Mfanyakazi wa Vodacom aeleza alivyochunguza Simu za Sabaya

Siku wavute Logs za Simu aliyokuwa anatumia Mwendakuzimu tutabaki Midomo wazi
 
Hivi huko mahakamani wakili wa mtuhumiwa ushahidi wa wazi ukiletwa mezani na usiokua na shaka hua anafanyeje? Anabisha tu kama huku mtaani kwetu au anakubali? Na akikubali si ni kama amemsaliti mteja wake?
Mawakili ni majizi yapo kibiashara zaidi. Yanajua kabisa unafungwa ila wanakukamua hadi senti ya mwisho.

Dawa malipo yafanyike baada ya kesi kwisha na uwe umeshinda.
 
Nauliza tu, sitetei uhalifu!!

Mashirika ya simu hayana privacy kwa wateja wao, kama mitandao ya nchi nyingine i.e USA etc?
... yaani ufanye uhalifu halafu makampuni ya simu yakupe privacy?
 
Mara nyingi ushahidi wa simu hautumiki katika maamuzi hata kama umekubaliwa.Kwani ni lazima simu ikisoma mnara wa mtaa fulani basi na mimi nitakuwepo hapo?Uthibitisho wa sauti ni mgumu kwani kuna watu wana vipaji kuiga sauti za watu...mwishoni unakuwa ushahidi wenye shaka
 
Kweli Watanzania akili zenu wengi zimelala
Hakuna kampuni Iko juu ya sheria
Ikifikia Serikali kutaka ushahidi Kwa sababu za kiusalama ni lazima kupewa ushirikiano sio ombi.
Utafichiwa Siri tu laiti ukiwa raia mwema
Chukua tahadhari kuanzia Leo kama ulitegemea simu kufanya uhalifu Ujue hauko salama.
 
Mara nyingi ushahidi wa simu hautumiki katika maamuzi hata kama umekubaliwa.Kwani ni lazima simu ikisoma mnara wa mtaa fulani basi na mimi nitakuwepo hapo?Uthibitisho wa sauti ni mgumu kwani kuna watu wana vipaji kuiga sauti za watu...mwishoni unakuwa ushahidi wenye shaka
Sms mkuu ndo evidence inayokubalika kwetu hapa ni sms na transactions tu na siyo call logs, call logs ni katika kutambua tu kuwa x, y na z walikuwa na mawasiliano na walisomeka wapi so mambo mazuri tuendelee kuwa makini na simu zetu
 
Ujinga mwingi sana humu Mkuu
Ngoja tukufahamishe kidogo ili uache mambo ya kukalili

Unapozungumzoa Sera za faragha za mteja (customer privacy) sio kwa service provider company pekeee, hio ni kwa kila kampuni lazima iwe na Sera ya faragha za wateja wake ingawa zinatofautiana kutokana na huduma inayotolewa na kampuni husika...
Acheni kukalili 3+2=5 nikitu kilekile ukisema 2+3=5. Utofauti wake ni kwamba kwenye swali no 1 tumeanza na 3 lakini kwenye swali la pili tumeanza na 2.
 
Back
Top Bottom