Nyamgluu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2006
- 3,160
- 1,719
Naomba ufafanuzi wa hii skendo kwa wale waijuao. Je hii ni dalili ya nguvu mpya dhidi ya ujambazi au over confidence ya ma afande imezua soo!??
-------------------------------------------------------
Afande Zombe aunganishwa kwenye tela
Hatimaye aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Dar, Abdallah Zombe ameunganishwa katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini waliokamatwa maeneo ya Sinza jijini.
Afande Zombe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kwa mauaji ya watu wannne; Ephraim Sabinus Chigumbi, Sabinus Chigumbi Jongo, Juma Ngugu na Mathias Lunkombe.
Zombe hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo na alirejeshwa kule alikozoea kuwasweka wahalifu mbalimbali katika gereza la Ukonga kuunganishwa na watuhumiwa wengine wa mauaji hayo.
Wengine walioko sero na wanaoshtakiwa kwa kosa hilo hilo ni maaskari Polisi; Christopher Bageni, Ahmad Makelle, Noel, Jane Andrew, Nyangelera, Emmanuel Mabula, Felix Sandys Cedrick, Michale, Abeneth, Rashid Mahmoud Lema na Rajabu Hamisi Bakari.
Wengine wanaoendelea kusakwa na jeshi hilo ni CPL Saada Allawi, PC Frank, SSGT James na CPL Festus.
Tukio hilo liliibuka Januari 14 mwaka huu baada ya kutokea tukio la ujambazi maeneo ya Kariakoo na jeshi la polisi likiongozwa na Afande Zombe lilikurupuka na kuwakamata wafanyabiashara hao katika maeneo ya Sinza na kupotea nao.
Taarifa za polisi zilizotolewa jioni ya siku hiyo hiyo zilitonya kuwa watu hao walikuwa majambazi na wameuawa katika mpambano mkali wa kurushiana risasi.
Awali Afande Zombe alishikilia msimamo wake kuwa watu hao walikuwa majambazi pamoja na kuwepo na ushahidi wa watu kibao waliokuwa wanawafahamu marehemu na alikuwa amefungua kesi mahakamani kuvishtaki baadhi ya vyombo vya habari kwa kumpakazia na kumkashifu.
Kesi hiyo itasikilizwa tena June 16 mwaka huu.