Kesi ya Sabaya ya uhujumu uchumi yaahirishwa kwa mara ya 10 leo Oktoba 10, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya imeahirishwa kwa mara ya 10, leo Oktoba 10, huku Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Kassim Nassir akiileza mahakama hiyo kuwa upelelezi wake utakamilika ndani ya siku 90.

Sabaya na wenzake wanne walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kwa mara ya kwanza Juni Mosi, 2022 wakikabiliwa na mashitaka 7 ikiwemo uhujumu uchumi, ambapo leo Oktoba 10 anatimiza siku 132 akiwa mahabusu.

Hata hivyo, Septemba 6, 2022 Mahakama hiyo iliwaachia huru washitakiwa wanne ambao ni Sylivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey, baada ya kukiri makosa yao na mahakama kuwahumu kulipa kila mmoja faini ya Tsh. 50,000 na fidia ya Tsh. 1 milioni kwa mwathirika wa tukio hilo ambaye ni Alex Swai.

Oktoba 10, Wakili wa upande wa utetezi, Hellen Mahuna aliileza mahakama hiyo kuwa kesi inayomkabili mteja wake ambaye ni Sabaya imekaa kwa siku 132 bila upande wa mashitaka kueleza chochote kinachoeleweka zaidi ya kusema upelelezi bado haujakamilika.

Hivyo, Wakili Mahuna akaiomba mahakama hiyo iangalie na itumie hekima na muongozo uliotolewa na Mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP) ya kwamba upelelezi unatakiwa ukamilike ndani ya siku 90.

"Kesi hii imekaa kwa siku 132 na upande wa mashitaka hawajatuambia chochote kinachoeleweka zaidi ya kutuambia kwamba upelelezi haujakamilika.

“Wanachokifanya ni kinyume na mwongozo waliopewa na DPP na kwamba wamekuwa hawakamilishi upelelezi kwa wakati na wanamweka mshatkiwa ndani na kumnyima haki zake za msingi," amesema.

Wakili Mahuna pia ameieleza mahakama hiyo kuwa kama kuna jambo upande wa mashitaka wanatakiwa kulifanya kutokana na mwongozo wa DPP walifanye na wasitegemee kwamba mwongozo umekaa siku 10 tu waangalie siku shauri hilo lilipofikishwa mahakamani.

Kwa upande wake Mwendesha mashitaka wa Serikali, Kassim Nassir ameieleza mahakama hiyo kuwa, kwa kuwa mwongozo huo umeanza kutumika Oktoba mosi 2022 na kwamba ni siku 10 tu zimepita upelelezi wa shauri hilo utakamilika ndani ya siku 90.

"Tangu mwongozo huo umeanza kutumika Oktoba mosi 2022 ni siku 10 tu zimepita, kwa hiyo siku 90 bado hazijaisha ,upelelezi wa shauri hili utakamilika ndani ya siku 90 kama mwongozo unavyoelekeza," amesema.

Hakimu Mshasha ameiahirisha kesi hiyo mpaka Oktoba 24, 2022 itakapotajwa tena na kwamba mshitakiwa ataendelea kuwa chini ya ulinzi wa Magereza akisubiri upelelezi utakapo kamilika.

Chanzo: Mwananchi
 
Ni dalili ya yeye kuachiwa
 
Chadema ni wanafiki sana.

Huwa wanajinasibu kutetea wanyonge kwani Sabaya haonewi hapo alipo??
 
kesi ya mchongo ukiona kesi inaahirishwa mara nyingi ujue hawana ushahidi ni uonevu tu
 
Back
Top Bottom