Kesi ya Mbowe inalichafua Taifa na kuzidisha ugumu kwenye ulinzi

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,233
12,508
Katika hali ya kawaida watanzania wanafikishwa mahali pabaya na utawala wa CCM. Kuibinya demokrasia kwenye taifa kunasababisha taifa kupata raia wakakamavu sana bila sababu.

Utawala wa makaburu, wareno, Idd Amin, au Gadaffi ulizaa raia wakakamavu sana kwenye mataifa hayo.

Kazi ya ulinzi inakuwa ngumu sana kama Serikali inayotawala ikiiminya demokrasia ya wazi. Hii inasababisha hata magaidi kupata sehemu za kufikia kiurahisi sana ndani ya nchi, kunasababisha vyama vya upinzani na waumini wa mabadiliko kujaa fukuto kwenye ubongo wao.

Kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa nchini na mambo yanayofanyika kwenye chaguzi sio afya kwa ulinzi na usalama wa taifa katika zama hizi.

Hakuna ubishi kuwa demokrasia ya aina hii inatoa kazi ya ziada kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama nchini. Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wapeni angalizo wanasiasa kuhusu aina hii ya demokrasia katika zama hizi za utandawaazi.

Ni wazi kuwa aina hii ya demokrasia itazaa akina mbowe wengi sana. Ni ukweli kuwa kesi hii itakwenda hadi 2025 ili wapinzani wawe bize na kesi badala ya kuimarisha demokrasia nchini.

Kama hukumu itatolewa mwezi July 2025 na uchaguzi ukawa October 2025 Kutakuwa na nini tena hapo?

Nionavyo Mimi sisi tunapita lakini Taifa halipiti, taifa ni kubwa kuliko mtu au kikundi, tuifikirie zaidi Tanzania kuliko madaraka na kundi, maana Iko siku historia yetu itaandikwa upya, IPO siku Mali zitagawanywa upya kwa usawa, nyumba yako iko siku itageuka kuwa hostel ya wanafunzi kutokana na ulivyoipata Leo, hata punje moja ya wizi itarejea kwa wenyewe.
 
Al Shabaab kuna siku watautumia mwanya wa nchi kujisingizia ina magaidi kufanya kweli. Watapiga tukio la kushangaza mbaki midomo wazi

Magaidi wakipiga tukio hujitokeza na kujitangaza.
 
Tusiombee huo Ugaidi husika uingie hapa Tz.
Tuache kujificha kwenye siasa tukishindwa kujibu hoja
 
Al Shabaab kuna siku watautumia mwanya wa nchi kujisingizia ina magaidi kufanya kweli. Watapiga tukio la kushangaza mbaki midomo wazi
Kule Uganda mlipuko wa jana ungeenda vizuri Wabunge wote ea Mseveni wangeteketea.

Waache utani na ugaidi
 
Hakuna mtu au kundi moja litafanikiwa kuimiliki nchi milele, nchi ni mali ya wananchi wote wa nchi husika. Mifumo yote ya kidemokrasia na ulinzi wa taifa iruhusu hili kutendeka.

Pesa nyingi sana ambazo zingetumika katika kuwaletea wananchi maendeleo yao zitatumika kwaajili ya kulinda kundi linalojitafutia maadui makusudi ililiendelee kubaki madarakani. Utawala wa aina hii unaifilisi nchi, maana lazima uwe na askari wengi zaidi wa kuwalinda na silaha nyingi na kali zaidi. Hii sio Sawa, maana fedha nyingi sana itatumika katika ulinzi wa ndani na nje ya mipaka. Kwanini tufike huko
 
Hivi hawa watu hawana hofu ya Mungu?
Wanajua kiyama chao kweli?
Kufanya haya wanayofanya hawa 'watesi' wa Mbowe inatakiwa uwe katili kuliko shetani mwenyewe.
Ole wenu nyie na vizazi vyenu maana laana ya ukatili huu itawatafuna hadi jehenam!
 
Naona Zanzibar inaipeleka puta Tanganyika.

Akina Sabaya wa Zanzibar (walioualwa na kujeruhi wakati wa uchaguzi mkuu) wao wanakula kuku wakati huku wanaozea jela.
 
Hivi inawezekanaje wagombea wote nchi nzima kuenguliwa wasigombee? Hapo dola inataka wananchi wafanye nini? Inawezekaje mtu ajitokeze na kudai hakuna siasa baada ya uchaguzj ambao aliyetangazwa kushindwa hahojiwi mahali popote duniani? Vyombo vya ulinzi na usalama wa taifa tusikae kimya mambo kama haya yanapojitokeza. Kazi yenu ni pamoja na kuzuia vyanzo vya uvunjifu wa Amani na utulivu kutoka ndani na nje ya mipaka.

Si kweli kwamba intelinjensia yetu haiwezi kunusa vitendo vya wanasiasa ambavyo vinakaribisha ugaidi ndani ya nchi. Kemeeni ili kazi yenu iwe na thamani hata mbele za mungu. Ni ujinga kusubiri hadi liharibike na Kuja kujutia kunyamaza kwako kmya wakati ulikuwa na nafasi ya kuzuia.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom