Kesi ya Kenya na Somalia huko ICJ; tuna lolote kujifunza kati yetu na Malawi?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Kuna usemi unasema mwenzio akinyolewa zako tia maji.

Kutokana na mwenendo wa kesi za kimataifa kuhusiana na mipaka inaonyesha mahakama na hata jumuiya ya kimataifa haina nguvu sana ya kulazimisha uamuzi wa mahakama.

Nilichojifunza ni kwamba kwenye mivutano yetu ya mipaka kinachoweza kukusaidia ni nguvu ulizo nazo.

Tukitegemea sana suluhisho la kidiplomasia tutalipoteza ziwa nyasa.
 
Maandiko yenyewe yanasomeka kutafuta amani kwa tabasamu haiwezekani, ukisoma Ezekieli 21 utaona.

Mtu anayekupiga kwa upanga huwezi kumuendea kwa tabasamu hata siku moja, dawa ni bita ni bita mura!.
 
Maandiko yenyewe yanasomeka kutafuta amani kwa tabasamu haiwezekani, ukisoma Ezekieli 21 utaona.

Mtu anayekupiga kwa upanga huwezi kumuendea kwa tabasamu hata siku moja, dawa ni bita ni bita mura!.
Aliye juu ya vyote alisema: tafuteni Aman na kila mtu.

Sasa hiyo amani utaipata vipi
ikiwa utamwendea na panga adui aliyekupiga ngumi ya sikio? 🤔🤔
 
Kama wanavyo jidanganya Zanzibar! Eti tukitengana nao watatakiwa kuchukua Mikoa ya Tanga, Dsm, Visiwa vya Rufiji, nk. Kwa sababu ya mikataba ya enzi hizo ya Sultan wao Seyyid Said na Wajerumani!

Kirahisi rahisi tu!!
 
Nimeangalia ramani ya Kenya Somali kabla ya mgogoro iko hivi ;
Screenshot_20211013-082315.png


Baada ya uamuzi wa ICJ imekuwa hivi;

Screenshot_20211013-082209.png



Kwa mtazamo wangu ICJ hawajaitendea haki Kenya kwa kuwa wamewapa kama 20% ya eneo gombaniwa (disputed area).

International riparian rights (law) ambayo ndiyo ilitumika kumaliza mgogoro wa Rasi ya Bakasi kati ya Cameroun na Nigeria, inasema nanukuu;

Riparian rights simply mean the rights bestowed on the people living along the banks of rivers. Riparian Rights are natural results that occur as rights because of residence in a specific. area. These are rights which belong to persons who live on a shore, bank or a river, ocean or lake.

Ndiyo maana hata kwa issue ya Lake Nyasa au kama Lake Malawi (kama wanavyoliita wenyewe Malawi), Tanzania haiwezi kupoteza haki yake.

Malawi wanatumia sababu za Kihistoria kuwa ni la kwao peke yao zinazotokana na Heligoland Treaty ya 1870 na uzembe wa Mkoloni Mwingereza ambaye Malawi ilikuwa colony lake na Tanzania ilikuwa trusteeship yake. Mwingereza akafanya uzembe kurekebisha mipaka hadi nchi zote 2 zikapata uhuru bila kurekebisha. Lakini Lake Nyasa ni mali ya nchi 3; Tanzania, Mozambique na Malawi.

Mpaka inakuwa exactly at the center of the lake
 
Hakuna mtu anayeweza kukubali ati kwenda kuoga kwenye Ziwa lazima awe na Tourist Visa.
... kuoga umeenda mbali sana Mkuu; kutuliza tu kiu ni lazima passport igongwe mhuri wa entry na exit! Mikataba waliyowekeana mabeberu kutunyang'anya haki yetu ya urithi tuliyopewa na Mungu ni batili kwa viwango vyovyote vile.
 
... kuoga umeenda mbali sana Mkuu; kutuliza tu kiu ni lazima passport igongwe mhuri wa entry na exit! Mikataba waliyowekeana mabeberu kutunyang'anya haki yetu ya urithi tuliyopewa na Mungu ni batili kwa viwango vyovyote vile.
Kwakweli bila Mabeberu pia tusingekuwa na haya Mataifa tungekuwa na Chiefdoms

Tatizo lingine ni sisi Waafrika,kuna kikao kimoja walichokaa wakuu wa Nchi za Kiafrika wakati huo OAU na kuazimia kuwa mipaka yote ilioachwa na Wakoloni isibadilishwe ibaki hivyohivyo tatizo linaanzia hapo.
 
Mtoa mada uko sahihi China na Japan kuna visiwa wanagombea Ila Japan hathubutu kumzingua China.

weee,zinadundwa kila siku huko na kila nchi ina majeshi yake ktk hicho kisiwa.

huu ugomvi wa mipaka kumbe sio kwenye site za ujenzi tuni mambo yako naturally.
 
Back
Top Bottom