Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa katika viunga vya Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakati Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu akifikishwa mahakamani hapo.
Yaliyojiri Mahakamani;
Mahakama imeanza, nitawaletea update za kesi hii ya uhaini dhidi ya Lissu ambapo jana tuliishia sehemu ya 222.
Sehemu ya 223
Majaji wameingia na Mshitakiwa pia ameingia.
Karani anasoma shauri hapa.
Anasimama Renatus Mkude anasema yupo na Ajuaye, Katuga, Thawabu, Cathbert Mbiringe.
Anasema leo tumekuja kwa ajili ya kupokea ruling na sisi tuko tayari.
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa unasemaje?
Lissu: Na mimi niko tayari.
Jaji anaanza kusoma hapa UAMUZI.
Uamuzi huu unatokana na pingamizi lililowekwa na pingamizi la mshitakiwa kutokana na taarifa ya kuongezwa kwa ushahidi.
Taarifa hiyo ililetwa tarehe 18/02/2026 na upande wa Mashitaka kwamba unatokana na pingamizi lililowasilishwa na mshitakiwa.
Notice hiyo ililetwa kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA.
Mshitakiwa alieleza Mahakama kwamba kifungu hicho kinaelezea shahidi ambae maelezo yake hayakusomwa wakati wa mwenendo kabidhi na hivyo walichokileta upande wa mashitaka ni kuleta ushahidi mpya.
Upande wa mashitaka walijibu notice ipo halali kwa mujibu wa sheria na imekibidhi matakwa ya kisheria na ipo kwa mujibu wa sheria.
Huo ndio ulikuwa msingi wa hoja za pande zote mbili.
Mahakama imeona hoja inayopaswa kuamuliwa ni je notice hiyo ipo kwa mujibu wa sheria?
Ili kurahisisha Mahakama imeona ili reproduce notice hiyo inavyosema.
Anasoma notice inavyosema kwamba ni notice ya kuongeza maelezo ya ziada ya shahidi husika ambae ni Amin Mahamba.
Hakuna mashaka kwamba upande wa mashitaka wanataka kuongeza ushahidi wa Amin Mahamba.
Kwa vile Amin Mahamba ni shahidi na statement yake ilishasomwa wakati wa committal ilishasomwa.
Notice inasema ushahidi unaotaka kuletwa ni wakati wa uchaguzi wa tar. 29/10/2026.
Anasoma kifungu cha 308 cha CPA kinavyosema.
Ukiangalia kifungu hicho kinatoa masharti au mazingira ambayo notice hiyo ni reasonable au laaa.
Masharti ni kwamba
1. Maelezo yatoke kwa shahidi
2. Uwe ni ule ushahidi ambao haukusomwa wakati wa committal
3. Uwe ni ushahidi ambao haukusomwa wakati wa proceedings
Kifungu cha 308 ndio kinachosema hawezi kutoa ushahidi hadi watakapoleta notice na hivyo basi ukiangalia hayo kifungu hicho cha 308 kinafungua mlango kwa shahidi ambae alikuwepo na bahati mbaya maelezo yake hayakuletwa.
Amin Mahamba maelezo yake yalikuwepo wakati wa commital, anataka kuleta mambo ya Uchaguzi ambayo hayakuwepo wakati wa committal.
Ipo kinyume na kifungu cha 308 cha CPA.
Hivyo basi kifungu cha 308 kinaweza kuruhusu notice hiyo tumeona kwamba kifungu hicho hakiruhusu kabisa.
Shauri la Remina Omary Abdul tumeona linahusiana na vielelezo vya wakati wa committal. Shauri hilo haliwezi kutibu chochote katika hoja iliyopo mbele yetu.
Hiyo notice ya kuongezwa kwa ushahidi ambayo imeletwa na upande wa mashitaka haitambuliwi na kifungu cha 308 cha CPA.
Kimsingi tunasema kwamba fundamentally haiko sahihi na baada ya kusema hayo basi notice hiyo ni incompetent na tiba pekeee iliyopo ni kwamba notice hiyo lazima iwe struck out. Ni hayo tu.
Anasimaa. RENATUS MKUDE anasema baada ya kupokea ruling tunatafakari tunaomba ahirisho ya lisaa limoja.
Twende kutafakari.
Bado majaji wanashauriana pale juu.
Anasimama Lissu anasema mmesema kuwa mashahidi waletwe leo na mlisema tutasikiliza uamuzi wa pingamizi na tutasikiliza shauri leo.
Sasa wanasema tuahirishe kusikiliza ili wakatafakari.
Wanaenda kutafakari nini? Ili iweje? Huu uamuzi haukatiwi rufaa.
Tusipoteze muda kila tunapopoteza muda anayeumia ni mimi sasa wao walipaswa kuleta mashahidi na wasitupotezee muda kabisa, tuendelee kusikiliza shauri hili.
Majaji wanaandika kidogo
Anasimama Renatus Mkude anasema tumemsikia Mshitakiwa
Tuna mambo mawili.
1. Tumepokea ruling ya Mahakama na tumeikubali
2. Jambo la pili ni kwamba tulimtaja shahidi ambaye lazima tuweze kumuandaa shahidi yetu
Jaji Ndunguru anasema tulisema muwe na mashahidi wakutosha. Tukiendelea kubishana tutapoteza muda, turudi mahakaman saa 5 kamili
===
Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam ikubalinana na pingamizi la Mshtakiwa Tundu Lissu kwenye Kesi ya uhaini inayomkabili, ambapo imekataa kupokea notisi ya kuongeza kiini cha shahidi (substance of evidence) iliyowasilishwa na Jamhuri Februari 18, 2026.
Mahakama imesema haikuwa notisi kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, hivyo notisi hiyo imetupiliwa mbali.
Februari 23, 2026 Lissu aliwasilisha pingamizi Mahakamani akipinga ombi la Jamhuri kutaka notice hiyo kupokelewa, ambapo Lissu alielezea kwamba notisi hiyo inakiuka matakwa ya kisheria. Jamhuri nao walieleza kuwa notisi hiyo inakidhi matakwa ya kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Katika hoja zake Lissu alieleza, kuwa ushahidi wanaotaka kuuleta Jamhuri unahusiana na upelelezi wa makosa yaliyofanyika wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Katika kutoa uamuzi wake Mahakama imeeleza kuwa imepitia notisi hiyo na kuona kuwa Jamhuri wanataka kuongeza Ushahidi wa ACP Amini Mahamba ambaye maelezo yake yalisomwa wakati wa mwenendo wa ukabidhi na kumbukumbu za Mahakama Kuu wakati wa kusomwa kwa hoja za awali. Umekubaliana na hoja aliyoitoa Lissu kuwa ushahidi unaotaka kuleta unahusiana na yaliyofanyika wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Kifungu cha 308 kinamaansha kuwa Ushahidi huo lazima uwe haukusomwa wakati wa mwenendo wa ukabidhi. Kifungu hicho kinafungua mlango kwa shahidi ambaye maelezo ya shahidi au Ushahidi wake haukusomwa wakati wa mwenendo wa ukabidhi.
Mahakama imerejea baada ya Mawakili wa Jamhuri kuchelewa kurudi kwenye chumba cha Mahakamani kuendelea na Kesi
Sehemu ya 224
Majaji wameingia muda huu saa nane Kamili Mchana.
Wanaandika pale juu.
Lissu ameingia na kuteta jambo na Dr. Nshala tunamsikia anasema waende kokote watakapotaka kwenda tutakutana nao huko. Sasa sijui ni wapi anamaanisha.
Anasimama Renatus Mkude Wakili wa Serikali kwa niaba ya jopo la Mawakili wa Serikali tunaomba radhi kwani tulifikiri tungetumia lisaa limoja.
Mchana huu nipo na Ajuaye, Thawabu Issa na Cathbert Mbiringe. Kwa wote tunawakilisha jamhuri na Mshitakiwa yupo.
Shauri lilipangwa kuendelea na mashahidi. Lakini tumetafakari na tunaitafsiri kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha Appellate Jurisdiction Act na kanuni ya 65(1) ya kanuni za Mahakama ya Rufani.
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) anatoa taarifa ya kuwasilisha taarifa ya mapitio (revision)
Anaendelea hapa Renatus Mkude, kuwa Notice of motion hiyo imeambatanishwa na kiapo cha Cathbert Mbiringe Wakili wa Serikali ambayo taarifa hii ya kutoa notice kwenda Mahakama ya Rufani imesainiwa leo Tar. 24/02/2026.
Na kupokelewa kwa mifumo ya kielektroniki inayotambulika na Mahakama na kusajili kama. CRIMINAL REVISION NO. 7203216/2026 imepokelewa na Mahakama ya Rufani Tanzania hapa Dar es salaam.
Ambalo chimbuko lake ni Criminal Sessions No. 19605/2025 ambayo iko mbele yenu Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu. (Ndunguru, Karyemaha, Kiwonde)
Kwa kuwa shahidi wetu aliyekuwa anafuata ACP Mahamba tuliyemuombea notice additional substamce of evidence na ikakataliwa.
Ni Rai yetu kwamba kwa kuwa shauri hili limeshapokelewa Mahakama ya Rufani haiwezi kusimama ili kuweza kutoa nafasi kwa shauri husika huko Mahakama ya Rufani kuweza kuamuliwa.
Ni hayo tu kwa sasa.
Tunamsubiri Lissu atajibu nini?
Lissu anaanza.
Baada ya kuzikiliza wasilisho la upande wa Mashitaka nina haya ya kusema.
1. Kwa vile mimi nipo gerezani na wanajua nataka wanipatie hiyo nakala ya Notice of Motion waliyofile niweze kuiona.
2. Ninafahamu na ninatumaini na wao wanajua kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 8(2)(d) cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa ambacho wamekitaja (Appellate Jurisdiction Act) wanafahamu kwamba hakiruhusu rufaa wala mapitio wala marejeo ya maamuzi ya Mahakama ambayo hayamalizi shauri la msingi. (Interlocutory decisions) sina shaka na wao wanalifahamu hilo.
3. Waheshimiwa Majaji siwaombi mtoe uamuzi wowote kuhusu hili ninalolisema.
Nataka iwe kwenye record kwamba nafahamu na naamini upande wa mashitaka wanafahamu lengo la kupeleka ombi la marejeo Mahakama ya rufani na wanafahamu hairuhusiwi ni kurefusha mashauri haya ili niendelee kukaa Gerezani. Ni hilo tu.
Kwamba tupeleke Mahakama ya Rufani ili huyu mbaya wao ambae ni mimi aendelee kukaa Gerezani.
Kwa vile wananipeleka kwe ye Mahakama ya Rufani nataka niwaeleze kuwa nitawafuata huko huko naenda kuwashughulikia huko huko.
Kama ambavyo kesi yao is dead on arrival najua hata hii revision yao pia imeshakufa.
Tutarudi hapa yakiisha huko ya Mahakama ya rufani tutarejea hapa na nitawashughulikia tukirudi.
Jambo la Mwisho Mawakili wangu wametaka kunipa nyaraka hapa lakini siwezi kupewa hadi nyie mseme.
Sijui wanaogopa nini watu wa magereza nisipewe huo uamuzi hapo ni makaratasi tu.
Naambiwa ni hukumu kutoka huko Umoja Wa Mataifa lakini Magereza wanaogopa nisipewe.
Tena ni uamuzi unaohusiana na mimi kuwepo Gerezani. Tatizo liko wapi?
Jaji anasema uko wapi? Umepelekwa wameuona wamesema wape Mawakili wa Serikali.
Wako wanasoma hapa Mawakili wa Serikali huo uamuzi.
Anasimama Renatus Mkude anasema mimi ni member wa working group za UN Human Rights Council.
Jaji: Tumesema apewe au asipewe?
Renatus Mkude: Apewe tu.
Sehemu 225
Lissu anaendelea hapa.
Kama mtakumbuka nilisema ninavyoishi Ukonga, siruhusiwi kuonana na Mawakili wangu in private.
Mnaruhusiwa kutembelea Magereza naomba mliangalie na hili kama itawapendeza inawapa Mamlaka ya kutoa mapendekezo na mamlaka za Magereza kurekebisha masuala yanayohusu wafungwa kama haya niliyosema.
Ni muhimu kwamba kuwasiliana na washauri wangu wa kisheria ilindwe kama sheria inavyosema bila kusikilizwa na maafisa wa Magereza.
Ni hayo tu Waheshimiwa
Tundu Lissu amemaliza na amekaa sasa.
Majaji wanaandika hapa.
Anasimama Renatus Mkude kuwa tutampatia hizi nyaraka ndani ya siku 14 tutampatia.
Hili la masuala ya utawala wa mambo ya magereza kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha National Prosecution Act na sisi ofisi ya DPP tutatembelea ili kuhakisha kunakuwa na fair trial.
Wameombwa Majaji anasema DPP ataenda eti huko Magereza kuangalia haki za Mtuhumiwa. Uongo uongo uongo. Hawana hata aibu hawa jamaa.
Majaji wanaandika baada ya kusikia hayo kutoka kwa Wakili wa Serikali, Renatus Mkude.
Majaji wanajadili pale.
Yuko Jaji muda wote yeye huwa anacheka anafurahi tu sijui huwa anatabasamu jambo gani? Wanaofika hapa Mahakamani wanamfahamu vizuri.
Jaji Ndunguru: Tumesikia hoja za Jamhuri na Hoja za Mshitakiwa nae kama ambavyo mshitakiwa ameturahisishia kuwa mikono yetu imefungwa kwamba yapo hayo maombi ya marejeo Mahakama ya Rufani.
Sasa shauri hili linasimama hadi pale Mahakama ya Rufani itakapotoa uamuzi.
Suala la Gerezani wakili wa Serikali amesema na sisi pia tumelichukua.
Mwenendo wa shauri hili unasimama hadi pale mambo ya Court of Appeal yatakapoisha.
Kesi hii imeahirishwa hadi hapo itakapoitwa tena.
- Kesi ya Lissu: Mahakama kujadili ombi Jamhuri kuongeza ushahidi wa ziada leo Februari 23, 2026
- Lissu: Wanataka tuzungumze mambo ya Oktoba 29 mtakuwa mmefungulia balaa na isije ikawa shida