GE2025 Kesi ya Mgawanyo wa Mali CHADEMA imeahirishwa hadi Agosti 7, 2025

GE2025 Kesi ya Mgawanyo wa Mali CHADEMA imeahirishwa hadi Agosti 7, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Baada ya Jaji Hamidu Mwanga kusikiliza hoja za ombi la kutaka ajitoe kwenye Kesi namba 8323/2025 ambayo imetoa zuio la muda kwa Chama cha Chadema kufanya shughuli zozote zile kiutendaji na oparesheni, uamuzi wake unatarajiwa kutolewa Julai 28, 2025.

Kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Issa Mohammed dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chadema na Katibu Mkuu.Ambapo waleta maombi waliwasilisha madai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali za Chama.

Ikumbukwe Julai 14, 2025 walioleta ombi hilo Mahakamani ambao Bodi ya Wadhamini ya Chadema na Katibu Mkuu walitoa hoja Mahakamani kuwa hawana imani na Jaji huyo kutoka na mienendo ya uamuzi mbalimbali ambao amekuwa akiutoa kwenye shauri hilo.

Akisoma hoja Mahakamani Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema kuwa Mh. Jaji Mwanga ana mgongano wa maslahi anatumika kuwahujumu.

Aidha alieleza Makama kuwa uamuzi wa kutoa zuio la kusitisha shughuli za kisiasa kwa muda, kuwa unaenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini alisema kuwa uamuzi huo unaweka hatarini mali za Chama kuporwa au kuibiwa kutokana na kukosekana kwa mamlaka za usimamizi.
photo_2025-07-28_10-01-36.jpg

photo_2025-07-28_10-01-34.jpg


photo_2025-07-28_10-01-32.jpg
Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, akizungumza na waandishi wa habari katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam, amesikitishwa na uamuzi wa Jaji kukataa kujiondoa kwenye kesi ya mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na viongozi wa zamani wa CHADEMA upande wa Zanzibar dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa chama.

Mnyika ameendelea kumtaka Jaji huyo ajiondoe kwa madai ya mgongano wa kimaslahi, huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Agosti 7, 2025.




 
Huyu hatajitoa kwa sababu ni mission kutoka kwa watawala, tena wa juu kabisa.
 
Unajidai unakubalika kisha unaogopa kushindanishwa.?
 
Back
Top Bottom