Kesi ya Mbowe inalichafua Taifa na kuzidisha ugumu kwenye ulinzi

Katika hali ya kawaida watanzania wanafikishwa mahali pabaya na utawala wa CCM. Kuibinya demokrasia kwenye taifa kunasababisha taifa kupata raia wakakamavu sana bila sababu.

Utawala wa makaburu, wareno, Idd Amin, au Gadaffi ulizaa raia wakakamavu sana kwenye mataifa hayo.

Kazi ya ulinzi inakuwa ngumu sana kama Serikali inayotawala ikiiminya demokrasia ya wazi. Hii inasababisha hata magaidi kupata sehemu za kufikia kiurahisi sana ndani ya nchi, kunasababisha vyama vya upinzani na waumini wa mabadiliko kujaa fukuto kwenye ubongo wao.

Kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa nchini na mambo yanayofanyika kwenye chaguzi sio afya kwa ulinzi na usalama wa taifa katika zama hizi.

Hakuna ubishi kuwa demokrasia ya aina hii inatoa kazi ya ziada kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama nchini. Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wapeni angalizo wanasiasa kuhusu aina hii ya demokrasia katika zama hizi za utandawaazi.

Ni wazi kuwa aina hii ya demokrasia itazaa akina mbowe wengi sana. Ni ukweli kuwa kesi hii itakwenda hadi 2025 ili wapinzani wawe bize na kesi badala ya kuimarisha demokrasia nchini.

Kama hukumu itatolewa mwezi July 2025 na uchaguzi ukawa October 2025 Kutakuwa na nini tena hapo?

Nionavyo Mimi sisi tunapita lakini Taifa halipiti, taifa ni kubwa kuliko mtu au kikundi, tuifikirie zaidi Tanzania kuliko madaraka na kundi, maana Iko siku historia yetu itaandikwa upya, IPO siku Mali zitagawanywa upya kwa usawa, nyumba yako iko siku itageuka kuwa hostel ya wanafunzi kutokana na ulivyoipata Leo, hata punje moja ya wizi itarejea kwa wenyewe.
Unatangaza Utalii, unaita wawekezaji wwkati huo huo unasema kuna magaidi
 
Huo ugaidi uliorindima jana huko kwa M7 uwe fundisho ukigeuka kipande hiki na kule kwa bunge ako hao mavilaza tuu we will shidaaaa for sure
 
Unatangaza Utalii, unaita wawekezaji wwkati huo huo unasema kuna magaidi
Wanazalisha jamii ambayo haitakubali kufia chini ya kitanda. Kuna watu ambao tangu mwaka 1992 wanahangaikia demokrasia kwa njia za wazi lakini imeshindikana, watu hawa walikuwepo, wapo na watakuwepo. Sina uhakika na idadi yao kama inaongezeka au inapungua, na mbinu wanzozitumia kudai demokrasia zinabaki ZILE ZILE au zinabadilika.

It a matter of time yote yatafahamika.
 
Hivi inawezekanaje wagombea wote nchi nzima kuenguliwa wasigombee? Hapo dola inataka wananchi wafanye nini? Inawezekaje mtu ajitokeze na kudai hakuna siasa baada ya uchaguzj ambao aliyetangazwa kushindwa hahojiwi mahali popote duniani? Vyombo vya ulinzi na usalama wa taifa tusikae kimya mambo kama haya yanapojitokeza. Kazi yenu ni pamoja na kuzuia vyanzo vya uvunjifu wa Amani na utulivu kutoka ndani na nje ya mipaka.

Si kweli kwamba intelinjensia yetu haiwezi kunusa vitendo vya wanasiasa ambavyo vinakaribisha ugaidi ndani ya nchi. Kemeeni ili kazi yenu iwe na thamani hata mbele za mungu. Ni ujinga kusubiri hadi liharibike na Kuja kujutia kunyamaza kwako kmya wakati ulikuwa na nafasi ya kuzuia.
Hao ni makada wa CCM tupu mazee
 
Huo ugaidi uliorindima jana huko kwa M7 uwe fundisho ukigeuka kipande hiki na kule kwa bunge ako hao mavilaza tuu we will shidaaaa for sure
Sisi hatutaki ugaidi kwakuwa magaidi wanaua hata wasiohusika na madai yao. Lakini hakuna kisichokuwa na kiasi na ukomo, hata demokrasia kubinywa Kuna ukomo wake wa kuhimili, watu wanaodai demokrasi kumiminiwa risasi ni kupitiliza kipimo.
 
Back
Top Bottom