Kesi ya Tundu Lissu sio ya kushangilia

Kesi ya Tundu Lissu sio ya kushangilia

Philipo Mwakibinga

Senior Member
Joined
May 13, 2013
Posts
110
Reaction score
175
LISSU BADO HAJAKWAMUA KISIKI KUZUIA KUAPISHWA KWA MHE. MTATURU...

Kuna upotoshaji unaendelea kwenye mitandano kuhusu maamuzi ya Mahakama juu ya mapingamizi ya Serikali kwenye kesi iliyofunguliwa na Tundu Lissu dhidi ya Mhe.Spika.

Ifahamike kuwa:

1.Tundu Lissu aliwasilisha maombi ya kibali (Leave) cha Mahakama Kuu kuruhusiwa kufungua maombi ya Kiutawala (Judicial Review) kupinga uamuzi wa Mhe. Spika kumvua ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambapo tayari kuna Mbunge ameshachaguliwa na anasubiri tu kuapishwa (Mhe. Miraji Mtaturu).

2. Lissu katika ombi lake la msingi kaomba kuzuia kuapishwa kwa mbunge huyo anataka Mahakama itamke kuwa uamuzi huo ulikuwa batili. Hata hivyo, ubunge wake ulikoma kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(c) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

3. Lissu ameomba kupatiwa uamuzi wa Spika wa kumwondolea Ubunge kama ulichapishwa kwenye Gazeti la Serikali. Maombi hayo ameleta kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi sura Toleo la 2015.

4. Kilichojiri Mahakamani leo tarehe 26.08.2019 pamoja na baadhi ya mapingamizi ys utetezi kutokubalika:

(i). Mahakama imeafikiana na hoja za Upande wa Utetezi kuwa kuna mapungufu katika hati za viapo vilivyowasilishwa na upande wa Lissu hivyo kuviondoa vipengele vyote kwenye viapo hivyo.

(ii). Mahakama imekataa kutoa Amri yoyote ya kuzuia kuapishwa kwa Mbunge Mteule mpaka itakaposikiliza pande zote mbili.

(iii) Mahakama imetaka pande zote mbili zikawasilishe hoja zao kuhusu maombi ya kibali cha kuomba mapitio ya uamuzi wa Mhe. Spika tarehe 02.08.2019.

KWA UAMUZI HUO, NI WAZI KUWA NGOMA HAIJAISHA IPO PALE PALE.....
 
Huyo mbunge alichaguliwa na nani
Swali zuri sana umemuuliza huyo kada wa Lumumba.......

Yeye ameeleza kuwa wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki, walipiga kura na kumchagua Mbunge Mtaturu, je anaweza kuitaja siku hiyo ulipofanyika uchaguzi huo??

Haya mambo mnayofanya CCM ya kupitisha wagombea wenu kibabe, sasa mwisho wake umekaribia sana........
 
Mkuu hata kama ni kusaka uteuzi usipotoshe

1. Mahakama imesema moja ya pingamizi inayoongelea kiapo licha ya kuwa yana mashiko ila hayaathiri hoja za msingi zilizowasilishwa yaani hata hizo aya zikifutwa bado hoja zilizobaki zinatosha kusikilizwa kwa kesi.

2.Mahakama haijakataa kusimamisha kuapishwa kwa mbunge mteule bali imesema hiyo hoja iletwe na itasikilizwa wakati wa majadiliano ya kesi ya msingi kuanzia September 2.

Mkuu usipotoshe ili kupata uteuzi, ulipokua CHADEMA ulijua kujenga hoja sema toka umerudi CCM unazidi kujidhalilisha hadi CCM wenyewe wanakudharau.

Shame on you scumbag
 
Halafu watu kama hawa waliong'oka ubongo ndio Magufuli anawapenda sana ili awaburuze , maana anaweza kuwatumia kama mashine tu , si unamuona Sabaya ?
 
Eti mahakama imekataa kutoa amri ya kuzuia kuapishwa kwa mbunge mtaturu!

Nigga!

Hicho kitu kimeongelewa hili shauri la juzi?

Hilo limo kwenye kesi ya msingi!

Na kesi ya msingi bado haijaongelewa!

Sasa sijui unazungumzia kesi ya msingi kwa sababu gani?

Una vituko aisee!

Mmeshachanganyikiwa tayari!
 
Back
Top Bottom