Kesi ya Sabaya: Video kutoka Benki zikionesha maboksi yenye fedha alizoomba Sabaya zawasilishwa Mahakamani

Hivi hatuez pata video Kama hizi za Bashite nae akamsaidie mwenzake kule. Hebu wadau wenye ushahidi tuukusanye tupate mawakili wa kutusaidia tujenge Tanzania yenye nidhamu
Ina maana CRDB haina siri kwa wateja wake?
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imepokea video sita zilizokuwa kwenye ‘flash disk’ iliyowasilishwa kama ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya, Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Wiki iliyopita, upande wa utetezi ulipinga kupokelewa kwa video hizo kama ushahidi katika kesi hiyo lakini baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote, imekubali kuzipokea.

Katika video hizo, watu wawili wanaonekana wakiingia katika benki ya CRDB tawi la kwa Morombo mkoani Arusha na kuchukua maburungutu ya fedha ambazo ziliwekwa kwenye maboksi.

Afisa wa benki alionekana akiwa ameshika maboksi mkononi kabla ya kuanza kuhakiki fedha hizo na kuzipanga kwenye maboksi, kisha aliziweka juu ya kiziti chenye matairi na kwenda kuwakabidhi watu hao wawili.

Watu hao ambao mmoja anaonekana ni mtu wa makamo aliyevaa koti kubwa na mwingine ni kijana, walichukua maboksi hayo yenye fedha na kwenda kuingia nayo kwenye gari la bluu.

Video hizo zilitolewa kama sehemu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri kupitia shahidi wake wa nne, Jonson Kisaka.
Attach hiyo video tuone mkuu
 
Alikuwa akitekeleza maagizo ya ibilisi joka kuu akasahau kuwa yupo Mungu wa Isaka na Yakobo mtengeneza njia pasipo na njia.
 
Sabaya kila kitu majukwaani ni kumtaja mungu tuu, na yule makonda ndio kujifanya wanachukia madawa, mashoga na mpaka kuimba mapambio jukwaani, kumbe walikuwa wachafu kweli kweli kuliko hao fake wauza madawa ya kulevya waliowasingizia
 
Huwezi kutenga wizi wa sabaya na utawala wa magufuli. Kwa kifupi huo wizi alitumwa na magufuli..
Nitakapokuwa rais mwaka 2035 nitaishangaza dunia,awamu ya tano ya sita watakuwa na kesi ya kujibu,Kuna watu watakuwa kama Mbowe wa leo.
Nitakata kujua aliyemshambulia Lissu/kupotea baadhi ya watu.
Nitataka kujua Kigogo ni nani na kwanini alifurahia sana kifo cha Magufuli.
Jiandaeni mwaka 2035 sio mbali.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imepokea video sita zilizokuwa kwenye ‘flash disk’ iliyowasilishwa kama ushahidi wa upande wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya, Lengai Ole Sabaya na wenzake.

Wiki iliyopita, upande wa utetezi ulipinga kupokelewa kwa video hizo kama ushahidi katika kesi hiyo lakini baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote, imekubali kuzipokea.

Katika video hizo, watu wawili wanaonekana wakiingia katika benki ya CRDB tawi la kwa Morombo mkoani Arusha na kuchukua maburungutu ya fedha ambazo ziliwekwa kwenye maboksi.

Afisa wa benki alionekana akiwa ameshika maboksi mkononi kabla ya kuanza kuhakiki fedha hizo na kuzipanga kwenye maboksi, kisha aliziweka juu ya kiziti chenye matairi na kwenda kuwakabidhi watu hao wawili.

Watu hao ambao mmoja anaonekana ni mtu wa makamo aliyevaa koti kubwa na mwingine ni kijana, walichukua maboksi hayo yenye fedha na kwenda kuingia nayo kwenye gari la bluu.

Video hizo zilitolewa kama sehemu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri kupitia shahidi wake wa nne, Jonson Kisaka.
Kazi ipo
 
Back
Top Bottom