikuwa nominated apewe uenyekiti BAVICHA taifa ila hakufanikiwa, then 2015 akawa amejiandaa kugombea jimbo la Lupa huko mbeya, alikatwa akahamia ACT na alianguka vibaya mno naona akaamua kusahau yote CCM waliomtendea akaenda kujiunga nao.

Kinachohuzunisha alipokua CHADEMA alikua anaongea nondo mno kuhusu uwajibikaji wa serikali lakini toka amerudi CCM kazi yake ni kutukana,kukosoa upinzani ilimradi apate uteuzi.

Inasikitisha sana
Cha ajabu sasa yupo chini ya Le mutuz na cyprian musiba anapewa maagizo na watu wasio na chembe ya Akili unategemea nini hapo?
 
Hapana kesi ilipangwa isikilizwe kwa mfululizo na kutolewa maamuzi ila CCM kwa kufahamu hilo wananunua muda kwa technicalities ili kesi iweze sogea hata kwa mwaka!!
Ila nachofahamu kma mahakama ikiona Lissu katolewa kimakosa itatakiwa nafasi yake irudishwe bila kujali kuna mtu kaapishwa au lah.
Wapo wajanja wale madalali wa siasa wamejichomeka humo ili wavune pesa na vyeo teuzi nk ndiyo wamekuwa chachu ya kuingilia uhuru wa mahakama
 
Watetezi wa CCM kwa 100% ni vilaza mbumbumbu ingawa hujiona ni wajanja lakini watambue kuwa watanzania siyo wajinga wanajua Sinema zao zote A_Z
 
Yawezekana mleta mada akawa mmoja wapo wa mawakili wanapwakilisha kila risasi iliyoingia mwilini wa Lissu? Risasi 16, mawakili 16.

Kama ni mmoja wapo basi sishangai kuisoma hii thread yake
Atakuwa ni mmojawapo na pengine kwa upeo wake Mdogo alidhani akija na mifano ile atafanikiwa kuwashawishi watanzania waamini ujinga wao
 
Huyo mbunge alichaguliwa na nani
Ni wa kuteuliwa sio wa kuchaguliwa hivyo wananchi wanayo haki ya kumkataa,kwani atawakilisha maslai ya anayemlipa Kwa mgongo wa wananchi Raha ya ubunge ni kuchaguliwa sio kuletewa nyumbani.
 

Attachments

  • Screenshot_2019-08-27-08-03-38.png
    Screenshot_2019-08-27-08-03-38.png
    401.1 KB · Views: 19
  • Screenshot_2019-08-27-07-53-58.png
    Screenshot_2019-08-27-07-53-58.png
    144.8 KB · Views: 19
Hii tabia ya wanasiasa kujifanya wanajua kila kitu imetufikisha hapa. Kwa nini msiwaache wataalam wa sheria wabishane na wengine muwe watazamaji? Vyombo vya habari vimeandika vizuri tu, kulikuwa na haja ya wewe kuandika ushabiki huu? Ndugu yangu Philipo Mwakibinga siasa ina mipaka yake. Ili udumu katika siasa jifunze miiko na mipaka yake na uishike. Uwe na siku njema!
 
LISSU BADO HAJAKWAMUA KISIKI KUZUIA KUAPISHWA KWA MHE. MTATURU...

Kuna upotoshaji unaendelea kwenye mitandano kuhusu maamuzi ya Mahakama juu ya mapingamizi ya Serikali kwenye kesi iliyofunguliwa na Tundu Lissu dhidi ya Mhe.Spika.

Ifahamike kuwa:

1.Tundu Lissu aliwasilisha maombi ya kibali (Leave) cha Mahakama Kuu kuruhusiwa kufungua maombi ya Kiutawala (Judicial Review) kupinga uamuzi wa Mhe. Spika kumvua ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambapo tayari kuna Mbunge ameshachaguliwa na anasubiri tu kuapishwa (Mhe. Miraji Mtaturu).

2. Lissu katika ombi lake la msingi kaomba kuzuia kuapishwa kwa mbunge huyo anataka Mahakama itamke kuwa uamuzi huo ulikuwa batili. Hata hivyo, ubunge wake ulikoma kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(c) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

3. Lissu ameomba kupatiwa uamuzi wa Spika wa kumwondolea Ubunge kama ulichapishwa kwenye Gazeti la Serikali. Maombi hayo ameleta kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi sura Toleo la 2015.

4. Kilichojiri Mahakamani leo tarehe 26.08.2019 pamoja na baadhi ya mapingamizi ys utetezi kutokubalika:

(i). Mahakama imeafikiana na hoja za Upande wa Utetezi kuwa kuna mapungufu katika hati za viapo vilivyowasilishwa na upande wa Lissu hivyo kuviondoa vipengele vyote kwenye viapo hivyo.

(ii). Mahakama imekataa kutoa Amri yoyote ya kuzuia kuapishwa kwa Mbunge Mteule mpaka itakaposikiliza pande zote mbili.

(iii) Mahakama imetaka pande zote mbili zikawasilishe hoja zao kuhusu maombi ya kibali cha kuomba mapitio ya uamuzi wa Mhe. Spika tarehe 02.08.2019.

KWA UAMUZI HUO, NI WAZI KUWA NGOMA HAIJAISHA IPO PALE PALE.....
Wala hakuna upotoshaji washangaliaji sie roho zetu kwa kwa hatua hii tuna amani, Kama Taifa Stars walivyofika Afcon hata wakifungwa mechi zote sie poa sababu dunia imeshaona mdhalimu ni Nani na Hila zake ni zipi.
TL mpaka hapa ni mshindi, tunajuwa Jiwe na anaowatuma hawatakubali kushindwa lakini nafsi zao zimeshakosa amani kwa matendo yao na dhamira ya mbovu kwa binadamu wenzao. Kuweka Kijiji Cha mawakili imetosha kusema wauwaji bado wanania na nguvu kubwa ya kutekeleza dhamira yao lakini Mungu Mkubwa.
 
Hizi si ndio mahakama zikitoa maelezo tofauti na matakwa upande fulani zinasemwa zinatumika? Msije kuwa vinyonga mbele ya safari tu.

Mahakama zinatumika, hilo halina mjadala. Usidhani kwa huo uamuzi wa jana unatosha kuonyesha kwamba hawatumiki.
 
LISSU BADO HAJAKWAMUA KISIKI KUZUIA KUAPISHWA KWA MHE. MTATURU...

Kuna upotoshaji unaendelea kwenye mitandano kuhusu maamuzi ya Mahakama juu ya mapingamizi ya Serikali kwenye kesi iliyofunguliwa na Tundu Lissu dhidi ya Mhe.Spika.

Ifahamike kuwa:

1.Tundu Lissu aliwasilisha maombi ya kibali (Leave) cha Mahakama Kuu kuruhusiwa kufungua maombi ya Kiutawala (Judicial Review) kupinga uamuzi wa Mhe. Spika kumvua ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambapo tayari kuna Mbunge ameshachaguliwa na anasubiri tu kuapishwa (Mhe. Miraji Mtaturu).

2. Lissu katika ombi lake la msingi kaomba kuzuia kuapishwa kwa mbunge huyo anataka Mahakama itamke kuwa uamuzi huo ulikuwa batili. Hata hivyo, ubunge wake ulikoma kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(c) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

3. Lissu ameomba kupatiwa uamuzi wa Spika wa kumwondolea Ubunge kama ulichapishwa kwenye Gazeti la Serikali. Maombi hayo ameleta kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi sura Toleo la 2015.

4. Kilichojiri Mahakamani leo tarehe 26.08.2019 pamoja na baadhi ya mapingamizi ys utetezi kutokubalika:

(i). Mahakama imeafikiana na hoja za Upande wa Utetezi kuwa kuna mapungufu katika hati za viapo vilivyowasilishwa na upande wa Lissu hivyo kuviondoa vipengele vyote kwenye viapo hivyo.

(ii). Mahakama imekataa kutoa Amri yoyote ya kuzuia kuapishwa kwa Mbunge Mteule mpaka itakaposikiliza pande zote mbili.

(iii) Mahakama imetaka pande zote mbili zikawasilishe hoja zao kuhusu maombi ya kibali cha kuomba mapitio ya uamuzi wa Mhe. Spika tarehe 02.08.2019.

KWA UAMUZI HUO, NI WAZI KUWA NGOMA HAIJAISHA IPO PALE PALE.....
kinachoniuma hapa sio wewe kua chizi nooo kinachoumiza Hapa nijinsi tulivyo tumia nguvu kukutetea kipindi una majanga pale Dodoma chuo Inauma pia inakera kuja kugundua tuliempigania niwewe mvizia vyeo pale lumumba
 
LISSU BADO HAJAKWAMUA KISIKI KUZUIA KUAPISHWA KWA MHE. MTATURU...

Kuna upotoshaji unaendelea kwenye mitandano kuhusu maamuzi ya Mahakama juu ya mapingamizi ya Serikali kwenye kesi iliyofunguliwa na Tundu Lissu dhidi ya Mhe.Spika.

Ifahamike kuwa:

1.Tundu Lissu aliwasilisha maombi ya kibali (Leave) cha Mahakama Kuu kuruhusiwa kufungua maombi ya Kiutawala (Judicial Review) kupinga uamuzi wa Mhe. Spika kumvua ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambapo tayari kuna Mbunge ameshachaguliwa na anasubiri tu kuapishwa (Mhe. Miraji Mtaturu).

2. Lissu katika ombi lake la msingi kaomba kuzuia kuapishwa kwa mbunge huyo anataka Mahakama itamke kuwa uamuzi huo ulikuwa batili. Hata hivyo, ubunge wake ulikoma kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(c) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

3. Lissu ameomba kupatiwa uamuzi wa Spika wa kumwondolea Ubunge kama ulichapishwa kwenye Gazeti la Serikali. Maombi hayo ameleta kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi sura Toleo la 2015.

4. Kilichojiri Mahakamani leo tarehe 26.08.2019 pamoja na baadhi ya mapingamizi ys utetezi kutokubalika:

(i). Mahakama imeafikiana na hoja za Upande wa Utetezi kuwa kuna mapungufu katika hati za viapo vilivyowasilishwa na upande wa Lissu hivyo kuviondoa vipengele vyote kwenye viapo hivyo.

(ii). Mahakama imekataa kutoa Amri yoyote ya kuzuia kuapishwa kwa Mbunge Mteule mpaka itakaposikiliza pande zote mbili.

(iii) Mahakama imetaka pande zote mbili zikawasilishe hoja zao kuhusu maombi ya kibali cha kuomba mapitio ya uamuzi wa Mhe. Spika tarehe 02.08.2019.

KWA UAMUZI HUO, NI WAZI KUWA NGOMA HAIJAISHA IPO PALE PALE.....
sawa wakili kilaza wa serikali, tumekusikia.
 
Hivi mbona watu wasiojua sheria ndo wakwanza kujiweka mbele kuanza kuelezea maswala ya sheria..kilichofanyika ni serikali kutaka kesi isisikilizwe kabisa...hakuna sehemu iliafikiwa kuzuia uapishaji maana kesi ilikua haijafika katika hatua ya either kusikilizwa au kutosikilizwa
 
Huyu Mwakibinga ni moja ya wale ambao Membe aliwaita "vichaa wa Lumumba" ambao wanapiga Kelele mitandaoni, vyeo vinaenda kwa "wahamiaji". Kesi haina msingi wowote na Lissu atashinda kwani kilichofanywa na Ndugai ni uvunjifu wa Sheria na kukosa Utu. Serikali itashinda na Lissu atarudi Bungeni.
 
Sijui mnyakyusa Wa Wapi huyu? Tukuyu,busokelo ,Kyela au ipinda

Ndiyo tatizo la nyie Ndugu zetu mnapenda kupata habari zinazowafurahisha tu..hamtaki kupata uchambuzi wa issues...Mnataka muambiwe huyo ameshinda wakati hata hoja ya msingi haijasikilizwa...dah..pity..
 
Kama tumeshinda kesi twaweza enda South kuwekea mkazo kama jamaa maana alishinda kesi Bongo
Hivi sisi wa ndani tunao idai serikali hatuwezi tukaishikilia ndege moja pale JNIA
 
mada kama hizi ma cdm hawazipendi na zinataka kuwatoa roho hapo nimchezo wa sheria tu ngoma ndo kwanza inaanza lissu must be out
 
Back
Top Bottom