Kesi ya Seth na Rugemalira: Serikali haitendi haki

Mtu anatengeneza makampuni zaidi ya matatu ili akwapue fedha za masikini kina mama ntilie wanaochangishwa na serikali yao ,

Huu ubinafsi wa kiwango hiki haujapata onekana,

Na bado wanaachiwa huru.

Hao mafisadi wanaokwiba majasho ya watanzania masikini watayalipa tu,

Kama sio wao, ni vizazi vyao na watadaiwa hata mbinguni.

Nawashitakia mafisadi yote Kwa Mungu mkuu.
 
Hivi tangu lini DPP akabeba mamlaka ya mahakama?

Tulikaa kimya kwa sababu kesi ya Habinder Seth na Rugemalira ilikuwa bado mahakamani, huwezi kuongea lolote kesi inapokuwa mahakamani, kwa sababu mahakama ni sehemu ya Haki.

Eti Seth amekiri kwa DPP kwenye formal statement kwamba yeye ana makosa na kwa hiyo alipe Bil. 26 Kama faini.

Huu ni ujangili wa serikali kwa raia wake, yaani Serikali inapora pesa kwa nguvu ilizonazo dhidi ya watu wenye pesa.

Kwa wasiojua hii ishu ilianza kipindi cha Hayati Magufuli, si tu Seth na Rugemalira bali watuhumiwa wengi wenye ukwasi mkubwa waliokuwa mahabusu walishurutishwa kukiri makosa yao kwa maandishi ili walipe faini na kutoka mahabusu.

Baadhi walifuata masharti hayo ya kijangili ya Serikali na walilipa faini na kutoka.

Seth na Rugemalira waligoma wakitaka haki itende Mahakamani, yaani mahakama ndo iamue endapo wana hatia au la.

Msimamo wao huo uliwaponza na kesi yao ilianza kupigwa Tarehe na kuwafanya wazidi kuteseka mahabusu.

Taarifa za uhakika nilizonazo kutoka familia ya Seth zinadai kwamba, ndugu wa Seth (wanafamilia na jumuiya za kisingasinga) waliona isiwe tabu, haijulikani lini mahakama itatoa haki,kwa kuwa pesa hutafutwa na uhai hautafutwi,waliona bora walipe pesa ili yaishe, Kama ujangili ni nini hicho?

Malipo ni hapa hapa Duniani, serikali ya CCM kazaneni kuonea watu, before you pay the price, and your time has drawn nigh....

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Watu wanaonewa sana na hii Serikali
 
Back
Top Bottom