Kesi ya Tundu Lissu sio ya kushangilia

Kesi ya Tundu Lissu sio ya kushangilia

Swali zuri sana umemuuliza huyo kada wa Lumumba.......

Yeye ameeleza kuwa wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki, walipiga kura na kumchagua Mbunge Mtaturu, je anaweza kuitaja siku hiyo ulipofanyika uchaguzi huo??

Haya mambo mnayofanya CCM ya kupitisha wagombea wenu kibabe, sasa mwisho wake umekaribia sana........
Kumbe wewe ni mpuuzi! Soma tena maandishi yako
 
Kwa wapenda haki huu ni ushindi hata kama atashindwa mbeleni!! Moja ya mapingamizi ilikuwa ni kuwa Lissu hana haki ya kufungua shauri.

Wanaoamini katika haki ya kusikilizwa wameshinda. Ushindi huu uko katika dhana ya “haki sawa mbele ya sheria”.

Tabia ya kuchukua maamuzi bila kuwapa nafasi ya kujitetea watu ndio imetufikisha hapa.

Ni muda sasa wa haki kutendeka. Lissu hakuhudhuria vikao na hakujulikana alipo (kwa mujibu wa Spika) na hakujaza form za mali na madeni. Haya ndio yaliyomkosesha ubunge! Tujikite huko ili Bunge lioneshe lilifanya uamuzi sahihi na wa haki. Makahaka itapatiwa nafasi kufanya maamuzi katika hilo.
 
Kesi ilipofikia ni kama halftime goli ni moja moja,tukirudi kipindi cha pili Lisu ataongezwa goli tu,hata kama ni kwa goli la mkono
 
Hii ngoma bado sijaelewa,Bunge linaanza tar 3 September,je ktk mazingira hayo si anaweza kuapishwa ?
Bunge linaanza 16,Sept, 2019 siku ya jumanne ndiyo siku anatarajiwa kuapishwa.
 
Hivi kitendo cha mawakili 16 wa serikali kushindana na mawakili 4 tu kinaashiria nini katika aina ya mawakili wa serikali tulionao? Kwa hali hii kuna kesi kweli za kimataifa tutaweza shinda ata moja?
 
Hata akikosa Ubunge
Mtapoteza hela nyingi kulipia madeni
Na bado ndege ikitua UK twaikamata

Hivi sisi wa ndani tunao idai serikali hatuwezi tukaishikilia ndege moja pale JNIA
 
Hivi kitendo cha mawakili 16 wa serikali kushindana na mawakili 4 tu kinaashiria nini katika aina ya mawakili wa serikali tulionao? Kwa hali hii kuna kesi kweli za kimataifa tutaweza shinda ata moja?

Nadhani hatujawai kushinda hata moja...na uwezekano wa kushinda ni kama haupo
 
LISSU BADO HAJAKWAMUA KISIKI KUZUIA KUAPISHWA KWA MHE. MTATURU...

Kuna upotoshaji unaendelea kwenye mitandano kuhusu maamuzi ya Mahakama juu ya mapingamizi ya Serikali kwenye kesi iliyofunguliwa na Tundu Lissu dhidi ya Mhe.Spika.

Ifahamike kuwa:

1.Tundu Lissu aliwasilisha maombi ya kibali (Leave) cha Mahakama Kuu kuruhusiwa kufungua maombi ya Kiutawala (Judicial Review) kupinga uamuzi wa Mhe. Spika kumvua ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambapo tayari kuna Mbunge ameshachaguliwa na anasubiri tu kuapishwa (Mhe. Miraji Mtaturu).

2. Lissu katika ombi lake la msingi kaomba kuzuia kuapishwa kwa mbunge huyo anataka Mahakama itamke kuwa uamuzi huo ulikuwa batili. Hata hivyo, ubunge wake ulikoma kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(c) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

3. Lissu ameomba kupatiwa uamuzi wa Spika wa kumwondolea Ubunge kama ulichapishwa kwenye Gazeti la Serikali. Maombi hayo ameleta kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi sura Toleo la 2015.

4. Kilichojiri Mahakamani leo tarehe 26.08.2019 pamoja na baadhi ya mapingamizi ys utetezi kutokubalika:

(i). Mahakama imeafikiana na hoja za Upande wa Utetezi kuwa kuna mapungufu katika hati za viapo vilivyowasilishwa na upande wa Lissu hivyo kuviondoa vipengele vyote kwenye viapo hivyo.

(ii). Mahakama imekataa kutoa Amri yoyote ya kuzuia kuapishwa kwa Mbunge Mteule mpaka itakaposikiliza pande zote mbili.

(iii) Mahakama imetaka pande zote mbili zikawasilishe hoja zao kuhusu maombi ya kibali cha kuomba mapitio ya uamuzi wa Mhe. Spika tarehe 02.08.2019.

KWA UAMUZI HUO, NI WAZI KUWA NGOMA HAIJAISHA IPO PALE PALE.....
Mahakama haipo huru ingawa Jaji kaamua kujitoa muhanga, hakuna upotoshaji bali nyie ndiyo mnaingilia uhuru wa mahakama na kama mahakama isingekuwa ni mahakamaccm kila kitu kingemalizika mapema lakini sasa mahakama haifanyi kazi kwa mujibu wa Sheria bali inafanya kazi kwa mujibu wa zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM na nyinyi mliojitoa fahamu kwa makusudi.
 
Mbona mnatumia nguvu nyingi sana kutuaminisha upumbavu.

Mmeweka Mawakili Nguli 16 kwa kesi ya kumvua Lissu Ubunge na risasi bado ziliingia ndani ya Mwili wake.

Hamuoni fedheha.
Rais na mwenyekiti wa CCM alishasema kuwa watanzania siyo wajinga lakini naona na yeye kasahau kauli yake ndipo Le mutuz na cyprian musiba wakaenda kuchukua pesa kuwalipa vijana mbumbumbu waje kusumbua watu mitandaoni wakizani wataamini ujinga wao.
 
Mbona mnatumia nguvu nyingi sana kutuaminisha upumbavu.

Mmeweka Mawakili Nguli 16 kwa kesi ya kumvua Lissu Ubunge na risasi bado ziliingia ndani ya Mwili wake.

Hamuoni fedheha.
Mahakama haipo huru badala waende kuipigania ndege irudi Tanzania wamekazania kumkandamiza Tundu lisu.
 
Hii ngoma bado sijaelewa,Bunge linaanza tar 3 September,je ktk mazingira hayo si anaweza kuapishwa ?
Na CCM wanafahamu hilo ndio maana wanatumia delaying tactics na technicalities ili muda usogee huku kesi ya msingi haijasikilizwa..... All in all hata akiapishwa kama ikionekana Lissu alionewa basi itabidi jamaa apishe tu ingawa itakuwa complicated mno.
 
Eti mahakama imekataa kutoa amri ya kuzuia kuapishwa kwa mbunge mtaturu!

Nigga!

Hicho kitu kimeongelewa hili shauri la juzi?

Hilo limo kwenye kesi ya msingi!

Na kesi ya msingi bado haijaongelewa!

Sasa sijui unazungumzia kesi ya msingi kwa sababu gani?

Una vituko aisee!

Mmeshachanganyikiwa tayari!
Watetezi wa CCM mitandaoni kwa 100% huwa ni wale mbumbumbu kwani hukariri vile wanavyolishwa na cyprian musiba na Le mutuz ambao ni watu wajinga wanye IQ ndogo 0.01 la cha ajabu eti hulipwa mabilioni na CCM kwa kazi ya kuwatetea mitandaoni.
 
Na CCM wanafahamu hilo ndio maana wanatumia delaying tactics na technicalities ili muda usogee huku kesi ya msingi haijasikilizwa..... All in all hata akiapishwa kama ikionekana Lissu alionewa basi itabidi jamaa apishe tu ingawa itakuwa complicated mno.
Watalazimisha kienyeji huyo jamaa wao awe mbunge lakini atakuwa ni mbunge Haramu asiye chaguo la wapiga kura, lakini mungu atamsimamia Tundu Lisu ingawa wanatumia pesa nyingi mbinu mbalimbali kuihujumu kesi yake , Cha muhimu kwa sasa Dunia kote wametambua kuwa zipo juhudi za makusudi za kuipindisha Sheria ili kumkomoa Tundu Lisu
 
Back
Top Bottom