Kesi ya Tundu Lissu sio ya kushangilia

Kesi ya Tundu Lissu sio ya kushangilia

LISSU BADO HAJAKWAMUA KISIKI KUZUIA KUAPISHWA KWA MHE. MTATURU...

Kuna upotoshaji unaendelea kwenye mitandano kuhusu maamuzi ya Mahakama juu ya mapingamizi ya Serikali kwenye kesi iliyofunguliwa na Tundu Lissu dhidi ya Mhe.Spika.

Ifahamike kuwa:

1.Tundu Lissu aliwasilisha maombi ya kibali (Leave) cha Mahakama Kuu kuruhusiwa kufungua maombi ya Kiutawala (Judicial Review) kupinga uamuzi wa Mhe. Spika kumvua ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambapo tayari kuna Mbunge ameshachaguliwa na anasubiri tu kuapishwa (Mhe. Miraji Mtaturu).

2. Lissu katika ombi lake la msingi kaomba kuzuia kuapishwa kwa mbunge huyo anataka Mahakama itamke kuwa uamuzi huo ulikuwa batili. Hata hivyo, ubunge wake ulikoma kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(c) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

3. Lissu ameomba kupatiwa uamuzi wa Spika wa kumwondolea Ubunge kama ulichapishwa kwenye Gazeti la Serikali. Maombi hayo ameleta kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi sura Toleo la 2015.

4. Kilichojiri Mahakamani leo tarehe 26.08.2019 pamoja na baadhi ya mapingamizi ys utetezi kutokubalika:

(i). Mahakama imeafikiana na hoja za Upande wa Utetezi kuwa kuna mapungufu katika hati za viapo vilivyowasilishwa na upande wa Lissu hivyo kuviondoa vipengele vyote kwenye viapo hivyo.

(ii). Mahakama imekataa kutoa Amri yoyote ya kuzuia kuapishwa kwa Mbunge Mteule mpaka itakaposikiliza pande zote mbili.

(iii) Mahakama imetaka pande zote mbili zikawasilishe hoja zao kuhusu maombi ya kibali cha kuomba mapitio ya uamuzi wa Mhe. Spika tarehe 02.08.2019.

KWA UAMUZI HUO, NI WAZI KUWA NGOMA HAIJAISHA IPO PALE PALE.....
Ulisoma shule gani ya sheria mkuu?
 
Mimi nimeanza kumuona 2013 au 2014 akiwa uvccm tena watu wakadai si mchicha mwiba humuhumu jf
Alikuwaha Rais wa wanafunzi UDOM, enzi hizo migomo kibao alikua kamanda haswaa yaani aliwapa muda mgumu sana CCM kwa nondo zake. Then alikuwa nominated apewe uenyekiti BAVICHA taifa ila hakufanikiwa, then 2015 akawa amejiandaa kugombea jimbo la Lupa huko mbeya, alikatwa akahamia ACT na alianguka vibaya mno naona akaamua kusahau yote CCM waliomtendea akaenda kujiunga nao.

Kinachohuzunisha alipokua CHADEMA alikua anaongea nondo mno kuhusu uwajibikaji wa serikali lakini toka amerudi CCM kazi yake ni kutukana,kukosoa upinzani ilimradi apate uteuzi.

Inasikitisha sana
 
LISSU BADO HAJAKWAMUA KISIKI KUZUIA KUAPISHWA KWA MHE. MTATURU...

Kuna upotoshaji unaendelea kwenye mitandano kuhusu maamuzi ya Mahakama juu ya mapingamizi ya Serikali kwenye kesi iliyofunguliwa na Tundu Lissu dhidi ya Mhe.Spika.

Ifahamike kuwa:

1.Tundu Lissu aliwasilisha maombi ya kibali (Leave) cha Mahakama Kuu kuruhusiwa kufungua maombi ya Kiutawala (Judicial Review) kupinga uamuzi wa Mhe. Spika kumvua ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambapo tayari kuna Mbunge ameshachaguliwa na anasubiri tu kuapishwa (Mhe. Miraji Mtaturu).

2. Lissu katika ombi lake la msingi kaomba kuzuia kuapishwa kwa mbunge huyo anataka Mahakama itamke kuwa uamuzi huo ulikuwa batili. Hata hivyo, ubunge wake ulikoma kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(c) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

3. Lissu ameomba kupatiwa uamuzi wa Spika wa kumwondolea Ubunge kama ulichapishwa kwenye Gazeti la Serikali. Maombi hayo ameleta kwa mujibu wa kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi sura Toleo la 2015.

4. Kilichojiri Mahakamani leo tarehe 26.08.2019 pamoja na baadhi ya mapingamizi ys utetezi kutokubalika:

(i). Mahakama imeafikiana na hoja za Upande wa Utetezi kuwa kuna mapungufu katika hati za viapo vilivyowasilishwa na upande wa Lissu hivyo kuviondoa vipengele vyote kwenye viapo hivyo.

(ii). Mahakama imekataa kutoa Amri yoyote ya kuzuia kuapishwa kwa Mbunge Mteule mpaka itakaposikiliza pande zote mbili.

(iii) Mahakama imetaka pande zote mbili zikawasilishe hoja zao kuhusu maombi ya kibali cha kuomba mapitio ya uamuzi wa Mhe. Spika tarehe 02.08.2019.

KWA UAMUZI HUO, NI WAZI KUWA NGOMA HAIJAISHA IPO PALE PALE.....
Asante kwa taarifa
 
pumbavu hili
 
Hili swala la lissu Ni muhimu sana kisiasa na kisheria.mahakama inapaswa kuwa makini sana, haiwezekani mbunge aondolewe kienyeji vivo kisa wa upinzani.
Nakumbuka kuna mbunge alishinda uchaguzi akiwa kitandani mgonjwa na akaendelea kuwa mbunge hadi mola alipomuita
 
Mahakama zinatumika, hilo halina mjadala. Usidhani kwa huo uamuzi wa jana unatosha kuonyesha kwamba hawatumiki.
Hahah

Wewe ndugu yangu umekuwa against kila kitu nahisi utawala wa awamu ya tano ujafanya vitu vizuri vyote vibaya tu mkuu.

Kwaiyo vinatukimikaje?
 
Kwanini wasishangilie wakati serikali haitaki Lissu aendelee na kesi lkn mahakama imeamua kesi iwepo. Yaana wewe hutaki mashabiki washangilie gori lililofungwa dakika ya kwanza kisa bado kuna dakika 89 za mchezo. Hiyo ni akili kweli...!
 
Hahah

Wewe ndugu yangu umekuwa against kila kitu nahisi utawala wa awamu ya tano ujafanya vitu vizuri vyote vibaya tu mkuu.

Kwaiyo vinatukimikaje?

Umefanya mazuri kiasi chake hilo halina mjadala, ila kwangu hayo mazuri ni wajibu na sio hisani kama inavyotaka kugeuzwa sasa. Mahakama inatumika, hii haijalishi unakubali ama la.
 
Sijui mnyakyusa Wa Wapi huyu? Tukuyu,busokelo ,Kyela au ipinda
Hahahaha umenikumbusha mbali sana mkuu, ni maeneo mazuri sana haya ukiwa mbeya, ukiiondoa Kyela ambayo ina joto kama Dar es salaam
 
Hizi si ndio mahakama zikitoa maelezo tofauti na matakwa upande fulani zinasemwa zinatumika? Msije kuwa vinyonga mbele ya safari tu.
Mahakama zetu sina wakati mgumu sana. Wananchi wanajua ni kiasi gani wanavyoshinikizwa na wanasiasa. Maamuzi ya ndio dhidi ya wananchi huona wameshinikizwa. Maamuzi ya hapana huonekana wamehongwa. Ni shida.
 
Bunge litaendelea na taratibu zake haliwezi kwenda kwa kufuata taarifa za vyombo vya habari wala kinachoendelea mahakamani
Hapana kesi ilipangwa isikilizwe kwa mfululizo na kutolewa maamuzi ila CCM kwa kufahamu hilo wananunua muda kwa technicalities ili kesi iweze sogea hata kwa mwaka!!
Ila nachofahamu kma mahakama ikiona Lissu katolewa kimakosa itatakiwa nafasi yake irudishwe bila kujali kuna mtu kaapishwa au lah.
 
Back
Top Bottom